Mbatia ni bora kuliko wanachama wote wasio wabunge wa CCM?


mikonomiwili

mikonomiwili

JF-Expert Member
Joined
Jan 11, 2011
Messages
274
Likes
1
Points
35
mikonomiwili

mikonomiwili

JF-Expert Member
Joined Jan 11, 2011
274 1 35
CCM ni chama cha sikunying ahapa Tanzania, ni chama ambocho kimeenea sehemu zote nchini kuliko chama kingine chochote na ni chama ambacho kinaaminika kua na wafuasi wengi kuliko vyama vyote Tanzania , pia ni chama ambacho kina vyanzo vingi vya hela kuliko vyama vyote Tanzania.

Pamoja na sifa zote hapo juu na nyingine nyingi hiki chama kinaonekana kukosa mwelekeo kwa kiwango kikubwa tena wakutisha.
sitaki kuamini kua eti kati ya wanachama wote wa ccm hakuna anaye weza kuteuliwa ubunge mpaka chama kikakope toka NCCR .
kunani huko NCCR?. Yaweza kua ni kwasababu ya mafanikio ccm iliopata baada ya kujiunga na CUF ndo maana wameamua kutengeneza kamseto ambako si rasmi.

wote tumeona matokeo ya muunganiko wa CUF na CCM pamoja na wanauita wa mafanikio lakini kwa kiwango kikubwa umeondoa upinza. Na sasa si CUF wala CCM anaye weza mkemea mwenzake kwani wote wana kula sahani moja. kwamaana hiyo basi CUF na CCM sasa ni chama kimoja huko visiwani.

ccm wana mbinu za hali ya juu sana kuwamaliza upinzani kisiasa na hii nikwaajili ya uchaguzi ujao, siosiri tena tumebakiwa na chama kimoja tu amabacho ndicho cha upinzani lakini vingine vimeshafuunga ndoa na ccm na vingine vipo njiani kufunga ndoa na ccm.

Nikwamasikitiko makubwa ninapenda kumwamwambia ndungu yangu Mabatia na wana NCCR wote kua mpaka sasa wameshindwa kuicheza karata ya ccm na wamejikuta wamefunga ndoa ambayo si ya lazima . Ninauhakika hii ndoa ita kiharibu chama cha NCCR kama wenzao wa CUF na sijui kama ni maamuzi ya chama ama ya Mbatia mwenyewe.

Si ni huyu huyu mbatia ali hama CCM kwambwewenyingi sana ??? iweje leo CCM imwone ana faa kuliko wanachama wote wa ccm. nasema tena huu nimchezo mchafu wa ccm wakudidmiza upinzani. Badala ya Mbatia kukaa na kujenga chama sasa ana enda tetea maslay ya CCM bungeni. Kwakua kachaguliwa na ccm ni lazima atakua upande wao. na ata sahau kabisa mambo ya chama hatimae chama kitakufa.

kwa upande mwingine hiinizarau kubwa kwa wanachama wa ccm kwakua alieondoka kwambwembwe na maneno mengi ameonekana ana faa kuliko hata walio kaa kwenye chama kwamuda wote na kuvumilia misukosuko yote iliopo ndani ya chama na sasa wanaonekana hawataweza isaidia tena ccm nibora waka kopa mtu nje. wana ccm mpoooo?


Mbatia kakubali uteuzi ili apate posho na kasahau kua alikua na kazi kubwa yakukijenga chama chake. Hili ni ni sawa na baba anaacha kujenga nyumbanikwake anaenda kujenga nyumba ya jirani huku yakwake ikiwa inavuja na kuendele kubomoka kwakasi kubwa. Mbatia hujawatendea haki wanachama wako na wana NCCR wote.

kunaswali najiuliza hapa hivi pale mjengoni ruzuku ya Mbatia itaenda kwenye chama chake ama itaenda CCM. hili sijalielewa vizuri na je mbatia atakaa upande wa upinzani ama ata kaa upande wa CCM? na je ikija hoja ya ccm kushindwa majukumu yake kama ilivyo tokea majuzijuzi je mbatia atakua upandegani ?
je kuna mwana NCCR yeyote bungeni ata weza kupinga hoja ya CCM bungeni kama tulivyo zoea? Hakika kunamaswali mengi ambayo hayana majibu na sijui tutayapalini ?

Ni vizuri Mbatia ukachukua na kadi ya CCM kabisa ili ikifika 2015 ugombee urahisi kwatiketi ya CCM hi ni kwasababu ccm hawatakua na mtu wakumsimamisha kugombea uraisi kama wamekosa wakumteua kua mbunge itawezekana vipi wapate wakumsimamisha kwenye nafasi ya uraisi?
Hongera mbatia kwakuonekana kua wewe ndo mtu safi kuliko wana CCM wote Tanzania na pia pole kwasababu umewageuka wanachama wako wote na hatimae umejiunga na chama ambacho walikikimbia .

Mwisho ni masikitiko makubwa serikali inatuambia haina hela, inashindwa kuwalipa waalimu na madactari na wafanyakazi wote vizuri lakini imeweza kuongeza wabunge na baraza la mawaziri kua kubwa zaidi ya lililopita. hii inamana mbaya sana kwa wananchi, Nisawa na baba aiambie familia yake kua hana hela ya mamtumizi lakini ana kaa baa kula na kunywa na kuagizia watu bia huku watoto wana lala njaa nyumbani.

Jamani tutumie kurayetu vizuri kuchagua angalau watu wanooweza fikiri kidogo.
 

Forum statistics

Threads 1,275,062
Members 490,894
Posts 30,531,839