Mbatia, Ndugai atafika mbele ya Bunge Februari kujiuzulu, ameanza kujiuzulu dhamana aliyokabidhiwa na chama kwa sababu hiki siyo kipindi cha Bunge

Jp Omuga

JF-Expert Member
Jan 16, 2012
6,052
2,000
Tunataka Katiba Mpya!
Changamoto zimekuwa mpya mpya. Huwezi tena kuzimanage kwa Katiba ya ccm ya 1997.

NB: Wakuu wa mihimili waache kujipendekeza pendekeza!!
 
kidereko

JF-Expert Member
Jun 13, 2021
888
1,000
Katiba inamtaka amuandikie barua ya taarifa Katibu wa Bunge. Haijataja kikao maalum cha Bunge. Na ofisi za Bunge ziko wazi siku zote.

Wabunge ataenda kuwaaga tu kama Spika wao. Ila atabaki nao kama mbunge wa kawaida.

Amefanya kiburi tu.

Amandla...
Mnajuaje Kama hajaandika kwenda kwa katibu wa bunge!?
 
Ukwaju

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
13,302
2,000
Watanzania wote sisi ni Mambumbu mpaka na Viongozi wetu
spika ameshajiuzulu tunakaa kubishana mpaka Katibu wa CCM anatangaza nafasi iwazi watakaa na kuteua jina lingine na kumpelekea Katibu wa Bunge wakati Katiba bado inafumba kuwa ni Bunge au Katibu
KOSA kubwa nianzie kwa CHADEMA NCCR ACT kwa Zitto na sisi
hiyo nafasi jamani ipo wazi kwa Watanzania kuchukua Fomu ya kugombea nafasi km Mtanzania binafsi (namkumbuka Marehemu N. Hezron Mhella alipambana na Spika Pius Msekwa na kupata kura nyingi tu pale Dodoma)
Leo Mbatia anakata rufaa Mnyika kanyamaza wakati CCM wanakimbiza jina lao ambalo litapita bila kupingwa na Wabunge
Pascal Mayalla tukachukue Fomu za Uspika safari hii tuachane na zile za Ubunge
naipitia Katiba Kifungu 66: (f) kinaruhusu Spika iwapo hatakuwa miongoni mwa wabunge
Nitarejea baada ya kukipata kifugu cha Uchaguzi wa Spika wa JMT
 
Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
16,809
2,000
Katiba inamtaka amuandikie barua ya taarifa Katibu wa Bunge. Haijataja kikao maalum cha Bunge. Na ofisi za Bunge ziko wazi siku zote.

Wabunge ataenda kuwaaga tu kama Spika wao. Ila atabaki nao kama mbunge wa kawaida.

Amefanya kiburi tu.

Amandla...
Ni msumbufu, nadhani udogo wa umbo na wenyewe ni tatizo. Kaonyesha kiburi kisicho na sababu lakini ni ngumu sana kwake kushindana na rais aliye madarakani.
 
sengobad

JF-Expert Member
Aug 13, 2017
5,157
2,000
Mwajiri wa spika ni chama maana ndio kilimdhamini kuwa spika ....bila CCM katibu wa Bunge hamtambui Job.....katibu wa Bunge anapokea barua ya chama kuthibitisha kujiuzuru kwa mtumishi wake. Na katiba imeelezea vizuri kujiuzuru kutaelekezwa kwenye mamlaka zilizo kuteua. Job kateuliwa na CCM na kupigiwa kura na bungeni.

Ni kazi ya mwajiriwa wa bunge (katibu) kupokea taarifa na kuanza maandalizi ya uchaguzi wa spika baada ya kupokea jina toka kwa mdhamini wa mgombea.
Aacheni bangi soma katiba inasemaje
 
Mwanga Mkali

JF-Expert Member
Jul 8, 2018
755
1,000
Umeandika upuuzi mtupu. Hakuna unachojua. Kasome katiba.

Hata wabunge wanadhaminiwa na vyama lakini wakijiuzulu, wanaandika barua kwa spika.

Spika amedhiniwa na chama chake kugombea nafasi ya uspika, lakini aliyemchagua kuwa spika, siyo chama chake. Na sheria ipo wazi kuwa spika atapaleka taarifa ya kujiuzulu Bungeni, siyo kwenye chama.

Ni akili ndogo sana inahitajika kuelewa hili. Ndugai siyo kwamba haelewi ila amefanya hivyo kuonesha kwamba ameshinikizwa na chama, na hivyo kuwataarifu hao waliomshinikiza kuwa kama uspika ni mali ya chama, basi amejiuzulu, lakini, kikatiba hajajiuzulu bado.
Hahaha subilia sana kwamba atajiuzulu kikatiba .... nothing will change those speculations ati ameshinikizwa na chama will remain yours... amejiuzuru kwa kuwa hakubaliani na rais na jopo lake la wapigaji. Kusema chama ni nani wakati na yeye yupo kamati kuu ni ujinga ulipitiliza. Ukopa fedha ambazo tayari umezitungia sheria ya kuzikamua kwa watu... then zifanye kazi ipi?

Government expenditure raised unnecessarily kwa mama na baraza lote kuwa nje ya kituo chao cha kazi... all of then wanalipwa per diem bado mafuta ya kuwaita watendaji kujadili maswa Dar nk... na kama hulijui picha lilianza baada ya spika kumhoji Prime minister kwamba fedha za kuendeshea serikali Dar zinalipwa toka budget gani? Kuanzia hapo Job akawa ameonyesha joto la 2025 according to hangaya...

Binafsi nilimshangaa kuomba radhi kwa kitu ambacho hakupaswa kuomba radhi kabisa... so komaa na katiba kwamba imepindishwa uone kama atabaki kwenye uspika... Feb 1 tunapata spika mwingine toka kundi pendwa.
 
Bejamini Netanyahu

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
60,105
2,000
Ni kweli Katiba inatamka kwamba Spika atajiuzulu mbele ya Bunge, na nikweli kabisa kwamba Spika alipaswa kujiuzulu mbele ya Bunge. Lakini ukweli uliowazi kwamba yeye kiu ya kuongoza Bunge imeisha kipindi ambacho hakuna Bunge linaendelea. Ilikuwa haiwezekani kujiuzulu mbele ya Bunge maana ilo Bunge halijakaa litakaa February

Endapo angeitisha bunge maaalumu kwa ajili ya kutangaza kujiuzulu mambo mawili yangetokea yasiyo na tija
1. Angevunja katiba kwa sababu kujiuzulu kwake hakujatajwa kwamba ataitisha Bunge la dharura.
2. Wabunge wangelazimika kulipwa stahiki za vikao vya dhararu pesa ambayo Ingetokana na kodi za wananchi na may muhimili wa serekali unaotunza fedha ungeweza kuzalisha audit query au Kugoma kulipa Kama ambavyo umewahi kuingilia bunge Hadi wakarejesha fedha kwa JPM

Kwa msingi huo Mhe Ndugai yupo sahihi kumjulisha Katibu wa Chama na kuwapa nakala Bunge Kwa ajili yakuanza maandalizi ya kujaza nafasi itakayokuwa wazi kikatiba hapo February. Hivyo takwa la kikatiba litatimizwa kwenye kikao kijacho Cha Bunge ambacho kitapokea taarifa rasmi ya kujiuzulu uspika na baadaye taratibu za kumpata spika mpya kufanyika.

Nimwombe Mhe. Mbatia asiangaike kwenda Mahakamani maana anachotaka kifanyike leo kisingeweza kufanyika hadi February. Kwa tafsiri nyingine Bunge halina taarifa rasmi yakujiuzulu kwa Spika hadi litakapokaa na kupewa taarifa ndipo mchakato wa kosheria wa kujiuzulu utakapokamilika.

Mwisho, nishukuru kwamba wale wote walioshindwa kutumia akili na maarifa waliyopewa na Mwenyenzi MUNGU wanavuliwa nguo. Ndugai alishindwa kujua Spika ana kazi gani yeye akawa anaambatana na RAIS Kila anapokwenda, akawa anapokea maelekezo Nini akafanye Bungeni, Leo wale waliomtuma wamemtumbua kwa fedhea
Ndugai hana akili timamu
 
Bejamini Netanyahu

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
60,105
2,000
Umeandika upuuzi mtupu. Hakuna unachojua. Kasome katiba.

Hata wabunge wanadhaminiwa na vyama lakini wakijiuzulu, wanaandika barua kwa spika.

Spika amedhiniwa na chama chake kugombea nafasi ya uspika, lakini aliyemchagua kuwa spika, siyo chama chake. Na sheria ipo wazi kuwa spika atapaleka taarifa ya kujiuzulu Bungeni, siyo kwenye chama.

Ni akili ndogo sana inahitajika kuelewa hili. Ndugai siyo kwamba haelewi ila amefanya hivyo kuonesha kwamba ameshinikizwa na chama, na hivyo kuwataarifu hao waliomshinikiza kuwa kama uspika ni mali ya chama, basi amejiuzulu, lakini, kikatiba hajajiuzulu bado.
Upo sahihi sn
 
Consultant

JF-Expert Member
Jun 15, 2008
11,242
2,000
Katibu wa Bunge anateuliwa na Rais!
Yaani RAIS amejipachika kila kona. Huu upuuzi upo Tanzania na kwingine ambapo mhimili mmoja ndio kila kitu.

Speaker aliyependekezwa na CCM hataweza kuwa huru na objective milele yote kwa mwenyekiti wa CCM
 
Fundi Mchundo

Platinum Member
Nov 9, 2007
7,660
2,000
Ni kweli kuwa Katiba haimtaji moja kwa moja Katibu wa Bunge. Inachosema ni kuwa Spika anatakiwa kuwasilisha taarifa ya kujiuzulu kwake kwenye bunge. Kwa kawaida kuwasilisha kuna maana unakabidhi kitu halisi kama barua, nyaraka n.k. Kiutendaji vitu vyote kama hivi vinawasilishwa kwa Mtendaji Mkuu wa taasisi husika. Ndio maana ukiandika barua wizarani unatakiwa umwandikie Katibu Mkuu sio Waziri. Hali kadhalika, mkoani barua na taarifa zote zinapaswa kupelekwa kwa Katibu Tawala sio Mkuu wa Mkoa. Kwa sababu Katibu wa Bunge ndio Mtendaji Mkuu wa Bunge basi taarifa iliyoandikwa inatakiwa iwe addressed kwake na sio kwengine. Kwa maoni yangu, ingekuwa wabunge wanahusika basi Katiba ingesema mbele ya kikao cha Bunge.
Lakini ukweli ni kuwa huu ni mfano wa kwa nini tunahitaji Katiba mpya ambayo haitatuchanganya. Kwa sasa hivi ni bora Mahakama itoe ufafanuzi.

Amandla...
 
battawi

JF-Expert Member
Mar 29, 2014
2,155
2,000
Tukio hili linadhihirisha wazi kuw Tanzania Hakuna Demokrasi na uhuru wa Mawazo .Ndio Maana Maon ya ndungai yamemkamilisha Raisi na kumfyatukia Spika akisahau kuwa ,Bunge ni Muhimili kama serikali katika nchi.
Yawezekana kikatiba Mama kaover lap Mamlaka yake, lakiniTabuu ya Tanzania imemlowesha Ndungai,.
Amevuna matunda ya mikono ya chama chake .
Sasa ndungai ashirikiane na Upinzani kushinikiza kuletwa kwa Katiba Mpya ili Future ya TZ iwe Nzuri

KATIBA YETU INADAI ETI KUNA MIHIMILI MITATU 3 ILIYO SAWA.
Serikali
Bunge.
Mahakama.
Hapa inaonesha wazi kuwa Serikali ndiyo iliyoweka shinikizo kw Spika Kujiuzulu.Na ndio muhimili wenye kudhibiti wengine. Kawa mantiki hii Mihimili mingine imeingiliwa na kushinikizwa.
Iko wapi hiyo demokasia hapa?
Kama Ingelikuwa Spika ni wa chama Kingine, na akaamua kuendelea kubaki ,nani angemlazimisha kujiuzulu?
Madai ya spika kuhusu serikali kukopa sana , ni ya kweli ila kosa lake ni kuwa yeye kama muhimili wa Bunge ulipaswa kuulizwa kama Mikopo hii iliidhinishwa na Bunge au Laa, na kama ilifanywa bila ya Idhini ya Bunge basi Raisi ndio angelazimika Kujiuzulu, au kutoa wito wa kuto kuwa na imani naye.

Hivi niulize ,chama cha siasa CCM nacho ni Muhimili?
au

Idara ya Usalama wa Taifa Jee? Mimi naona huu ndio Muhimili mkuu, wakitaka uwepo madarkani utabaki,wakitaka uondoke Utatoka
Katiba yetu ni ya kizamani sana haindani kabisa na Mabadiliko ya TABIA NCHI ya siasa za dunia namahitaji ya Utandawazi ,

KATIBA MPYA INAHITAJIKA NOW NOT TOMOROW
 
Maulaga59

JF-Expert Member
Feb 1, 2021
1,449
2,000
Ni kweli Katiba inatamka kwamba Spika atajiuzulu mbele ya Bunge, na nikweli kabisa kwamba Spika alipaswa kujiuzulu mbele ya Bunge. Lakini ukweli uliowazi kwamba yeye kiu ya kuongoza Bunge imeisha kipindi ambacho hakuna Bunge linaendelea. Ilikuwa haiwezekani kujiuzulu mbele ya Bunge maana ilo Bunge halijakaa litakaa February

Endapo angeitisha bunge maaalumu kwa ajili ya kutangaza kujiuzulu mambo mawili yangetokea yasiyo na tija
1. Angevunja katiba kwa sababu kujiuzulu kwake hakujatajwa kwamba ataitisha Bunge la dharura.
2. Wabunge wangelazimika kulipwa stahiki za vikao vya dhararu pesa ambayo Ingetokana na kodi za wananchi na may muhimili wa serekali unaotunza fedha ungeweza kuzalisha audit query au Kugoma kulipa Kama ambavyo umewahi kuingilia bunge Hadi wakarejesha fedha kwa JPM

Kwa msingi huo Mhe Ndugai yupo sahihi kumjulisha Katibu wa Chama na kuwapa nakala Bunge Kwa ajili yakuanza maandalizi ya kujaza nafasi itakayokuwa wazi kikatiba hapo February. Hivyo takwa la kikatiba litatimizwa kwenye kikao kijacho Cha Bunge ambacho kitapokea taarifa rasmi ya kujiuzulu uspika na baadaye taratibu za kumpata spika mpya kufanyika.

Nimwombe Mhe. Mbatia asiangaike kwenda Mahakamani maana anachotaka kifanyike leo kisingeweza kufanyika hadi February. Kwa tafsiri nyingine Bunge halina taarifa rasmi yakujiuzulu kwa Spika hadi litakapokaa na kupewa taarifa ndipo mchakato wa kosheria wa kujiuzulu utakapokamilika.

Mwisho, nishukuru kwamba wale wote walioshindwa kutumia akili na maarifa waliyopewa na Mwenyenzi MUNGU wanavuliwa nguo. Ndugai alishindwa kujua Spika ana kazi gani yeye akawa anaambatana na RAIS Kila anapokwenda, akawa anapokea maelekezo Nini akafanye Bungeni, Leo wale waliomtuma wamemtumbua kwa fedhea
[https://res]

Baada ya kuibuka kwa mitazamo tofauti baada ya aliyekuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai kujiuzulu, tumemtafuta aliyekuwa Spika wa Bunge kuanzia 1994 hadi 2005 Pius Msekwa kwaajili ya ufafanuzi.

Msekwa ameeleza kuwa taratibu zote zimefuatwa na hakuna kilichoharibika kwa mujibu wa katiba ya Tanzania.

''Spika amechaguliwa na bunge, kwahiyo utaratibu sahihi barua ya Spika kujiuzulu ni lazima ipelekwe kwenye bunge na isomwe ndani ya bunge'' Spika Mstaafu Pius Msekwa ametoa ufafanuzi.

Zaidi msikilize hapa
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom