Mbatia na unabii wako wa kishetani umegonga mwamba

Katikati ya mwezi uliopita Mbatia alijitokeza kwenye vyombo vya habari (mwanahalisi tv online) akasema baada ya wiki mbili kutakuwa na vifo vingi sana vya corona nchini kwetu katika namna ambayo haijawahi kutokea na hospitali zitazidiwa sana!

Ni janga kubwa!! Wee mbatia wewe!! yaani unaamua kuwa dalali wa mabeberu ili wapige pesa ya chanjo kichaa isiyoweza kumkinga mchanjwaji na maambukizi mapya!!

Hata kama una njaa ndo unaamua kuja na mkwara wa kutaka kutuingizia hofu!! Nilikupinga na kama una ubavu nenda tana mwanahalisi tv online ukarudie maneno yale yale!!

Acha wiki mbili, karibuni mwezi mzima unapita watanzania tupo salama salimini!! Vifo vilivyopo ni vya kawaida na hakuna maiti zilizozagaa wala hakuna taharuku yoyote na hakuna hospitali iliyozidiwa!! Wagonjwa wa corona mnaendelea kuwatafuta kwa tochi.

Tuambie Mbatia umefaidika nini kuwa na nabii wa Ibilisi kuhusu corona?? Manabii wa mauti kuhusu Tanzania waliokutangulia waligonga mwamba, na wewe umegonga mwamba na wajao watagonga mwamba!

Kwa taarifa yako maombi ya watanzania wacha Mungu ya mwaka 2020 hayaja-expire!! Na tunazidi kumwomba Mungu!! Timu ibilisi mtasubiri sana!

Hakuna namna ya kutuingizia hofu! Waambieni wanaowatuma kuwa Mungu wa Tanzania yuko macho!!
Aaah aah! Anafanana na yule Daktari aliyesema Tanzania kuna baa la ugonjwa wa Zika!
Kama kawaida alishangiliwa sana na makamanda! Lakini mpaka Leo imebaki story.
 
Jamani mimi mwezi uliopita nilikuwa ndani ya Basi natokea Arusha nakuja Dar nilikuwa nasikia abiria wakiongea kwenye simu karibia kila abiria alikuwa akiongea kwamba anakwenda kwenye msiba.

Katika umri wangu huu sijawahi kukutana na hali kama ile.
 
We mbayuwayu hebu tumia akili wewe. Haikusaidii chochote kuleta ushabiki maandazi kwenye tatizo.

We huoni hii misiba sasa hivi? Unaona sawa tu?

Eti Mungu wa Tanzania.
Hujasikia pale Moshi kumekuwa na uhaba wa majeneza hata watengeneza majeneza wakaomba msaada?
 
Back
Top Bottom