LazaroSMtindi
Senior Member
- May 6, 2008
- 100
- 5
Magazeti mengi ya leo Tanzania yamepambwa na taarifa za Mbatia wa NCCR kumtaka Spika wa Bunge ajiuzulu ati kwa kushabikia ushirikina Bungeni. Hii ni mara ya nne namwona Mbatia akitumika kama wakala wa mafisadi. Mara ya kwanza alikuja juu kumtetea Lowassa kuwa hakupewa nafasi ya kusikilizwa na Kamati ya Mwakyembe juu ya Richmond, bila kujua kuwa nafasi ya kujitetea alikuwa nayo Lowassa ndani ya Bunge, akachagua kujiuzulu kwa haraka ili mambo mengi yasijulikane. Kesi za EPA na Rada zilipojitokeza, Mbatia akawa bubu kabisa, akisubiri nafasi ya kumkaba koo Spika anayeruhusu mijadala ya aina hiyo Bungeni! Suala la ushirikina lilipoingia Bungeni, Mbatia akawa kinara wa hoja hiyo bila kuelewa kuwa uchunguzi ulikuwa wa lazima kujua kama kile kilichodaiwa kumwagwa Bungeni kilikuwa na sumu au la! Spika Sitta alijieleza vizuri kabisa toka mwanzo kuwa haamini mambo ya kishirikina, lakini lazima achukue tahadhari kulinda usalama wa Wabunge. Sitta alikosea wapi kumwita Mkemia Mkuu wa Serikali kuchunguza unga au vumbi lililokuwemo Bungeni? Mbona safari za ndege zinaahirishwa kwa bahasha ndogo tu kuonekana kwenye kiti mpaka uchunguzi ufanyike? Huo ni ushirikina? Tatizo la Mbatia ni elimu au uwakala/ukuwadi wa kulipwa na mafisadi? Watu tunaelewa kuwa shangazi wake Mbatia kaolewa na Mzee Bomani, Msukuma! Hiyo ndo sababu ya kumtetea kila Msukuma na rafiki zao hata akiwa fisadi? Tunaelewa kaoa Mhaya. Sasa hiyo ndo iwe sababu kuwatetea akina Karamagi wote? Mbatia unaitia aibu NCCR. Ndo maana, chini yan uongozi wake, NCCR imeshindwa kwenye chaguzi zote toka vitongoji hadi taifa kwa kukosa hoja na kutetea mafisadi. Sisi wengine tunamwona Sitta kama kiongozi wa mapambano magumu ya kutetea maslahi ya umma Tanzania. Hatutakubali kumpoteza ati kwa kumuudhi shemeji ya Mbatia au mjomba wake. NCCR ziiii!