nyamadoke75
Member
- Apr 1, 2020
- 86
- 280
Mwenyekiti wa NCCR -Mageuzi Taifa, James Mbatia amejikuta kwenye wakati mgumu Mara baada ya kuishiwa fedha za kuwalipa waendesha pikipiki aliokuwa amewakusanya kuhudhulia mkutano wake kama wanachama wapya.
Mbatia alifika katika ukumbi wa hotel ya Corridor Spring jijini Arusha majira ya saa 6.30 mchana na baada ya salamu mbalimbali kutoka kwa wanachama aliodai wamehama kutoka vyama vingine vya upinzani, alianza kuhutubia na baadaye alitoa kadi kwa wanachama hao wapya wapatao 225.
Hata hivyo baada ya zoezi hilo kukamilika baadhi ya waendesha pikipiki walizingira gari la Mbatia na kuanza kumzonga wakitaka malipo yao ya sh, 10,000 hadi 20,000 waliokuwa wameahidiwa wakati wakikusanywa kutoka kwenye vijiwe vya pikipiki, hata hivyo hadi anaondoka.eneo hilo baadhi yao waliohudulia mkutano. Huo walikuwa bado wamekaa nje ya hoteli hiyo wakisubiri malipo yao huku wengine wakichana kadi kwa hasira walizokabidhiwa na kuzitupa.
Amani Mbise, Joshua Omari na Matayo Palangyo walisema kuwa wao wamefuatwa kwenye vijiwe vya boda boda na kuambiwa tuhudhulie mkutano wa Mbatia kwa muda WA masaa mawili tu tutapewa shilingo 10,000.
"Tumekaa ukumbini tangu SAA nne asubuhi hadi alipokuja SAA sita mchana, tumeshangaa akitugawia kadi za chama chake huku tukitambulishwa kuwa ni wanachama wapya" Alisema mmoja ya waendesha pikipiki Matayo Palangyo.
Watu hao walienda mbali zaidi wakidai kuwa mpango anaoufanya wa kununua wanachama kupitia waendesha pikipiki bila kuwalipa fedha alizoahidi ni kuwadhulumu muda wao wa kazi.