Mbatia amwomba Waziri Mkuu amsaidie kumtoa Kafulila bungeni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbatia amwomba Waziri Mkuu amsaidie kumtoa Kafulila bungeni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by April, Jan 29, 2012.

 1. April

  April Member

  #1
  Jan 29, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13

  Wanajamii,

  Katika hali isiyo ya kawaida baada ya Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, Bw.James Mbatia na wenzake kumaliza mazungumzo Ikulu hivi majuzi, habari za uchunguzi zinasema ya kuwa, mojawapo ya hoja ilikuwa ni kuiomba serikali isaidie kuhakikisha Mh. David Kafulila (Mb. Kigoma Kusini) anatenguliwa ubunge.

  Chanzo kinaeleza kuwa, mwishoni mwa wiki jana James Mbatia ameandika barua ndefu kwa Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akimuomba aingilie kati suala hilo kuhakikisha Bunge linatengua tamko la awali la kuendelea kumtambua David Kafulila kama mbunge.

  Barua hiyo iliyoandikwa Ofisi ya Waziri Mkuu na kupigwa chapuo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Mh. William Lukuvi
  (kama ishara ya kuridhia pendekezo hilo la Mbatia), inaomba nguvu ya Waziri Mkuu itumike kubadili msimamo wa Bunge.
  Pia imeelezwa kuwa, barua hiyo imelalamikia Ofisi ya Bunge kwa kumtambua Mh. David Kafulila kama mwakilishi wa wabunge wa NCCR kwenye msiba wa Marehemu Mh. Regia Mtema katika viwanja vya Karimjee ambapo ilipelikea Mh. Kafulila kushangiliwa na wabunge wengi pasipo itikadi.
  Bw. Mbatia anasisitiza kuwa hali hiyo imemdhalilisha yeye pamoja na chama chake cha NCCR Mageuzi.
  Ikiwa zimebaki siku chache tuu vikao vya Bunge kuanza..............................................:hatari:
  Chanzo chetu kitaendelea kutuhabarisha juu ya ombi hilo la Mbatia kwa serikali yetu sikivu.
  Nawasilisha.


  CHANZO: Ofisi ya Waziri Mkuu
   
 2. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #2
  Jan 29, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  inalekea kafulila kamgusa pabaya mbatia
   
 3. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #3
  Jan 29, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,804
  Likes Received: 1,118
  Trophy Points: 280
  Sasa hao enisisiara Mageuzwa wanataka mwenzao ale wapi?
   
 4. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #4
  Jan 29, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,705
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  Kafulila kaza buti baba but kama vp rudi 2 home CDM 2takupokea lakini ukirudi plz...... Acha zile ishu za kiburi koz we mwenyewe uliwahi kumwambia chacha wangwe dat' uongozi bila demokrasia ni udikteta lakini demokrasia bila nidhamu ni fujo" so take care men na ukumbuke kauli yako.
   
 5. k

  kiche JF-Expert Member

  #5
  Jan 29, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 456
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kwa maana hiyo inadhihirisha kuwa serikali inacheza na sheria/katiba,kwa upande wa bunge watatumia kujuana kutekeleza ombi hilo na kwa vile spika walimweka wao wanaweza kufanikiwa ila ili wasionekane kuwa wanaingilia bunge hasa ikizingatiwa kuwa bunge lilishatoa kauli,watacheza na mahakama ambazo wanazimudu kuliko kawaida,tusubiri hukumu ya fasta tofauti na watu walivyokuwa wanategemea!!!.
   
 6. February

  February Member

  #6
  Jan 29, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 90
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Me nilidhani nccr wangeachana na huyo kafulila. Kama amewazidi nguvu kwenye jimbo lake waelekeze majimbo mengine wana wabunge na kama mkoa mzima umeasi watengeneze mkoa mwingine kama dodoma au morogoro. Ipo mingi tu haina upinzani. Kuendelea kumfuatilia ni kumjenga kafulila na kunaidhofisha nccr. Ningeshauri wapige siasa hata mwaka mzima bila kumtaja kafulila waone kama atasikika.huu ni ushauri wa bure. Kuendelea kumfuatilia ni kumfanya aonekane muhimu bila sababu. Huyu sio shujaa kwanin mnataka aonekane shujaa?
   
 7. M

  Mgaya D.W JF-Expert Member

  #7
  Jan 29, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 966
  Likes Received: 192
  Trophy Points: 60
  ukiwa na wivu kwa wenzako kila jambo linafanywa na wengne unaona kama vle we unpitwa,mbatia kapoteza dira,hajitambui,anapenda mambo ya kijamii yafanyike kadri ya hisia zake,kumfuatia kafulila ni kupoteza muda,kesi ipo mahakamani kwanin asisubiri maamuz ya mahakama.dah!pole mbatia kwa kuonesha uwezo wako wa kuona kwa jicho la tatu ni mdogo.unataka kulipwa bilion 5 na bank ya nbc kisa walisema mbumbumbu wa mambo ya kibenki,unataka upewe ushndi wa halima mdee na then unagombania madaraka ya kafulila aliyopewa na wananchi wa kigoma.mbatia jitafakari then jipange mzee!
   
 8. George Kahangwa

  George Kahangwa Verified User

  #8
  Jan 30, 2012
  Joined: Oct 18, 2007
  Messages: 539
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Tulipokwenda Ikulu tulizungumza na Mhe. Rais pamoja na baadhi ya mawaziri wake na Mwanasheria mkuu wa serikali kuhusu, mambo mawili; Mchakato wa kuipata katiba mpya, na ongozeko la gharama za umeme.

  JF haina budi kulinda heshima yake dhidi ya upotoshaji. Barua inayotajwa na mwanzisha mada, si miongoni mwa hoja zilizopelekwa ikulu
   
 9. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #9
  Jan 30, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,501
  Likes Received: 5,612
  Trophy Points: 280
  Mkuu zipo tuhuma za kupika zinazoweza kushusha credibility ya JF lakini si hii.sipendi viongozi wakiguswa humu wasivyopendwa wanakimbilia kusema heshima ya JF inashuka.

  Nafikiri majibu ya hoja kama ulivyofanya ni vizuri zaidi maana watu watachambua pumba na mchele! Lakini pia bado hujajibu hoja Mbatia amemuandikia barua waziri mkuu kama mtoa mada anavyosema au ni uongo?
   
 10. O

  OMEGA JF-Expert Member

  #10
  Jan 30, 2012
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 671
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 60
  Si angemuandikia David Cameroon ambaye anatetea haki zao
   
 11. April

  April Member

  #11
  Jan 30, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Ndugu yangu Kahangwa, mimi naweza kuthibitisha niliyoyaandika. Je, nikithibitisha unaahidi utathibitisha unachotetea wewe?
   
 12. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #12
  Jan 30, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,501
  Likes Received: 5,612
  Trophy Points: 280
  Keshakimbia harudi thread hii tena!
   
 13. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #13
  Jan 31, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,819
  Likes Received: 1,140
  Trophy Points: 280
  Katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania haimpi Waziri Mkuu wala Spika wa Bunge mamlaka ya kufanya hivyo kwa sababu hakuna kipengelea kinachoelezea hatima ya mbunge anayefukuzwa au kuachishwa uanachama ni nini. Inazungumzia hatima ya mbunge aliyeacha nafasi hiyo kutokana na sababu nyingine zozote nje ya ile ya kuachishwa uanachama wa chama chake cha siasa. Mambo haya yaliwezekana wakati wa Chama Kimoja walipofukuzwa Hamad Rashid na Maalim Seif kutoka CCM, lakini ilikuwa possible kwa sababu utawala ule haukuwa unaendeshwa kwa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bali kwa katika ya CCM.

  Kutokana na mapungufu haya ya katiba, kafulila ataendelea kuwa mbunge, huku akiendelea kuvutana na uongozi wa chama chake mpaka aidha, akijiunga na Chama kingine cha siasa au akiamua mwenyewe kujiuzulu nafasi yake ya ubunge. Vinginevyo kwa hali ya sasa, atachokosa sana sana ni ushirikiano na Chama Chake, lakini heshima yake kama mbunge, posho na mishahara, ipo pale pale mpaka mwaka 2015.
   
 14. George Kahangwa

  George Kahangwa Verified User

  #14
  Jan 31, 2012
  Joined: Oct 18, 2007
  Messages: 539
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  April, ninachokubishia wewe ni uongo kwamba hiyo hoja ni miongoni mwa tuliyoyapeleka Ikulu. Nilikuwepo Ikulu. Kama umeona barua ofisini kwa waziri mkuu sema hivyo, usiundanganye umma kwamba tulienda ikulu kuzungumza mambo ya Kafulila
   
 15. George Kahangwa

  George Kahangwa Verified User

  #15
  Jan 31, 2012
  Joined: Oct 18, 2007
  Messages: 539
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Ndg. mtazamo, kama unanisema mimi, bora tu uedit ulichoandika
   
 16. +255

  +255 JF-Expert Member

  #16
  Jan 31, 2012
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 1,908
  Likes Received: 285
  Trophy Points: 180
  Kwa maelezo yako issue ya Kafulila hamkuizungumzia Ikulu ila mmemuomba Waziri Mkuu ashughulike nayo!
   
 17. George Kahangwa

  George Kahangwa Verified User

  #17
  Jan 31, 2012
  Joined: Oct 18, 2007
  Messages: 539
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Nashauri usome tena nilichotofautiana na mtoa mada
   
 18. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #18
  Jan 31, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Mkuu umeangalia factor gani ya kusema sirikali yetu ni sikivu?
   
 19. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #19
  Jan 31, 2012
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,421
  Likes Received: 436
  Trophy Points: 180
  Kaahangwa, go and tell Mbatia. NCCR must rethink itself.....

  Tell your colleagues that Tanzania is no linger the teritory of the great man.........

  and that if NCCR sticks to its dirty politics as it was not written to disturb reforms as it was started

  and if it continues to be the personal property of Mr Mbatia....

  then its going to die very soo.....n......

  ni hayo tu. leave kafulila alone! hamumuwezi, umma hauwezi kukubali, serekali haiwezi kukubali, mahakama haiwezi kukubali, wala bunge haliwezi kukubali..........

  acheni siasa za kishoga... huu ni wakati wa kufanya kazi.....you better find some business to do if you cannot politics...
   
 20. April

  April Member

  #20
  Jan 31, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Naomba nirudie kama hujanielewa, nimesema hivii, mojawapo ya mliyoyazungumzia Ikulu ilikuwa ni pamoja na kumwomba Waziri Mkuu aingilie kati suala la Kafulila pamoja na kuwa ya kwamba kwa maandishi mmekwishaliwakilisha hilo kwake. And yes, barua ofisini kwa Waziri Mkuu nimeiona.
  Sijaudanganya umma kama ninyi ndugu zangu washirika wa CCM mnavyotudanganya wakati upinzani wenu una mushkeli.


   
Loading...