Wakudadavuwa
JF-Expert Member
- Feb 17, 2016
- 17,506
- 15,997
Mbatia amekera sana, ametumika kuua demokrasia nchini. Ametumika kuua NCCR-Mageuzi kwa maslahi yake binafsi. Mbatia alikuwa wa kwanza kukaza shingo kutetea ujinga wa akina Lowassa na kundi lake huku akiua chama chake. Leo NCCR-Mageuzi ina mbunge mmoja tu ambaye ni yeye baada ya kupewa hisani na Mbowe kama malipo ya kukuza CHADEMA. NCCR-Mageuzi ndicho chama kilicholeta mageuzi na changamoto ya siasa za vyama vingi nchini.
Mbatia lazima ajue laana hii ya kuua chama haitakuacha, una jambo moja tu la kufanya ni ukipona maradhi yako omba radhi watanzania na utangaze kuhamia CHADEMA ili kutoa fursa ya vijana kuimarisha siasa za upinzani Tanzania. Umekuwa popo muda mrefu sasa ni wakati wa kuonyesha rangi yako halisi tujue kama wewe ni myama au ndege.