Mjukuu wa bibi Pili.
Member
- Dec 21, 2011
- 71
- 75
MWENYEKITI mwenza wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), James Mbatia amewataka wananchi katika jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro, kudai mgao shilingi 609, 000 kwa kila mmoja, toka kwa viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM),fedha zilizotokana na ufisadi katika akaunti ya Tegeta Escrow ya kiasi cha sh,bilioni 321.
Mbatia aliyasema hayo kwa nyakato tofauti katika vijiji vya Mrimbo-Uwo, Matala, Kondiki, Mwika Lole, Maringa, Msae-Kinyambuo na Kondeni vilivyopo Kata ya Mwika Kusini na Kata ya Mwika Kaskazini, Wilaya ya Moshi wakati akiwanadi wagombea wa nafasi ya Ueneyekiti katika vijiji hivyo.
Mbatia aliyepokelewa katika vijiji hivyo kwa majani ya Masale alisema wananchi hawapaswi kuendelea kuumia kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa maabara na shule za Kata kwa sababu wanao uwezo wa kutumia fedha
zilizochotwa katika akaunti hiyo kuchangia maendeleo.
Source;Mie Mwenyewe.mba