Mbaroni kwa madai ya kumuua mpenzi wa zamani akimtuhumu kumloga

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Kurwa Langi (50) Mkazi wa Urambo mkoani Tabora, Kurwa Langi (50), anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kumuua Kumbi Shija, mkazi wa Kata ya Kiloleni, kwa madai kuwa amemloga ashindwe kufanya tendo la ndoa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Barnabas Mwakalukwa, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo lililotokea Novemba 8, mwaka huu, usiku.

Mwakalukwa alisema mauaji hayo yametokea baada ya baadhi ya waganga wa kienyeji kupiga ramli chonganishi kwa madai kuwa Shija amehusika kumloga mtuhumiwa hivyo kushindwa kufanya tendfo la ndoa.

Kutokana na mauaji hayo, alisema waganga waliohusika watakamatwa na kuhojiwa kisha sheria itachukua mkondo wake.

Alisema Langi alipohojiwa aliwaambia polisi kuwa alichukua uamuzi huo baada ya kwenda kwa mganga wa kienyeji na kuambiwa kwamba Shija ambaye aliwahi kumchumbia ndiye anayemloga.

Mtuhumiwa huyo, kwa mujibu wa Mwakalukwa, alisema aliwahi kumposa binti huyo na baadaye kughaili kumuoa na kwenda kuoa mwanamke mwingine.

Alisema baadaye, akiwa kwenye ndoa yake, alikuwa akishindwa kutekeleza jukumu la ndoa kwa mke wake na alipoona tatizo hilo, aliamua kwenda kwa waganga wa kienyeji watano ambao wote walimwambia amelogwa na mwanamke aliyemchumbia na kumwacha.

“Kutokana na kuambiwa huko waganga hao, Langi aliamua kwenda kutekeleza mauaji hayo,” alisema Mwakalukwa.

Ofisa Mtendaji wa Kata ya Kiloleni, Amos Nicholas, alisema Shija alifia hospitalini katika karakati za kuokoa maisha yake.

Alisema baada ya kushambuliwa na mchumba wake huyo wa zamani, walimpeleka mwanamke huyo hospitalini lakini alifia mikononi mwa madaktari kwa sababu alikatwa sehemu mbaya.

Ofisa Tarafa wa Tarafa wa Usoke, Nelson Majula, alitoa pole huku akisema ama ilivyokuwa sheria ya kata ya Tarafa ya Usoke huku mwanamume aliyemkaribisha mtuhumiwa huyo anayejulikana kama Issa Mohamed mkazi wa Kata ya kiloleni naye amejikuta hatiani baada ya kumaribisha mgeni pasipo kufuata taratibu za kijiji.
 
...Kama ni Kweli, kulikuwa na lazima ya Kumuua Huyo X-fiancee?
Si angemuomba tu radhi kwa aliyomtenda na kumuomba tu amrejeshee uanaume wake??
 
Waganga wote watano wamemtaja huyo binti kuwa ndio analoga, je, alikuwa akiwapa hints juu yake au walikuwa wanajua tu wenyewe?
 
...Kama ni Kweli, kulikuwa na lazima ya Kumuua Huyo X-fiancee?
Si angemuomba tu radhi kwa aliyomtenda na kumuomba tu amrejeshee uanaume wake??
Yeah, hii ingekuwa placebo nzuri sana, ofcourse hakurogwa ila aliaminishwa hivyo, so yule binti kusema tu nimekusameheningetosha kumponya, maana tatizo lipo kichwani
 
Kurwa Langi (50) Mkazi wa Urambo mkoani Tabora, Kurwa Langi (50), anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kumuua Kumbi Shija, mkazi wa Kata ya Kiloleni, kwa madai kuwa amemloga ashindwe kufanya tendo la ndoa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Barnabas Mwakalukwa, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo lililotokea Novemba 8, mwaka huu, usiku.

Mwakalukwa alisema mauaji hayo yametokea baada ya baadhi ya waganga wa kienyeji kupiga ramli chonganishi kwa madai kuwa Shija amehusika kumloga mtuhumiwa hivyo kushindwa kufanya tendfo la ndoa.

Kutokana na mauaji hayo, alisema waganga waliohusika watakamatwa na kuhojiwa kisha sheria itachukua mkondo wake.

Alisema Langi alipohojiwa aliwaambia polisi kuwa alichukua uamuzi huo baada ya kwenda kwa mganga wa kienyeji na kuambiwa kwamba Shija ambaye aliwahi kumchumbia ndiye anayemloga.

Mtuhumiwa huyo, kwa mujibu wa Mwakalukwa, alisema aliwahi kumposa binti huyo na baadaye kughaili kumuoa na kwenda kuoa mwanamke mwingine.
  1. Kwa hiyo kwa takribani miaka 30 (assumption ameoa akiwa na 20) hakuweza chochote!!!
  2. Hao waganga wakimruka wakamtaka mtuhumiwa aonyeshe ushahidi (cheti cha matibabu) ataonyesha ushahidi gani kuwa hayo majibu ni yao?
  3. Nashauri wataalamu wachukue sampuli ya chakula cha mtuhumiwa huenda lishe kwa huyo mkewe haikuwa nutritive ndiyo akashindwa tendo
 
Back
Top Bottom