Mbaroni kwa kuwafanyia wanafunzi mitihani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbaroni kwa kuwafanyia wanafunzi mitihani

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Msongoru, Sep 23, 2008.

 1. Msongoru

  Msongoru JF-Expert Member

  #1
  Sep 23, 2008
  Joined: Apr 16, 2008
  Messages: 306
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  na Shangwe Thani, Shinyanga  JESHI la Polisi mkoani Shinyanga, linawashikilia walimu wawili wa shule za msingi kwa tuhuma za kuwafanyia mtihani wa taifa wa kumaliza elimu ya msingi wanafunzi watano kinyume cha sheria na taratibu za mitihani.

  Kamanda wa Polisi mkoani Shinyanga, Shaibu Ibrahim, alisema ofisini kwake jana kuwa tukio hilo lilitokea Septemba 11 wakati wanafunzi wa shule za msingi nchini wakifanya mtihani wa taifa wa darasa la saba.

  Aliwataja walimu wanaoshikiliwa na polisi kuwa Bengwe Hiellele (44), mwalimu wa Shule ya Msingi ya Ibango, iliyopo katika Kijiji cha Salawe Wilaya ya Shinyanga Vijijini na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Itobanilo, John Madirisha.

  Mwalimu Hielele, aliyekuwa msimamizi wa mtihani katika shule hiyo kwa kushirikiana na mwalimu Madirisha ambaye ni mwalimu mkuu wa Shule ya Itobanilo, wanadaiwa kuwafanyia mtihani wanafunzi watano, kinyume cha sheria na taratibu za mitihani.

  Kamanda Ibrahim, aliwataja wanafunzi waliofanyiwa mitihani kuwa ni Shangaluka Msala, Frank Jumanne, Maganga Magadya, John Jumanne na Saidi Cosmas na kwamba uchunguzi wa awali wa polisi umebaini kuwa wanafunzi hao walitoa shilingi 20,000 kila mmoja ili wasaidiwe kufanyiwa mtihani na walimu hao.

  Alibainisha kuwa kabla ya kukamatwa kwao walimu hao walikuwa wamewafanyia mitihani ya hisabati, Kiswahili, Sayansi na Kiingereza na mwalimu Hielele, alipopekuliwa mfukoni alikutwa akiwa na karatasi ya maswali ya somo la hisabati ambao ulifanyika Septemba 10 mwaka huu.
   
 2. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #2
  Sep 23, 2008
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280

  Hayo ndo ya Shinyanga!!!! Chuo cha Ustawi wa jammi jamaa la Mzumbe University lilikuja kumfanyia girlfriend wake mtihani!!!! Hii ni habari nyepesinyepesi ya wiki iliyopita. Jamani maksi za kwenye vyeti somteimes si lolote, ndiyo maana mtu anaomba kazi cheti flying colours. Then mpe practical duties. deliverables ni zero au tuseme hasi kabisa then unashangaa mbona cheti kapasua sana??? Hizi ni sawa na maksi za chupi.

  Yale yale ya BOT wafanyakazi watano vyeti ni fake??? Sasa je wao walifanyiwa mtihani au ni vyeti vilichongwa mitaani?? Usanii mwingi Tanzania.
   
 3. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #3
  Sep 23, 2008
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Hiyo habari hapo juu ni kielelezo kidogo cha hali halisi (Rushwa, Ufukara uliokubuhu, Udhalimu/oppression.... the list goes on). Natabiri kwamba JK atakuwa raisi wa kwanza wa TZ kushitakiwa.


  Ujumbe mzito kwenye katuni.

  .
   
 4. K

  Kipanga JF-Expert Member

  #4
  Sep 23, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 679
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Ni njaa tu za walimu wetu....20,000 umfanyie mwanafunzi mtihani. Nadhani sirikali ya JK iwe makini katika kupanga viwango vya mishahara vya watumishi wake.

  Yawezekana na ufisadi unaondelea unawapa machungu walimu kuona viongozi wanafisadi kila siku na wao wameona bora wafisadi katika maeneo yao...Nchi haina mwenyewe sasa....
   
 5. Msongoru

  Msongoru JF-Expert Member

  #5
  Sep 23, 2008
  Joined: Apr 16, 2008
  Messages: 306
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Lakini pia sisi wengine kusoma hatutaki!! Ni wavivu mno.
   
 6. S

  Swabiri Member

  #6
  Sep 23, 2008
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  That is so bad only 20 k
   
Loading...