Nenda Ikulu ukimkosa uje utuambie, usisubiri tu kupewa ushahidi na wengine hata wewe unaweza kufanya.
Unaelewa kwamba ukienda Ikulu na kumkosa Magufuli hilo halithibitishi lolote?

Unaweza kufikiri kwa kutumia mantiki?
 
Huu ujinga ndio alikuwa nao yule dogo(ngonyani) wa DIT kipindi kile kazusha mwamunyange kafa. Alivyofika mahakamani akasema mleteni mwamunyange....... Alionekana kituko. Kumbe wanatoa humu huu ujinga
Pole Sana Benedict ngonyani, pole kwa kukaa segerea sababu ya ujinga wa mitandaoni
Kwa haki, hawatakiwi kumfunga kwa uzushi bila kuthibitisha kwamba alichosema ni uzushi.

Sasa wakisema kwamba habari kuwa Rais Magufuli anaumwa ni uzushi, inabidi wathibitishe kwamba haumwi.

Na kwa sasa hata kumuonesha live tu hawawezi.

Kwa nini?

Hizi habari kwamba Magufuli anaumwa ni uzushi tu ama kweli?
 
Ndio maana watu wanaombea kifo
Hajafa kafungua macho alfajirii baada ya kuwa amekata kauli toka tarehe 4/3 ina maana zaidi ya siku kumi kuwa kwenye machine hajitambui, haonekani kuwa timamu ....japo watalazimisha aanze kutoa maagizo ,kwenye nchi inayofuata katiba angehitaji miezi kadhaa ya kuangalia afya yake ....
 
Hajafa kafungua macho alfajirii baada ya kuwa amekata kauli toka tarehe 4/3 ina maana zaidi ya siku kumi kuwa kwenye machine hajitambui, haonekani kuwa timamu ....japo watalazimisha aanze kutoa maagizo ,kwenye nchi inayofuata katiba angehitaji miezi kadhaa ya kuangalia afya yake ....
Umezitoa wapi hizi
 
Wenye magazetiyaliyoandika kuwa Mbowe, Mrema na Sarungi wamekufa wameshakamatwa?
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Ramadhani Kingai amesema Polisi wanamshikilia Charles Majura (35) ambaye ni Fundi Simu, kwa kosa la kimtandao kwa kusambaza taarifa za uzushi kuwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli ni mgonjwa.

Pia, Kingai amesema wanamsaka mwanaharakati anayejiita Kigogo katika mtandao wa Twitter, kwa tuhuma za kuzusha hofu na uongo kwamba Rais John Magufuli anaumwa.

View attachment 1724776
 
Jamaa ameonekana kanisani jana? Kuna yeyote alieona clip yake Jamaa akizungumza na waumini wenzake kanisani kama anavyofanya kila jumapili? Ok kama majibu ni hapana na hapana isiwe tabu.

Usipomuona mtu unaemjua au kumzoea kumuona mahali fulani, hakuna kosa kuuliza cha mno? Nasi tunasema nini cha mno hadi jamaaa anashindwa kufika kanisani au ametoka katika dini ya ukiristo?
 
Back
Top Bottom