77.jpg
 
Maajabu makubwa kabisa haya!

Amesambaza kwa kutumia media gani?

Hakuna weledi hapo. Waliosambaza ni wengine huyo wanamuonea tu ili waonekane wanapiga kazi. Mediocrely done.
Kuna theory inasema "to get the end, go to the beginning"
 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Ramadhani Kingai amesema Polisi wanamshikilia Charles Majura (35) ambaye ni Fundi Simu, kwa kosa la kimtandao kwa kusambaza taarifa za uzushi kuwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli ni mgonjwa.

Pia, Kingai amesema wanamsaka mwanaharakati anayejiita Kigogo katika mtandao wa Twitter, kwa tuhuma za kuzusha hofu na uongo kwamba Rais John Magufuli anaumwa.

View attachment 1724776
Hii kesi akipelekwa mahakamani kwa uzushi, mshtakiwa kasema kama mimi mzushi tupeni ushahidi usiopinguka rais Magufuli yupo na afya nzuri, tuonesheni rais huyu hapa leo na ana afya nzuri, kwa ushahidi wa kumuonq na wa jopo la madaktari, mahakama itakuwa sehemu nzuri sana na kumaliza ubishi.

Kama Magufuli hayupo hai/ hana afya nzuri, na mshtakiwa ana wakili mzuri, hii kesi kufikishwa mahakamani na kumalizwa kisheria kumfunga mshtakiwa ni vigumu sana.

Wataupa nafasi upande wa mshtakiwa kuoneshwa ushahidi kwamba Magufuli ni mzima.
 
Hii kesi akipelekwa mahakamani kwa uzushi, mshtakiwa kasema kama mimi mzushi tupeni ushahidi usiopinguka rais Magufuli yupo na afya nzuri, tuonesheni rais huyu hapa leo na ana afya nzuri, kwa ushahidi wa kumuonq na wa jopo la madaktari, mahakama itakuwa sehemu nzuri sana na kumaliza ubishi...
Nenda Ikulu ukimkosa uje utuambie, usisubiri tu kupewa ushahidi na wengine hata wewe unaweza kufanya.
 
Hii kesi akipelekwa mahakamani kwa uzushi, mshtakiwa kasema kama mimi mzushi tupeni ushahidi usiopinguka rais Magufuli yupo na afya nzuri, tuonesheni rais huyu hapa leo na ana afya nzuri, kwa ushahidi wa kumuonq na wa jopo la madaktari, mahakama itakuwa sehemu nzuri sana na kumaliza ubishi....
Huu ujinga ndio alikuwa nao yule dogo(ngonyani) wa DIT kipindi kile kazusha mwamunyange kafa. Alivyofika mahakamani akasema mleteni mwamunyange....... Alionekana kituko. Kumbe wanatoa humu huu ujinga.

Pole Sana Benedict ngonyani, pole kwa kukaa segerea sababu ya ujinga wa mitandaoni
 
Ni AIBU kukamatwa na kuwekwa ndani kwasababu za kijinga kama hizi...
Wewe huoni aibu kwa wakamataji ila kwa mkamatwaji tu?

Haya mambo ya uzushi hayapaswi hata kujadiliwa na jeshi la polisi.

Hakuna raia anayeamini tetesi bila kuona ktk vyanzo mahususi.

Utashangaa hapelekwi mahakami..na akipelekwa utaambiwa uchunguzi bado unaendelea.
 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Ramadhani Kingai amesema Polisi wanamshikilia Charles Majura (35) ambaye ni Fundi Simu, kwa kosa la kimtandao kwa kusambaza taarifa za uzushi kuwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli ni mgonjwa....
Vipi jamani kuna anaejua kama mheshimiwa alihudhuria ibada ya jumapili na kutoa hutuba yake ya kila jumapili kanisani?
 
Back
Top Bottom