Mbaroni kwa kukutwa na vifaa vya kukeketea wasichana

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
POLISI wa Kanda Maalumu ya Tarime/Rorya, wanamshikilia mkazi wa Kijiji cha Tagota wilayani Tarime mkoani Mara, Nyamanosi Magaigwa (78), kwa kukutwa na vifaa vya kukeketea wasichana na akiwa katika maandalizi ya kuwakeketa wasichana wawili.

Magaigwa alikamatwa akiwa na nyembe 80, unga wa muhogo na ulezi ukiwa ndani ya kisonzo ambapo wasichana wawili wanafunzi waliotaka kukeketwa, wameokolewa na polisi na kupelekwa kwa wenzao zaidi ya 300 waliopo katika Kanisa Katoliki katika Kituo cha Masanga, Tarafa ya Ingwe.

Akiwa na mtuhumiwa huyo ofisini kwake Desemba 16, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tarime/Rorya, Costantine Massawe, alisema bibi huyo alikamatwa Desemba 15 saa 11 jioni katika Kijiji cha Tagota kilometa tatu kutoka mjini Tarime baada ya kupata taarifa kutoka kwa wasamaria.

Taarifa hizo, Kamanda Massawe alisema zilieleza kwamba kulikuwa na wasichana wanafunzi wawili, Prisca Mwita (15), anayesoma Shule ya Msingi Nyamongo na Neema Matiko (17), wa Shule ya Sekondari ya Ronsoti Sekondari kidato cha pili, wangekeketwa muda huo na bibi huyo, licha ya kuwagomea wazazi wao.

“Nilituma askari wangu maeneo hayo na walipofika eneo hilo walimkuta mama huyo tayari akiwa amejiandaa kutaka kuwakeketa wasichana hao, ndipo askari wangu walimkamata ngariba huyo pamoja na vifaa hivyo mnavyoviona hapo zikiwemo nyembe 80, kisonzo na
unga,” alisema Kamanda Massawe.

Kamanda Massawe alisema mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani wakati wowote ule kujibu mashitaka ya kukeketa watoto wa kike; na kutoa mwito kwa mashirika ya umma na yasiyo ya kiserikali kuungana kutoa elimu juu ya madhara ya kukeketa watoto wa kike.
 
Back
Top Bottom