Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,005
- 9,872
Watu wawili wamefikishwa mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na mashtaka ya kukutwa na vipande saba vya meno ya tembo yenye thamani ya shilingi za kitanzania zaidi ya milioni 34.
Watu hao ni Abubakar Msangi na Yazidu Njunju, ambao wamesomewa mashtaka hayo mbele ya hakimu mkazi Cassian Matembele na wakili wa serikali mwandamizi Wankyo Simon na kudai kuwa upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika na kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 7,mwaka huu.
Kwa mujibu wa hati ya mashtaka ya washtakiwa wote kwa pamoja wanadaiwa kutenda kosa hilo tarehe 16,Oktoba 2020, ndani ya wilaya ya Temeke katika mkoa wa Dar es salaam ambapo walikutwa na vipande saba vya meno ya Tembo vyenye thamani ya shilingi za kitanzania 34,293,000 bila kuwa na kibali kutoka maliasili.
Aidha Hakimu Matembele amedai kuwa makosa hayo hayana dhamana hivyo washtakiwa wamerudishwa rumande hadi hapo kesi itakapotajwa tena.