Mbaroni kwa kukutwa na meno ya tembo

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
2,774
2,000
Watu wawili wamefikishwa mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na mashtaka ya kukutwa na vipande saba vya meno ya tembo yenye thamani ya shilingi za kitanzania zaidi ya milioni 34.

Watu hao ni Abubakar Msangi na Yazidu Njunju, ambao wamesomewa mashtaka hayo mbele ya hakimu mkazi Cassian Matembele na wakili wa serikali mwandamizi Wankyo Simon na kudai kuwa upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika na kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 7,mwaka huu.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka ya washtakiwa wote kwa pamoja wanadaiwa kutenda kosa hilo tarehe 16,Oktoba 2020, ndani ya wilaya ya Temeke katika mkoa wa Dar es salaam ambapo walikutwa na vipande saba vya meno ya Tembo vyenye thamani ya shilingi za kitanzania 34,293,000 bila kuwa na kibali kutoka maliasili.

Aidha Hakimu Matembele amedai kuwa makosa hayo hayana dhamana hivyo washtakiwa wamerudishwa rumande hadi hapo kesi itakapotajwa tena.
 
Hakimu Mfawidhi

JF-Expert Member
Oct 30, 2018
1,832
2,000
Mtu anaeua tembo, 'a gentle giant' anapaswa kuuliwa na yeye. Tembo ni wachache, hawana ugomvi na mtu, wapole halafu kuna wapumbavu bado wanawaua, hao watu hawapaswi kuendelea kuishi.
 
AK-12

Member
May 14, 2020
7
45
Hivi wanaposema meno ya tembo wanamaanisha zile "pembe za ndovu" (Tusks) au ni meno kama meno anayotumia tembo kutafuna nyasi.

Maana ninachojua mm ni kuwa zile pembe ndio zenye thamani kwakua zinamatumizi mbalimbali, ila kuhusu meno ya tembo sijui yanakazi gani.

Wajuzi tujuzane tafadhali.
 
Iceberg9

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
18,410
2,000
Mbunge wa Ccm alikutwa na Nyara za serikali kibao+silaha za kuwawindia akapigwa fine tu na maisha yanaendelea fresh kabisa.
Sasa unataka kufanana na mbunge, wewe utaingia lockup kijana na uozee huko
 
Iceberg9

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
18,410
2,000
Watu wawili wamefikishwa mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na mashtaka ya kukutwa na vipande saba vya meno ya tembo yenye thamani ya shilingi za kitanzania zaidi ya milioni 34.

Watu hao ni Abubakar Msangi na Yazidu Njunju, ambao wamesomewa mashtaka hayo mbele ya hakimu mkazi Cassian Matembele na wakili wa serikali mwandamizi Wankyo Simon na kudai kuwa upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika na kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 7,mwaka huu.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka ya washtakiwa wote kwa pamoja wanadaiwa kutenda kosa hilo tarehe 16,Oktoba 2020, ndani ya wilaya ya Temeke katika mkoa wa Dar es salaam ambapo walikutwa na vipande saba vya meno ya Tembo vyenye thamani ya shilingi za kitanzania 34,293,000 bila kuwa na kibali kutoka maliasili.

Aidha Hakimu Matembele amedai kuwa makosa hayo hayana dhamana hivyo washtakiwa wamerudishwa rumande hadi hapo kesi itakapotajwa tena.
Sema mwizi mpaka umkamate kashaiba sana, hawa watakua walikua wazoefu
 
mjingamimi

JF-Expert Member
Aug 3, 2015
25,854
2,000
Yale pia ni meno
Hivi wanaposema meno ya tembo wanamaanisha zile "pembe za ndovu" (Tusks) au ni meno kama meno anayotumia tembo kutafuna nyasi.

Maana ninachojua mm ni kuwa zile pembe ndio zenye thamani kwakua zinamatumizi mbalimbali, ila kuhusu meno ya tembo sijui yanakazi gani.

Wajuzi tujuzane tafadhali.
 
Jamaa_Mbishi

JF-Expert Member
Jun 15, 2013
7,682
2,000
Watu wawili wamefikishwa mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na mashtaka ya kukutwa na vipande saba vya meno ya tembo yenye thamani ya shilingi za kitanzania zaidi ya milioni 34.

Watu hao ni Abubakar Msangi na Yazidu Njunju, ambao wamesomewa mashtaka hayo mbele ya hakimu mkazi Cassian Matembele na wakili wa serikali mwandamizi Wankyo Simon na kudai kuwa upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika na kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 7,mwaka huu.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka ya washtakiwa wote kwa pamoja wanadaiwa kutenda kosa hilo tarehe 16,Oktoba 2020, ndani ya wilaya ya Temeke katika mkoa wa Dar es salaam ambapo walikutwa na vipande saba vya meno ya Tembo vyenye thamani ya shilingi za kitanzania 34,293,000 bila kuwa na kibali kutoka maliasili.

Aidha Hakimu Matembele amedai kuwa makosa hayo hayana dhamana hivyo washtakiwa wamerudishwa rumande hadi hapo kesi itakapotajwa tena.
Picha tafadhali
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom