Mbaroni kwa kukutwa na magogo ya sh milioni 383

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
2,774
2,000
SERIKALI imemfikisha mahakamani mfanyabiashara, Edgael Lema (43) akikabiliwa na mashtaka nane ikiwemo kukutwa na kontena 18 za magogo yenye thamani ya Sh milioni 383.

Mfanyabiashara huyo alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jana mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Vicky Mwaikambo.

Wakili wa Serikali Mwamdamizi, Maternus Marandu, akimsomea mashtaka alidai mshtakiwa ambaye ni Mkazi wa Goba anadaiwa kuongoza genge la uhalifu, kusafirisha magogo, kugushi, kutoa nyaraka za uongo, kukwepa kodi na utakatishaji wa fedha.

Marandu alidai katika shtaka la kwanza kati ya Novemba 2015 na Januari 2016 maeneo yasiyojulikana nchini Tanzania, mshtakiwa akiwa na watu wengine ambao hawapo mahakamani hapo, walijipanga kuongoza genge la uhalifu huku wakijua kufanya hivyo ni kosa la kisheria.

Katika kosa la pili kati ya Novemba 2015 na Januari 2016 maeneo tofauti jijini Dar es Salaam, mshtakiwa huyo akiwa na watu wengine ambao hawapo mahakamani wanadaiwa walisafirisha kontena 18 yenye vipande 5,296 vya magogo aina ya mkurungu yenye thamani ya Sh 383,140, 840 ambazo ni mali ya Tanzania bila ya kupewa kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa Maliasili.

Shtaka la tatu na la nne ni la kugushi ambapo kati ya Mei 14 mwaka 2015 na Machi 16 mwaka 2015 maeneo yasiyojulikana nchini Tanzania, mshtakiwa huyo akiwa na watu wengine ambao hawapo mahakamani wanadaiwa kutengeneza nyaraka za uongo wakijaribu kuonyesha kuwa imetolewa na ofisi ya Serikali ya Zambia huku wakijua si kweli.

Katika shtaka la tano na sita inadaiwa tarehe isiyojulikana makao makuu ya Bandari ya Dar es Salaam, mshtakiwa akiwa na watu wengine ambao hawapo mahakamani wakijua ni udanganyifu walitoa nyaraka za uongo kwenye ofisi hiyo wakionyesha nyaraka hizo zimetolewa na ofisi ya Serikali ya Zambia huku wakijua si kweli.

“Shtaka la saba inadaiwa kati ya Novemba 2015 na Januari 2016 maeneo ya Jiji la Dar es Salaam mshtakiwa akiwa na nia ya kukwepa kodi alitoa nyaraka za uongo ili kukwepa kulipa kodi ya Sh 383, 140, 840 huku akijua kufanya hivyo ni kosa la kisheria.

“Shtaka la mwisho kati ya Novemba 2015 na Januari 2016 jijini Dar es Salaam mshtakiwa anadaiwa kujipatia Sh 383, 140, 840 huku akijua fedha hizo zilikuwa zimetokana na uhalifu wa kukwepa kulipa kodi,”alidai.

Wakili Marandu alidai upelelezi haujakamilika anaomba tarehe nyingine ya kutajwa.

Mshtakiwa hakuruhusiwa kujibu kitu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi ya uhujumu uchumi.

MTANZANIA
 
Perfectz

JF-Expert Member
May 17, 2017
7,016
2,000
Wakili wa Serikali Mwamdamizi, Maternus Marandu, akimsomea mashtaka alidai mshtakiwa ambaye ni Mkazi wa Goba anadaiwa kuongoza genge la uhalifu, kusafirisha magogo, kugushi, kutoa nyaraka za uongo, kukwepa kodi na utakatishaji wa fedha.
 
Complex Analysis

JF-Expert Member
May 9, 2020
219
500
Mbona sijaelewa kitu kakamatwa na magogo yenye thamani ya milioni 383...mara kakwepa kodi ya milioni 383???how comes mzigo wa milioni 383 kodi yake ni milioni 383

Alafu hapohapo unasikia sjui kuongoza genge la uhalifu,kiukweli toka moyoni i smell something fishy..

kuna watu wamekuwa wakibambikiwa sana kesi zenye nia ya kuwakomoa na kuwanyima dhamana..MUNGU YUPO NA ANAONA WALE WOTE WANAOTUMIA NAFASI ZAO KUKANDAMIZA WENGINE HUKU MOYONI MWAO WANAJUA KABISA WANACHOFANYA NI KITENDO CHA UONEZI NA DHULUMA
 
J C

JF-Expert Member
Dec 12, 2013
2,706

Ipo siku yatakwisha hukumu ya Mungu huja taratibu pale uovu wao utapojaa ktk kikombe cha gadhabu yake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
chakii

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
18,922
2,000
Mbona sijaelewa kitu kakamatwa na magogo yenye thamani ya milioni 383...mara kakwepa kodi ya milioni 383???how comes mzigo wa milioni 383 kodi yake ni milioni 383

Alafu hapohapo unasikia sjui kuongoza genge la uhalifu,kiukweli toka moyoni i smell something fishy..

kuna watu wamekuwa wakibambikiwa sana kesi zenye nia ya kuwakomoa na kuwanyima dhamana..MUNGU YUPO NA ANAONA WALE WOTE WANAOTUMIA NAFASI ZAO KUKANDAMIZA WENGINE HUKU MOYONI MWAO WANAJUA KABISA WANACHOFANYA NI KITENDO CHA UONEZI NA DHULUMA
Kesi ni moja ila ina sura tofauti tofauti na mwisho ni hasara ya Milioni 383+ ambayo serikali imepata
 
TumainiEl

JF-Expert Member
Jan 13, 2010
4,571
2,000
SERIKALI imemfikisha mahakamani mfanyabiashara, Edgael Lema (43) akikabiliwa na mashtaka nane ikiwemo kukutwa na kontena 18 za magogo yenye thamani ya Sh milioni 383.

Mfanyabiashara huyo alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jana mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Vicky Mwaikambo.

Wakili wa Serikali Mwamdamizi, Maternus Marandu, akimsomea mashtaka alidai mshtakiwa ambaye ni Mkazi wa Goba anadaiwa kuongoza genge la uhalifu, kusafirisha magogo, kugushi, kutoa nyaraka za uongo, kukwepa kodi na utakatishaji wa fedha.

Marandu alidai katika shtaka la kwanza kati ya Novemba 2015 na Januari 2016 maeneo yasiyojulikana nchini Tanzania, mshtakiwa akiwa na watu wengine ambao hawapo mahakamani hapo, walijipanga kuongoza genge la uhalifu huku wakijua kufanya hivyo ni kosa la kisheria.

Katika kosa la pili kati ya Novemba 2015 na Januari 2016 maeneo tofauti jijini Dar es Salaam, mshtakiwa huyo akiwa na watu wengine ambao hawapo mahakamani wanadaiwa walisafirisha kontena 18 yenye vipande 5,296 vya magogo aina ya mkurungu yenye thamani ya Sh 383,140, 840 ambazo ni mali ya Tanzania bila ya kupewa kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa Maliasili.

Shtaka la tatu na la nne ni la kugushi ambapo kati ya Mei 14 mwaka 2015 na Machi 16 mwaka 2015 maeneo yasiyojulikana nchini Tanzania, mshtakiwa huyo akiwa na watu wengine ambao hawapo mahakamani wanadaiwa kutengeneza nyaraka za uongo wakijaribu kuonyesha kuwa imetolewa na ofisi ya Serikali ya Zambia huku wakijua si kweli.

Katika shtaka la tano na sita inadaiwa tarehe isiyojulikana makao makuu ya Bandari ya Dar es Salaam, mshtakiwa akiwa na watu wengine ambao hawapo mahakamani wakijua ni udanganyifu walitoa nyaraka za uongo kwenye ofisi hiyo wakionyesha nyaraka hizo zimetolewa na ofisi ya Serikali ya Zambia huku wakijua si kweli.

“Shtaka la saba inadaiwa kati ya Novemba 2015 na Januari 2016 maeneo ya Jiji la Dar es Salaam mshtakiwa akiwa na nia ya kukwepa kodi alitoa nyaraka za uongo ili kukwepa kulipa kodi ya Sh 383, 140, 840 huku akijua kufanya hivyo ni kosa la kisheria.

“Shtaka la mwisho kati ya Novemba 2015 na Januari 2016 jijini Dar es Salaam mshtakiwa anadaiwa kujipatia Sh 383, 140, 840 huku akijua fedha hizo zilikuwa zimetokana na uhalifu wa kukwepa kulipa kodi,”alidai.

Wakili Marandu alidai upelelezi haujakamilika anaomba tarehe nyingine ya kutajwa.

Mshtakiwa hakuruhusiwa kujibu kitu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi ya uhujumu uchumi.

MTANZANIA
wana kas tukumbuke ile story ya Mfalme alie kuwa hamjuwi Yusuph. Aliwapa tabu sana Israel kiasi walilia nakukumbuka nyumbani. Mafalme aliwapa kazi ngumu na ateso makali ilifika mahali walijuta. Kilio chao kilikuwa kikuu kikamfikia Mungu ndipo akamtuma Musa kuwaokoa. Ndugu wana wakusi kama Nikweli au ni uwongo ila vilio vitafika Mbinguni.
 
Complex Analysis

JF-Expert Member
May 9, 2020
219
500
Kesi ni moja ila ina sura tofauti tofauti na mwisho ni hasara ya Milioni 383+ ambayo serikali imepata
ukisoma maelezo ya hiyo habari kuna mapungufu mengi sana,any way hapa duniani tunapita mwisho wa siku kila mtu mungu atamlipa kutokana na anayoyafanya kwa wakati wake
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom