Mbaroni kwa kujifanya Ofisa Usalama wa Taifa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbaroni kwa kujifanya Ofisa Usalama wa Taifa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by sir.JAPHET, Aug 18, 2012.

 1. sir.JAPHET

  sir.JAPHET JF-Expert Member

  #1
  Aug 18, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 700
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  [h=2][/h] Ijumaa, Agosti 17, 2012 07:24 Na Abraham Gwandu, Arusha

  JESHI la Polisi mkoani Arusha linamshikilia Faraji Majid (35) mkazi wa Dar es Salaam kwa tuhuma za kujaribu kutapeli Sh milioni 150 kutoka kwa wafanyakazi wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania ( TANAPA).

  Majid akiwa na mtuhumiwa mwingine, Seleman Wambura ambaye alitoroka, walitaka viongozi wa TANAPA kutoa kiasi hicho cha fedha kama wanataka "mambo" yao yasifike ngazi za juu.

  Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Zuberi Mwombeji, tukio hilo lilitokea katika ofisi za shirika hilo wakati watuhumiwa hao walipojitambulisha kama wafanyakazi wa Ofisi ya Rais kikosi maalumu cha kudhibiti rushwa na fedha haramu (ant-money laundering and combating of illegal financing).

  "Ni kweli tunamshikilia Faraji Majid ambaye taarifa za awali zinaonyesha ni tapeli wa kimataifa na ameshafanya matukio mengi ya utapeli. Tunaendelea kumhoji halafu tutamfikisha mahakamani huku tukiwasaka wengine, akiwamo Wambura aliyetoroka," alisema Kamanda Zuberi.

  Mmoja wa watumishi ambao walikuwa wanatafutwa na watu hao aliiambia MTANZANIA kuwa ‘matapeli’ hao waliwataka kujaza fomu maalumu ambayo ni tofauti na ile ya maadili ya viongozi wa umma, huku wakitaka kujua chanzo cha utajiri walionao.

  "Walikuja ofisini nikawapokea kama wageni wengine na nikataka waeleze kilichowaleta ofisini kwangu, cha kushangaza walianza kunitisha kwamba wametoka Ofisi ya Rais, kwa hivyo wanataka nieleze nimepata wapi fedha za kujenga nyumba na gari ninalomiliki, nikashangaa!" alieleza na kuongeza:

  "Wakati wananihoji wakatoa fomu hiyo ya kujaza, nikawauliza wanaihitaji lini, kwani dodoso lilikuwa refu na baadhi ya vitu vilihitaji muda kuvikumbuka, lakini kilichonishangaza wakasema wanataka nijaze vitu ninavyokumbuka, kwani wana haraka, hapo nikajua hawa ni matapeli.

  "Nilipoona vitisho vyao nikawaomba nikutane nao nje ya ofisi za shirika wakati wa jioni ili nipate fursa ya kuripoti tukio hilo ngazi zinazohusika kwa sababu tayari nilishawatilia shaka kwamba si wafanyakazi wa Ikulu, hata vitambulisho vyao vinatia shaka.

  "Kabla ya kukamatwa, tulikutana nao pale wakatuambia kwamba sisi wote ni Watanzania na wao hawataki kutuharibia kazi zetu, hawataki waturipoti ngazi za juu na kama tunataka kuendelea na kazi tumalizane kwa maana tuwape fedha nyingi zaidi ya Sh milioni 150 ili watuache."
   
 2. M

  Mlyafinono Senior Member

  #2
  Aug 18, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 177
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Rama hayumo kwenye hilo sakata?
   
 3. Kakende

  Kakende JF-Expert Member

  #3
  Aug 18, 2012
  Joined: Aug 18, 2012
  Messages: 2,734
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Watu kujifanya usalama wa Taifa na kuja kwa staili ya kuuliza utajiri wa wafanya kazi inaonekana ni jinsi gani wafanyakazi wa serikali ni wezi wa kutupa, nenda Mbezi beach Dar na Njiro Arusha uone wafanyakazi ambao hata mshahara wao haufiki 500000 walivyofanya matusi?
   
 4. kupe

  kupe JF-Expert Member

  #4
  Aug 18, 2012
  Joined: Jul 26, 2012
  Messages: 1,025
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  hao usalama fake ni wezi na hao tanapa ni wezi inabidi polisi iwakamate wote tu
   
 5. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #5
  Aug 18, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,314
  Likes Received: 5,605
  Trophy Points: 280
  Hao wamekosea kidogo timing tu,wenzao huwa hawaendi hivyo na kila siku wanawapiga wezi wa mashirika ya umma.pesa haramu inaibiwa kiharamu pia!siku zao zimefikia mwisho acha sheria iwahukumu sasa!ingawa najua ushahidi mgumu kidogo na wao wako smart sana!haow ana mtandao lazima kazi si ndogo ati! Ni hatari sana hao jamaa huwa wanajitambulisha na kutoa vitambulisho kabisa vinavyofanana na vya TISS.
   
Loading...