Mbaroni Kwa Kufukua Makaburi na Kuiba Mifupa ya Maiti

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,268
33,040
Mbaroni Kwa Kufukua Makaburi na Kuiba Mifupa ya Maiti
6055850.jpg
Thursday, November 10, 2011 1:05 AM
Polisi nchini Pakistan wamewatia mbaroni watu wawili kwa tuhuma za kufukua makaburi yapatayo 40 na kuiba mifupa ya maiti.
Baada ya makaburi mengi kufukuliwa na mifupa ya maiti kuibwa, polisi nchini Pakistan wamewatia mbaroni watu wawili kwa tuhuma za kufukua makaburi na kuiba mifupa ya maiti.

Wanaume hao walivamiwa na polisi usiku wa manane wakati walipokuwa wakifukua makaburi ya Gulshan-e-Maymar ya jiji la Karachi ili waibe mifupa ya maiti.

Polisi walianza msako wa kuwatafuta watu wanaoiba mifupa ya maiti baada ya makaburi yapatayo 40 kufukuliwa na mifupa ya viungo mbalimbali vya maiti kuibwa.

Polisi waliovaa nguo za kiraia walianza msako kwenye makaburi ya jijini Karachi baada ya siku ya jumatatu makaburi kwenye mji wa Gadap kukutwa yakiwa yamefukuliwa huku baadhi ya viungo vya maiti vikiwa vimenyofolewa.

Televisheni ya Dunya ya nchini Pakistan ilisema kuwa watuhumiwa waliwaambia polisi kuwa viungo vya maiti walikuwa wakiviuza kwa waganga.

Kumekuwa na matukio mengi ya imani za kishirikina nchini Pakistan ambapo baadhi ya watu wamekuwa wakienda kwa waganga ambao wamekuwa wakiahidi kuwa wana uwezo wa kutibu maradhi mbalimbali sugu.

Waganga hao wamekuwa wakidai kuwa kwa kutumia siri zao za uganga, wana uwezo wa kutibu maradhi sugu, kuwaroga maadui, kuleta bahati kwenye maisha na pia kuyarudisha mapenzi pale mahusiano yanapovunjika.


Chanzo: Mbaroni Kwa Kufukua Makaburi na Kuiba Mifupa ya Maiti
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom