Mbarawa: Asilimia 80 ya watanzania wapata maji

esther mashiker

JF-Expert Member
May 29, 2018
616
552
1087535


WIZARA ya Maji imewasilisha makisio ya bajeti ya wizara hiyo, ambayo ni zaidi ya Sh bilioni 634.196. Fedha zilizotengwa kwa ajili ya maendeleo ni Sh bilioni 610.469, zitakazotumika kukamilisha miradi mbalimbali ya maji nchini.

Aidha, upatikanaji wa maji katika maeneo ya vijijini, umeongezeka mwaka mmoja uliopita kutoka asilimia 58.7 hadi asilimia 64.8 huku wa mijini ikika asilimia 80 Akisoma hotuba ya Bajeti ya mwaka 2019/20, Waziri wa Maji, Profesa Mbarawa alisema kiasi hicho cha fedha, kimelenga kukisha majisa na salama kwa asilimia 85 kwa vijijini na asilimia 90 kwa mjini ikapo mwaka 2020.


Kati ya fedha zilizoombwa, zaidi ya Sh bilioni 23.7 zitatumika kwa ajili ya matumizi ya kawaida na fedha za mshahara kwa wafanyakazi za wizara na chuo cha maji. “Kati ya fedha za maendeleo Sh bilioni 610.469 za maendeleo, Sh bilioni 349.449 sawa na asilimia 57 ni fedha za ndani na Sh bilioni 261.020 sawa na asilimia 43 ni fedha za nje,” alisema.

Katiba hotuba yake, Mbarawa alisema miradi inayotarajiwa kutekelezwa kwa mwaka wa fedha ni pamoja na utafutaji wa vyanzo vipya vya maji. Aidha, serikali kwa kushirikiana na Serikali ya Oman, itachimba visima 100 kwa ajili ya kusambaza maji katika shule za sekondari na msingi.

Katika kukia azma hiyo, maeneo 98 katika shule za msingi 58 na sekondari 40 yalifanyiwa utati kwa ajili ya kuchimba visima. Pia serikali itatekeleza mradi wa kuboresha huduma ya uondoaji majitaka kwa kushirikiana na Serikali ya Korea Kusini, utakaogharimu dola za Marekani milioni 90.

Alisema hadi Aprili mwaka huu, mtaalamu mshauri atakayesimamia mradi huo amepatikana na ameanza kazi ya mapitio ya usanifu wa kina na kuandaa makabrasha ya zabuni “Mradi huu utahusisha ujenzi wa mfumo wa majitaka wa mabomba yenye urefu wa kilometa 376 kutoka maeneo ya katikati ya jiji, Ubungo, Kinondoni, Mwananyamala, Msasani na Ilala hadi kwenye mtambo wa kusasha majitaka utakaojengwa eneo la Jangwani,” alieleza.

Alisema kuwa mtambo utakuwa na uwezo wa kusasha lita milioni 200 za maji taka kwa siku. Vilevile alisema ujenzi wa mradi huo, utahusisha kubadili mwelekeo wa bomba linalomwaga majitaka baharini na kuyapeleka kwenye mtambo wa Jangwani. “Ujenzi wa mradi unatarajiwa kuanza katikati ya mwaka 2019/20 na serikali imetenga Sh bilioni 10 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo.

Profesa Mbarawa alisema hadi kukia Aprili mwaka huu jumla ya miradi ya maji 1,659 yenye vituo vya maji 131,370 imejengwa. Kati ya vituo vilivyojengwa, vituo 86,780 vinafanya kazi na uwezo wa kuwahudumia watu watu 25,359,290 ambao ni sawa na asilimia 64.8 ya wananchi waishio vijijini.

Akiwasilisha maoni ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, Mahmoud Mgimwa aliomba serikali kuongeza tozo kutoka Sh 50 hadi Sh 100 kutoka kwenye mafuta au chanzo kingine kwa ajili ya kuongeza fedha zitakazogharamia miradi ya maji kupitia Mfuko wa Taifa wa Maji. “Kwa miaka mitatu sasa kamati imekuwa ikiishauri serikali kuimarisha makusanyo ya Mfuko wa Taifa wa Maji kwa kuongeza tozo ya mafuta kwa kila lita ya petroli na diseli kutoka shilingi 50 hadi shilingi 100. Kutotekelezwa kwa ushauri huo kunaathiri ufanisi wa utekelezaji wa miradi ya maji hususan kwa maeneo ya vijijini” alisema.
 
vijijini upatikanaji wa maji ni mgumu sana tena sana, labda mijini kuna unafuu lakini si vijijini,serikali pia iingie vijijini isaidie watu hali ya upatikanaji wa maji ni tishio.
 
vijijini upatikanaji wa maji ni mgumu sana tena sana, labda mijini kuna unafuu lakini si vijijini,serikali pia iingie vijijini isaidie watu hali ya upatikanaji wa maji ni tishio.
Moja ya Tatizo la vijijini wanavijiji wametawanyika Sana yaani utakuta unatumia pesa nyingi kupeleka maji Kwa watu wachache Sawa na umeme
Unakula unaweza transform ya kuwatosheleza wakazi laki mbili lakini wanaotumia umeme ni watu wasiozidi 20 ktk kijiji kimoja
 
Back
Top Bottom