MBARALI RAHA: Polisi wameua na Wananchi wateketeza KITUO CHA MAFUTA!

Serikali ya Mbarari inashangaza sana, kilichotaikwa si kukutaza magari, walitakiwa kuimarisha barabara ili magari yapite maana mbarari kuna vitu muhimi ikiwemo mpunga, namshangaa pinda anasisitizia kilimo kwanza wakati miundo mbinu mibuvu, na magufuli nae amekomalia barabra za mjin tu, mwisho poleni wana mbarari, lakini kamwe msiache kupigania haki yenu,
 
Kweli nchi hii tuna kazi.hatuna polisi,mahakama,raisi wala wabunge na mawaziri.wote bongolala tu.
 
hiyo ndio serikali yetu ndg zangu, sijajua tunafanyaje na huu uozo wa kushambulia kwa risasi za moto. nina hofu jeshi letu la polisi limezidiwa na risasi nyingi sana maghalani sasa wameamua kuanza kuzitumia kwa fujo. SHAME ON U, MUNGU AWAHUKUMU APENDAVYO
 
Hivi rules za engagement za jeshi la polisi zinasemaje katika tukio kama hili?
 
viongozi wa serikali huwa wanajifanya hawaamini kuwa sheria zinawahusu masikini ingawa mkulu alishakili enzi za vuguvugu la mabilioni ya EPA kuwa tukiwapeleka mahakamani tutapoteza kilakitu kwakuwa watu hao wanafedha nyingi wanaweza kuishinda serikali na hatimae kutakiwa kulipwa tena!.sasa jeshi la polisi limeshindwa kuilinda barabara zidi ya matajiri wenye magari yenye uzito zidi ya tani 8 hatimae raia wakaamua kuilinda!.
polisi badala ya kuwasaidia wenyewe wanawauwa tena walinzi wa barabara, je hii si dalili tosha kuwa nchi imeshauzwa na walionunua tunao humuhumu bongo!
poleni sana nduguzetu wa mbarali!. na hongereni kwa uzalendo mliouonyesha dhidi ya rasilimali za umma!
polisi wameshindwa kulinda malizetu sasa raia wameanza kutekeleza wajibu wao!
 
Kinachotokea Mbarali, latest info: Nimepokea taarifa kutoka kwa mtu aliye mkutanoni wakati huu. Kuwa DC akiongozana na Mbunge wamefika Ubaruku. DC anasema Serikali na wananchi wamefanya makosa. Wananchi wanakataa. Wanamwambia: " Tunataka mashamba yetu!". Wana mabango pia na maandishi hayo. Na hivi sasa wananchi wanaandamana kuele...kea Rujewa. Huko kuna mwili wa marehemu ambao utasafirishwa kwenda Lupembe, Njombe.
 
Watu sasa wameamua kuchua hatua mkononi kwa sababu wanaona serikali hawasikilizi sauti zao.

Inasikitisha, na huyu JK asipokuwa makini, nchi haitakalika.
 
Ndio matokeo ya kuchagua CCM na Kikwete. Wanafikiri wenyewe haki ya kutumia barabara ni wao na wawekezaji!
 
Kinachotokea Mbarali, latest info: Nimepokea taarifa kutoka kwa mtu aliye mkutanoni wakati huu. Kuwa DC akiongozana na Mbunge wamefika Ubaruku. DC anasema Serikali na wananchi wamefanya makosa. Wananchi wanakataa. Wanamwambia: " Tunataka mashamba yetu!". Wana mabango pia na maandishi hayo. Na hivi sasa wananchi wanaandamana kuele...kea Rujewa. Huko kuna mwili wa marehemu ambao utasafirishwa kwenda Lupembe, Njombe.

Lakini Maggid ulishawahi kulizungumzia hili suala la mashamba hapa, kwa nini serikali wanakuwa wagumu kuwasikiliza wananchi? Nadhani Tanzania inaelekea pabaya, Viongozi wameweka pamba masikioni na wanachi wameanza kudai haki zao...
 
magari ya kumwaga maji ya pilipili ni gharama sana kuyanunua kuliko risasi. Majidi endelea kula displini kwa ulichokipanda octoba'10 sasa inakula kwako
 
Kwa sehemu kubwa,nyuma ya migogoro ya ardhi tunayoiona sehemu zinazozalisha vizuri kuna vigogo wa serikali ndani yake, wageni tunawasingizia ili kuficha ukweli. Mbalari napafahamu vizuri na jinsi ardhi ilivyo ajenda ngumu kwa wanavijiji wale. Ukiachia mbali ardhi iliyonyang`anywa na mafisadi,bado kuna vijiji kadhaa vitafutwa kupisha upanuzi wa mbuga ya Ruaha, tayari Ihefu imemeza bonde kubwa, na madibira wanaanza kujengwa bwawa kubwa kabisa ambalo litachukua vijiji kadhaa ili kupisha bwawa hilo, ukienda Chimala, kuna kapunga rice farm ambalo nalo ni kilio kila uchao.

Wanasiasa wanatuua jamani kwa tamaa zao, pili ujinga/woga wetu ndio matatizo/umaskini wetu. Mbalari ni noma tupu jamani.
 
magari ya kumwaga maji ya pilipili ni gharama sana kuyanunua kuliko risasi. Majidi endelea kula displini kwa ulichokipanda octoba'10 sasa inakula kwako

Umenifanya nicheke sana, kwani Maggid alipanda nini? Au ni wakati ule alikuwa akizungumzia chama ni itikadi na sio mtu?
 

Ndugu Zangu,

Babu yangu alipata kutafsiri kwa watu wake kauli ya DC: " Idzi Ilogola umujetu si monga ukweli, si monga la" ( Kisangu) Maana yake:

- Anayoongea huyu mwenzetu mengine ya ukweli, na mengine ni uongo.

Msingi wa tafsiri hiyo ni kuwataka watu wake wafikiri kwa bidii na wapime wenyewe. Kuna vurugu zimeripotiwa kule kwetu Mbarali. Kijana mmoja amepoteza uhai jana jioni: Justin, amepigwa risasi ya kichwa na ubongo kufumuka. Hassan, amejeruhiwa vibaya kwa kupigwa risasi ya kiuno. Kosa lao: Kuhoji mamlaka, polisi.

Mbarali ni kwetu. Nimefika Mbarali mara kwa mara. Nimewasikia WanaMbarali wanaonung'unika. Nimeandika makala kadhaa kuelezea kilio cha WanaMbarali. Kwangu mimi, kilichotokea jana ilikuwa ni suala la wakati tu. Na mamlaka husika zisipolifanyia kazi haraka hili la Mbarali, nahofia madhara zaidi kutokea.

Hivi sasa kule Mbarali kuna marufuku ya magari makubwa kufika Rujewa na Ubaruku kusomba mazao kwa vile yanaharibu barabara. Marufuku hiyo ina karibu mwezi mmoja sasa. Hali hiyo inamfanya mkulima wa mpunga Mbarali kuuza kilo yake ya mchele kwa shilingi 650 mpaka 700 badala ya elfu moja.

Wachuuzi wa mchele wanadai wanafidia gharama ya kukodi magari madogo kusomba magunia ya mchele mpaka barabara kuu pale Igawa. Mkulima huyu kwa kuuza kilo ya mchele kwa shilingi mia saba ina maana ya kupunjika zaidi. Faida yake ukitoa gharama zote inabaki kuwa shilingi mia au hata shilingi 80 kwa kilo. Mkulima huyu anahitaji kumsomesha mwanawe pia.

Wanambarali wanashangaa na kuhoji, iweje marufuku ya malori makubwa ipigwe na wakai huo huo wanaona malori makubwa ya mafuta yanapita barabara hiyo hiyo kupelekea mafuta kwa wenye biashara hiyo. Ndio sababu ya baadhi wenye hasira, jana wakafikia hatua ya kusimamisha lori hilo na kuhoji. Wenzao wakapigwa risasi. Ndipo wananchi kwa hasira wakachoma moto lori la mafuta na kituo cha mafuta.

Ndio, kilichofuatia ni majonzi makubwa. Tunalaani tena mauaji yale yaliyofanywa na polisi wetu. Bomu la machozi lilitosha kuwatawanya waliokusanyika badala ya kutumia risasi za moto. Kulikoni jeshi la polisi?


Na sasa kuna taarifa zinatolewa. Kuna ya ukweli, kuna ya kupotosha. WanaMbarali wanaujua ukweli. Wana kilio. Ni kilio cha haki. Wanahitaji mtu wa kwenda kuwasikiliza. Autafute ukweli. Kisha itafutw suluhu ya mgogoro unaofukuta kabla maafa makubwa zaidi hayajatokea. Inahusu ardhi. Mashamba yao, binafsi na ya umma yaliyouzwa kwa wawekezaji katika hali ya utata. Wawekezaji wanaowanyanyasa WanaMbarali ikiwamo kuwafungia wananchi maji ya mifereji kwa mashamba yao ya mpunga.

Ndio, inahusu hali za wakulima na wafugaji wa bonde la Usangu. Serikali iingilie kati sasa kuwasaidia watu wake wa Mbarali badala ya kuwalazimisha kuchukua hatua wenyewe. Hatujachelewa.


Maggid
Iringa
mjengwa

mkuu nimekupa lihasante hapo juu.
But mkuu hii si ndo serikali uliyokuwa unaitaka huwezi kuandika barua kwa mjomba ili awasaidie ndugu zetu? au hata wewe hakusikilizi??
HUMU SISI TUNAHASILA TUU NA HAPO UNATUONGEZEA HASILA JUU YAKE AU WALIFANYA KAMA ARUSHA, WALIVAMIA!
SERIKALI INALALA NCHI INAANGAMIA.
 
Wana JF,
Nchi imeuzwa, nimeamini sasa. Huko Mbarali, barabara ilifungwa, cha kushangaza tenka la mafuta likapita. Kisha wakaandamana kwa nn linapta. Polisi wakapga risasi wa2 wawili. Sasa wananchi wamenifurahsha, wamechoma hlo TANKER NA KITUO CHA MAFUTA!

badilisha heading unafurahia watu kuuwawa? acha siasa za kitoto
 
Back
Top Bottom