MBARALI RAHA: Polisi wameua na Wananchi wateketeza KITUO CHA MAFUTA! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

MBARALI RAHA: Polisi wameua na Wananchi wateketeza KITUO CHA MAFUTA!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pasco_jr_ngumi, Jan 14, 2011.

 1. Pasco_jr_ngumi

  Pasco_jr_ngumi JF-Expert Member

  #1
  Jan 14, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 1,811
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Wana JF,
  Nchi imeuzwa, nimeamini sasa. Huko Mbarali, barabara ilifungwa, cha kushangaza tenka la mafuta likapita. Kisha wakaandamana kwa nn linapta. Polisi wakapga risasi wa2 wawili. Sasa wananchi wamenifurahsha, wamechoma hlo TANKER NA KITUO CHA MAFUTA!
   
 2. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #2
  Jan 14, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,870
  Likes Received: 4,550
  Trophy Points: 280
  Kama mbwai,mbwai tu. No more talking,actions only.

  AMANDLA.
   
 3. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #3
  Jan 14, 2011
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Aisee kilichobakia nasi raia tutoe magobole yetu:smile-big:
   
 4. ggg

  ggg Member

  #4
  Jan 14, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 60
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
   
 5. spencer

  spencer JF-Expert Member

  #5
  Jan 14, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 2,797
  Likes Received: 1,339
  Trophy Points: 280
  Xactly Maria Roza.

  If its your Right, Baby Don't hestate

  Same Principles should be applied.

  They Hit Us, We Hit Them Back.

  Mbarali Welldone
   
 6. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #6
  Jan 14, 2011
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Chanzo cha machafuko hayo ni nini?
   
 7. Zegreaty

  Zegreaty JF-Expert Member

  #7
  Jan 14, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 638
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  hawa watu naona sasa ni wakutolewa uvivu tu mpaka kieleweke
   
 8. n

  niweze JF-Expert Member

  #8
  Jan 14, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 1,008
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  When JK Will Learn the Bitter Lesson? Is Anyone Saw Jk Recently? Jamani Yupo Wapi Huyu Msanii? Mbona Hakieleweki TZ? Kumbe Msanii Hana Nguvu Tena TZ na Kuna Uwezekano TZ Inaongozwa na Mkuu wa Polisi. "Chadema Washeni Moto na Mikakati ya Kuingia Ikulu Sasa Kabla JK na Kikundi Chake Hakija Vuka Mpaka na Mali za Taifa"" Wananchi Tulinde Nchi Sasa, Wanaondoka Hawa...
   
 9. K

  Karandanya Member

  #9
  Jan 14, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sasa kilichobaki kila mtu asali kwan tunakoelekea hakuna kuonewa tena kwanza bongo hakuna serikali kila mtu ni kiongozi au vp mazee?
   
 10. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #10
  Jan 14, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,484
  Likes Received: 5,869
  Trophy Points: 280
  Polisi waua tena kwa risasi Send to a friend Thursday, 13 January 2011 21:24 0diggsdigg

  Brandy Nelson, Mbeya na Ramadhan Semtawa

  POLISI nchini wameendelea kutumia risasi za moto dhidi ya raia na jana wanadaiwa kuwauwa watu wawili kwa kuwapiga risasi katika vurugu zilizotokea katika wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya.

  Habari kutoka Mbarali zinasema polisi walitumia mabomu ya kutoa machozi na risasi za moto kuzima vurugu ambazo chanzo chake ni mabishano baina ya raia na polisi hao.

  Vurugu hizo zilizotokea jana majira ya saa nane mchana zinadaiwa kusababishwa na baadhi ya wakazi wa kata ya Ubaruku kuzuia kuingia katika eneo lao lori lenye uzito wa zaidi ya tani kumi.

  Baadhi ya walioshuhudia tukio hilo walisema hatua ya wananchi kuzuia kwa lori hilo inatokana na kuwepo kwa amri ya serikali wilayani Mbarali itayokataza magari yenye uzito mkubwa wa zaidi ya tani kumi kuingia katika kata ya Ubaruku.

  Mmoja wa mashuhuda hao alisema lori hilo lilipokuwa likijaribu kuingie katika eneo hilo wananchi walianza kulizuia huku wakimhoji dereva wake sababu za kuvunja amri iliyopo.

  "……walipokuwa wakiendelea kuhojiana na dereva, polisi walifika hapo na hapo wananchi wakaanza kuwauliza polisi sababu za kuruhusu gari kuingie katika eneo lao wakati serikali imeishakataza..," alisema shuhuda huyo na kuongeza:

  " ni kama polisi na wananchi walishindwa kuelewana lugha hapo tukaanza kusikia mabomu ya machozi na risasi…".

  Alisema hatua ya polisi iliwafanya wananchi kutawanyika na wengine kuanza kuyavamia magari yaliyokuwa kwenye kituo cha mafuta likiwemo gari lililosababisha mvutano huo.

  Katika tafrani hiyo magari mawili yaliyokuwa kwenye kituo cha mafuta yalichomwa moto. Magari hayo yanasadikiwa kuwa ni mali ya ndugu wa mwekezaji katika shamba la mpunga la Mbarali.

  Mkuu wa Wilaya ya Mbarali, Kanali Cosmas Kayombo alipohojiwa alikiri kupata taarifa hizo lakini akadai kwamba yuko mbali na tukio hilo na amedai kuwa amewasiliana na mbunge jimbo la Mbarali Dickson Kulufi afike eneo la Tukio.

  Kamanda wa polisi Mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi alipohojiwa alisema kuwa analifuatilia tukio na mpaka tunakwenda mitamboni tayari gari nne mbili zikiwa zimebeba askari wa kutuliza ghasia (FFU), moja ikiwa imebeba polisi waliovalia kiraia huku wakiongozwa na king`ora kikipiga kelele zikiwa zinaelekea eneo la tukio.

  JESHI la Polisi limesema jiji la Arusha sasa liko shwari baada ya vurugu zilizotokea Januari 5 mwaka huu lakini, Kurugenzi ya Makosa ya Jinai inaendelea na uchunguzi kubaini kama kuna makosa mengine ya kijinai dhidi ya viongozi wa Chadema.

  Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa polisi, Paul Chagonja, aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa polisi hawawezi kuzuia haki za watu lakini pia ifahamike kuwa wana wajibu wa kulinda usalama wa wengine.

  "Operesheni ya kurejesha amani na utulivu imekamilika na hivi sasa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai kwa kushirikiana na timu ya wadau wengine wa Usalama kama vile Haki Jinai, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali bado wanaendelea na uchunguzi,

  ... ili kuona matukio yoyote ya makosa ya kiutendaji na makosa mengine ya kijinai yaliyotendwa kwa upande wa Chadema na viongozi wao."

  Kamishna huyo aliwaonya watu aliowaita wanasiasa wanaojaribu kutumia nguvu ya umma kujipatia umaarufu na kudharau mamlaka zilizopo akisema watashughulikiwa.

  "Eti wapo wanaosema nchi haitawaliki,... sisi tunasema sheria zipo na wanaotaka kuingia madarakani wasubiri uchaguzi wa 2015. Watu wanapaswa kutambua mamlaka ya polisi, tuko kulinda mamlaka halali ya Jamhuri ya Muungano. Hata wakiingia wapinzani polisi tutakuwepo na tutalinda mamlaka halali," alisisitiza Chagonja.

  Chagonja ambaye alifanya mkutano huo kutoa kile alichokiita ufafanuzi wa upande wa polisi baada ya kuwepo taarifa za upande mmoja, alitumia picha hizo zilizorekodiwa katika vurugu kuonyesha chanzo cha mauaji hayo na kwamba viongozi wa Chadema wanapaswa kulaumiwa na sasa wanajibaraguza baada ya kumwaga damu.

  "Kufuatia hamasa hiyo wafuasi wa Chadema wanaokadiriwa kuwa zaidi ya 3,000 waliitikia wito wa viongozi hao na kuanza kuelekea kituo kikuu cha polisi Arusha, ili kwenda kuwatoa kwa nguvu watuhumiwa waliowekwa mahabusu kama walivyoazimia mkutanoni, lakini hili halisemwi... watu wanazungumza ya upande mmoja tu," alifafanua Chagonja huku akiwaonyesha waandishi wa habari picha kupitia kwenye kompyuta.

  Akirejea mchakato mzima wa maombi ya kibali cha mkutano, Chagonji alisema jeshi hilo wilayani Arusha lilipokea barua ya Chadema kuomba kibali cha maandamano hayo mnamo Desemba 31 mwaka jana, yenye kumbukumbu namba CDM/AR/W/20/10, ikitoa taarifa ya dhamira hiyo kufanya maandamano Januari 5, 2011.

  Kamishna huyo alianisha maeneo ambayo Chadema iliomba kupita maandamano hayo kwamba ni kuanzia Philips, kuelekea Sanawari, Mianzini, Kituo Kikuu cha mabasi kuelekea mnara wa Azimio, kupitia polisi, Manispaa, Clock Tower kushukia barabara ya Sokoine kisha Friends corner na kuingia viwanja vya NMC.

  "Mkuu wa Polisi wilaya ya Arusha mjini baada ya kupokea barua hiyo, aliwajibu Chadema kwa barua Kumb Na AR/B.5/Vol11/63 ya tarehe 4 Januari 2011, akiwaruhusu kufanya maandamano na mkutano tarehe 5 Januari, 2011, lakini akiwataka warejee mazungumzo ya ana kwa ana yaliyofanyika tarehe 3 Januari 2011 ofisini kwa kamanda wa polisi mkoa yakihusisha viongozi wa chama hicho na polisi," alifafanua.

  Aliongeza kwamba, pamoja na mambo mengine mazungumzo hayo yalibainisha umuhimu wa kuchagua njia moja itakayotumika katika maandamano hayo kati ya njia zilizotajwa kwa ajili ya kuwezesha polisi kuangalia usalama wa mali na raia huku shughuli nyingine za kiuchumi na biashara zikiendelea.

  "Njia hizo ni aidha, itumike kuanzia Philips, Sanawari mataa, kushuka na barabara ya AICC, Goloondoi, barabara ya Sokoine, Friends corner na kuingia uwanja wa NMC, au kuanzia Philips, Sanawari mataa, Florida Annex, Kituo cha mabasi, CRDB benki, Friends Corner hadi uwanja wa NMC, " aliweka bayana na kuongeza,

  ...siku hiyo ya maandamano ilikuwa ni siku ya kazi watu wengine wangekuwa wanaendelea na shughuli zao katika mitaa hiyo, hivyo matumizi ya njia yalipaswa kuzingatia haki za watumiaji wengine ili kuondoa usumbufu usio wa lazima."

  Hali ya miundombinu ya barabara kwa njia ya Arusha ni finyu, hivyo matumizi ya njia mbili kwa wakati mmoja ni wazi yangezuia matumizi ya barabara kwa watumiaji wengine kwa muda mrefu."

  Lakini, Chagonja lisema Januari 3, 2011 mkuu wa polisi wilaya ya Arusha mjini alipokea barua ya Chadema yenye Kumb Na CDM/AR/W/02.1.11 iliyosainiwa na Magoma Derick mwenyekiti wa chama hicho wilaya, ikimjulisha maandamano yataanzia Philips na msafara wa Dk Slaa utaanzia uwanja mdogo wa ndege wa Kisongo huku pia yangekuwepo Annex hoteli na kisha kuelekea NMC.

  Aliongeza, "kwa maana ya barua hiyo siyo tu Chadema hawakuchagua njia mojawapo kama ilivyoelekezwa bali waliongeza njia nyingine ya pili itakayoongozwa na Dk Slaa, kuanzia uwanja wa Kisongo kinyume na maelekezo ya polisi."

  Kaminisha huyo wa operesheni alifafanua, " hata hivyo, wakati mawasiliano hayo yakiendelea taarifa za kiintelejensia zilizokusanywa katika kipindi cha wiki moja kuishia Januari 4, 2011, zilionyesha kuna matishio makubwa ya kiusalama. Matishio hayo yalilenga kuharibu sura ya mji wa Arusha katika uso wa dunia ukizingatia Arusha ni mji wa kibiashara."

  Alisema Chadema ilijulishwa kusitishwa kwa mandamano hayo Januari 4 na ofisi ya Polisi mkoa kwa barua yenye Kumb NaARR/B.5/1.VOL.V111, iliyopokelewa muda wa mchana na diwani Estomi Mala, ambaye alikuwa mjumbe kutoka chama hicho na mgombea nafasi ya umeya wa jiji la Arusha, aliyetumwa kufanya majumuisho na kamanda wa polisi wa mkoa wa Arusha kuhusu maandalizi ya mkutano huo.

  Hata hivyo, alisema manmo Januari tano saa 5:00 asubuhi ndipo viongozi na wanachama wa Chadema isivyo halali wakaanza maandamano kuanzia Mount Meru hoteli kwenda viwanja vya NMC na hapo kutawanywa na polisi kwa amani, kabla ya kauli za kichochezi za Dk Slaa alizotoa kwenye mkutano akiagiza waliokamatwa kwenye maandamano hayo wakakombolewe.

  Katika sehemu ya picha hizo inamuonyesha Dk Willbroad Slaa, akitangazia umati wa vijana uliokuwepo uwanjani hapo kwamba, kabla ya mkutano kumalizika viongozi waliokamatwa na kushikiliwa kituo cha Polisi Kati akiwemo Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema, walipaswa kuachiwa huru na kuwaleta uwanjani hapo.

  Sehemu nyingine ya picha za kwenye mkutano zinamuonyesha Mbunge wa Moshi mjini Philemon Ndesamburo, akilalamika kukumbana na mkono wa chuma wa dola huku akitaja jina la Rais Jakaya Kikwete akisema, "Kikwete Ndesa anapigwa mabomu...aloo Ndesa anapigwa Kikwete... Kikwete wewee humjui Ndesa... Kikwete hujui vurugu za Ndesa alooo?"
   
 11. Fredwash

  Fredwash JF-Expert Member

  #11
  Jan 14, 2011
  Joined: Oct 27, 2009
  Messages: 594
  Likes Received: 161
  Trophy Points: 60
  kilichotokea MBEYA ni kuwa serikali iliweka sheria kuzuia magari yaliyozidi tani kumi kutumia barabara hiyo kwa kuwa yanaharibu barabara (sasa sijui ni kwa nini hasiitengeneze akili za wapi hizi) kwa hiyo ilikuwa inawalazimisha wakulima wa mpunga kubeba mazao yao kwa mikokoteni ili kusafirisha mpunga huo... Sasa juzi wananchi wakaona lori la mafuta linalokadiriwa kuwa na tani kumi au zaidi likipita kwenda kupeleka mafuta somewhere... hapo ndipo wanachi wakahoji iweje lile lori liruhusiwe na wao wakatazwe... then klichofata wanachi wakalizuia polisi kufika kama kawaida wakatumia ubabe... THEN PAKACHIMBIKA........ end of story.. just onether chao of POLICE FORCE
   
 12. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #12
  Jan 14, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Naona kuna haja ya hawa polisi kuwapeleka somalia wawe wanajeshi ndo watumie ipasavyo izo silaha zamoto
  Maana naona wana hamu sana ya vita
   
 13. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #13
  Jan 14, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  I am thinking the same. I dought kama JK atamaliza miaka mitano anaweza kukimbilia west indies.
   
 14. m

  maggid Verified User

  #14
  Jan 14, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180

  Ndugu Zangu,

  Babu yangu alipata kutafsiri kwa watu wake kauli ya DC: " Idzi Ilogola umujetu si monga ukweli, si monga la" ( Kisangu) Maana yake:

  - Anayoongea huyu mwenzetu mengine ya ukweli, na mengine ni uongo.

  Msingi wa tafsiri hiyo ni kuwataka watu wake wafikiri kwa bidii na wapime wenyewe. Kuna vurugu zimeripotiwa kule kwetu Mbarali. Kijana mmoja amepoteza uhai jana jioni: Justin, amepigwa risasi ya kichwa na ubongo kufumuka. Hassan, amejeruhiwa vibaya kwa kupigwa risasi ya kiuno. Kosa lao: Kuhoji mamlaka, polisi.

  Mbarali ni kwetu. Nimefika Mbarali mara kwa mara. Nimewasikia WanaMbarali wanaonung'unika. Nimeandika makala kadhaa kuelezea kilio cha WanaMbarali. Kwangu mimi, kilichotokea jana ilikuwa ni suala la wakati tu. Na mamlaka husika zisipolifanyia kazi haraka hili la Mbarali, nahofia madhara zaidi kutokea.

  Hivi sasa kule Mbarali kuna marufuku ya magari makubwa kufika Rujewa na Ubaruku kusomba mazao kwa vile yanaharibu barabara. Marufuku hiyo ina karibu mwezi mmoja sasa. Hali hiyo inamfanya mkulima wa mpunga Mbarali kuuza kilo yake ya mchele kwa shilingi 650 mpaka 700 badala ya elfu moja.

  Wachuuzi wa mchele wanadai wanafidia gharama ya kukodi magari madogo kusomba magunia ya mchele mpaka barabara kuu pale Igawa. Mkulima huyu kwa kuuza kilo ya mchele kwa shilingi mia saba ina maana ya kupunjika zaidi. Faida yake ukitoa gharama zote inabaki kuwa shilingi mia au hata shilingi 80 kwa kilo. Mkulima huyu anahitaji kumsomesha mwanawe pia.

  Wanambarali wanashangaa na kuhoji, iweje marufuku ya malori makubwa ipigwe na wakai huo huo wanaona malori makubwa ya mafuta yanapita barabara hiyo hiyo kupelekea mafuta kwa wenye biashara hiyo. Ndio sababu ya baadhi wenye hasira, jana wakafikia hatua ya kusimamisha lori hilo na kuhoji. Wenzao wakapigwa risasi. Ndipo wananchi kwa hasira wakachoma moto lori la mafuta na kituo cha mafuta.

  Ndio, kilichofuatia ni majonzi makubwa. Tunalaani tena mauaji yale yaliyofanywa na polisi wetu. Bomu la machozi lilitosha kuwatawanya waliokusanyika badala ya kutumia risasi za moto. Kulikoni jeshi la polisi?

  Na sasa kuna taarifa zinatolewa. Kuna ya ukweli, kuna ya kupotosha. WanaMbarali wanaujua ukweli. Wana kilio. Ni kilio cha haki. Wanahitaji mtu wa kwenda kuwasikiliza. Autafute ukweli. Kisha itafutw suluhu ya mgogoro unaofukuta kabla maafa makubwa zaidi hayajatokea. Inahusu ardhi. Mashamba yao, binafsi na ya umma yaliyouzwa kwa wawekezaji katika hali ya utata. Wawekezaji wanaowanyanyasa WanaMbarali ikiwamo kuwafungia wananchi maji ya mifereji kwa mashamba yao ya mpunga.

  Ndio, inahusu hali za wakulima na wafugaji wa bonde la Usangu. Serikali iingilie kati sasa kuwasaidia watu wake wa Mbarali badala ya kuwalazimisha kuchukua hatua wenyewe. Hatujachelewa.


  Maggid
  Iringa
  mjengwa
   
 15. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #15
  Jan 14, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Maggid

  Unaonekana uko karibu na hawa watu, naomba kueleweshwa lori na kituo cha mafuta vilichomwa moto baada ya watu kuuliwa au kabla.

  (Sina nia ya kutetea polisi, lakini vyombo vya habari vimekuwa vikitupa habari za kutuchanganya)
   
 16. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #16
  Jan 14, 2011
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Hii ya magari yanaharibu barabara ndio naiskia leo, nijuavyo wanyama ndio huharibu barabara za vumbi.

  Lakini ku-empower watu wa chini na wa kati ni jukumu la halmashauri na hao wakulima kwene SACCOS zao, na pengine mbunge wao angeshirikia hapo ku-overview. Hamuezi kulima successfully kama hakuna means za kueleweka za masoko na usafirishaji..umaskini hautoondoka.

  Kuhusu wawekezaji ..well, pamoja na kusema sana lakini bado inafahamika vyema sasa kwamba kaulimbiu ya watawala bado ni ileile, 'mgeni njoo mwenyeji apigike'.
   
 17. m

  maggid Verified User

  #17
  Jan 14, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180

  Gaijin,

  Ahsante. Nimepokea taarifa za karibuni kabisa kutoka chanzo changu cha kuaminika. Aliyefariki ni mtu mmoja, kijana Justin. Bado sijapata jina la pili. Mwingine, Hassan, amejeruhiwa vibaya kwa kupigwa risasi ya kiuno. Yuko hai.

  Wananchi wenye hasira walichoma moto lori na kituo cha mafuta baada ya wenzao wawili kupigwa risasi. Nimehariri pia tafsiri yangu hapo juu.
   
 18. Maarifa

  Maarifa JF-Expert Member

  #18
  Jan 14, 2011
  Joined: Nov 23, 2006
  Messages: 2,881
  Likes Received: 1,051
  Trophy Points: 280
  MAGUFULI INGIA MBALALI TENGENEZA BARABARA. WAZIRI WA ARDHI/ KILIMO VIPI HAO WAKULIMA WADOGO KUNYANG'ANYWA ARDHI?

  Ila ikumbukwe kuwa bila mabadiliko hayaletwi kwa arenale na alinacha. Mpaka kidigo kakafara- damu hapo ndo watu wanafunguka macho. AMANI YA UKONDOO SASA KWISHA. Na tatafika pazuri. kama wengine ndo tutakuwa kafara basi tukutane mbinguni! Lakini walioko madarakani kutudanganya na amanni sasa waache. Ubabe wa polisi hausaidii, wataua lakini bado tutaibuka kama viwavi jeshi!
   
 19. N

  Ngonini JF-Expert Member

  #19
  Jan 14, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 2,024
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  same story, sasa hivi mabomu ya machozi yameisha ni kuua tu kwa kwenda mbele. Tusubiri Mungu atafanya kile ambacho ameamua kukifanya nchi hii baada ya dhuruma ya muda mrefu.
   
 20. e

  elimukwanza Senior Member

  #20
  Jan 14, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 167
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  baada ya kumaliza kazi yako maalum sasa umerudi katika sura ya uzalendo.Karibu maggid karibu,si wewe ni njaa.karibu sana
   
Loading...