Mbaraka mwishehe vs Michael Vicent nani zaidi?

Rufiji dam

JF-Expert Member
Feb 20, 2020
3,767
8,683
Onyo mada kwa wakubwa tu:
Baraka na Rehema za mungu ziwe nanyi.
Tanzania miaka ya nyuma iliweza kuvuma sana katika burudani ya muziki kupitia muziki wa dansi. Na kulikuwa na wanamuziki hasa na bendi nyingi. Ndani ya burudani ya muziki kuna vyombo mbalimbali ambayo ikirindima ndio muziki unatokea. Moja ya chombo hicho ama ala hiyo ni gitaa la solo ama leading gutair. Tanzania akatokea mwanamuziki mahiri sana kiasi cha kupewa jina la sololist International, ambaye alivuma sana mji kasoro bahari lakini asili yake ni Pwani ya Mzenga Chalinze, Mbaraka Mwishehe akivuma na Moro Jazz kisha umauti ukimfika akiwa na Super Volcano kifo hakikosi sababu na vijineno(nitakuja kuelezea siku za usoni mkasa wa kifo chake na utata wa mdogo wake Matata). Kuna vibao kibao akiwa moro Jazz mfano Jogoo la Shamba, CHakula cha masimango, Nisalimie Zaire na Mtaa wa Saba nk. Akienda Super Volcano akatimu vumbi hasa na Vibao kama mshenga, Sembuli, Mashemeji Wangapi, Baba Mdogo nk. Huyu mpaka leo anaitwa ni mcharaza gitaa la solo hatari kutokea. Achana na akina Mulenga, SHem Ibrahim Kalenga, Abdalah Tembo, Wema Abdalah, Saidi Mabera na nk. Dunia ya muziki wa Tanzania ama kwa kutojua ama kwa unazi wao wanamsahau mpiga Gitaa hatari sana nchini Tanzania ambaye kuna siku nilikuwa nimekaa na mgeni kutoka nje aliposikia gitaa la Michael Vicent alishangaa sana na kuuliza huyu ni Mtanzania kapiga gitaa hili? Nikamwambia naam mzungu, huyu ni mtanzania haswa aliyejaliwa vipaji lukuki katika viganja vyake wale mama zetu na baba zetu mliokuwa mnafanyakazi Urafiki hapana shaka huyu mwamba mnajua shughuli yake. Ndie aliyekuwa akibuni na kuchora mitindo mbalimbali ya khanga. Pata muda sikiliza vibao vya Wanachakachua Urafiki Jazz Band kama Asmah, Geza Ulole, Mwenyeki, Safari ya Uguja na Tanga, Rukia, Kwa Mjomba na vibao kibao. Kisha utapata jibu mwenyewe je Mbaraka anastahili kuitwa Sololist Internationale ama huyu Santana wa Tanzania Michael Vicent. Nikipata muda nitakuja kumuangalia mpigaji Saxphone bingwa kuwahi kutokea nchini Tanzania. Andiko hili sikutaja akina Nguza Marshall Vicking na Supreme Field Marshal Ndala Kashaba. Hawa Watanzania wageni. Karibuni. Wakubwa tu.
 
Mbona mnatuchanganya aisee hawa ni kina nani?
 
Kuhusu hilo la kubuni na kuchora mitindo ya khanga hapo kiwanda cha nguo Urafiki mbona huko nyuma iliwahi kuripotiwa kwamba aliyekiwa akifanya kazi hiyo alikuwa ni mzee Francis Kanyasu au kwa jina maarufu Ngosha ambaye pia tulishaambiwa kuwa ndiye aliyechora nembo ya taifa? Au ndiyo kutaka kuwanyang'anya hao marehemu wawili Mbaraka na Ngosha haki yao ili zote zihamie kwa huyo Vicent asiyejulikana na wengi? Hivi kweli kwenye solo ndiyo umlinganishe Mbaraka na huyo Vicent wa kuokoteza kutoka majalalani (asiye na umaarufu wowote)?
 
ukitaka umfaidi Mbaraka Mwinshehe Mwaruka sikiliza
Easter
Dokta Kleruu
Maonyesho Japan
Tina
Morogoro
fundi haswaaa tena haswaaaa
 
Similar Discussions

2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom