Nani zaidi kati ya Mbaraka Mwishehe, Hemed Maneti na Marijani Rajabu?

Jibaba Bonge

JF-Expert Member
May 6, 2008
1,246
401
Wana JF wale waliokuwepo enzi za wanamuziki hawa. Kama wangepambanishwa nani angekuwa zaidi? Najua kila mmoja alikuwa na kipaji chake tofauti na mwingine na uanamuziki wao ulikuwa tofauti pia lakini kama ingekuwa kuchagua mmoja tu kati ya hao, yupi alikuwa anakusuuza moyo wako? Kwanini?
 
Marijani Rajabu ni mkali ile mbaya. Hakuna wa kumkamata. Haijapata kutokea na sijui kama itakuja kutokea akapatikana mkali zaidi yake.
 
Mkuu JB, mimi natamba kuwa nilikuwepo wakati huo na nilingia muziki wa Mbaraka Mwinshehe mwaka 1972.
Huyu bwana ni Maestro, hana mwenzake.
Vocals zake zilikuwa nyororo na poetic na solo ndo usiseme.
Maudhui ya tungo zake zilikuwa zinagusa jamii nzima.
Mkuu umenikumbusha enzi ambazo sasa hazipo kabisa, tungo zilizo tamba
" Enyi vijana silikilizeni, acheni mpenzi wa mapenzi..."
"Twawapongeza waandishi wetu"
"Expo 70"
"Hiloo oh oh ulijidai wewe mbabe sana"
"Moro yapendeza"
Na vibao vingine vingi.
Hii haina maana kuwa Jabali la muziki na Maneti hawakuwa wazuri,wakati wa Mbaraka hawa walikuwa watoto wadogo kimuziki.
Hata hivyo waliliendeleza libeneke.
 
Mkuu unaikumbuka hii?:

Mzee Saidi eeh, alikuja lalamikaa eh
Kasikia fununu kwamba unavuruga nyumba za watu,
Kaja kutoa onyo anasema kijana ole wako,
Umefanya mambo mengi lakini haya yamezidi kipimo,
Mchezo na nyumba za watu, sawasawa kucheza na moto...
Acha acha mara moja hatari kubwaaaaa, hatari kubwaaaaa......

Au

Ilikuwa asubuhiii na mapema, jua linachomoza eh, Ndipo nilipatwa na msituko usioosemekana maama........ Nilipata habari kumetokea ajali ya kutisha saana.......... kwenye daraja la Salenda magari mawili yamegongana maaama................

Zuweena ningempata wapi, Zuweena mwingine sawa na yeye,
Mtoto aliyeumbika mwenye tabia za kupendeza, Zuweena Zuweena kweli nampeenda.

Ahhh! Mwacheni Marijani Rajabu awe Marijani Rajabu. Hana mfanowe.
 
Marijani .
Sio tu kwamba ni jabali wa muziki ila pia ni nguli haswa wa medani ya muziki wa dansi.
Ndio maaana hata chama cha muziki wa dansi tanzania (chamudata) kilimtangaza kuwa ndio mwanamuziki wa milenium iliyopita.)
 
Mkuu JB, mimi natamba kuwa nilikuwepo wakati huo na nilingia muziki wa Mbaraka Mwinshehe mwaka 1972.
Huyu bwana ni Maestro, hana mwenzake.
Vocals zake zilikuwa nyororo na poetic na solo ndo usiseme.
Maudhui ya tungo zake zilikuwa zinagusa jamii nzima.
Mkuu umenikumbusha enzi ambazo sasa hazipo kabisa, tungo zilizo tamba
" Enyi vijana silikilizeni, acheni mpenzi wa mapenzi..."
"Twawapongeza waandishi wetu"
"Expo 70"
"Hiloo oh oh ulijidai wewe mbabe sana"
"Moro yapendeza"
Na vibao vingine vingi.
Hii haina maana kuwa Jabali la muziki na Maneti hawakuwa wazuri,wakati wa Mbaraka hawa walikuwa watoto wadogo kimuziki.Hata hivyo waliliendeleza libeneke.
Mkuu, nakubaliana nawe katika hilo. Hapa wangewekwa Maneti na Marijani. Hawa wanaweza kuwekwa pamoja kwenye mizani. Lakini Mbaraka saizi yake ni akina Kilaza, Michael Enock, Wema Abdallah na wengine wa enzi hizo. Na kwa hao wooooooooote, hamna wa kumpiku Mbaraka.
 
Nawapenda wote... so kwangu droo.... kisingizio kila mmoja alikuwa na muda wake... Mwaruka ananiliza muda mwingine, maneti balaa.... Marijan nae sio mchezo
 
Mkuu JB, mimi natamba kuwa nilikuwepo wakati huo na nilingia muziki wa Mbaraka Mwinshehe mwaka 1972.
Huyu bwana ni Maestro, hana mwenzake.
Vocals zake zilikuwa nyororo na poetic na solo ndo usiseme.
Maudhui ya tungo zake zilikuwa zinagusa jamii nzima.
Mkuu umenikumbusha enzi ambazo sasa hazipo kabisa, tungo zilizo tamba
" Enyi vijana silikilizeni, acheni mpenzi wa mapenzi..."
"Twawapongeza waandishi wetu"
"Expo 70"
"Hiloo oh oh ulijidai wewe mbabe sana"
"Moro yapendeza"
Na vibao vingine vingi.
Hii haina maana kuwa Jabali la muziki na Maneti hawakuwa wazuri,wakati wa Mbaraka hawa walikuwa watoto wadogo kimuziki.
Hata hivyo waliliendeleza libeneke.

Mkuu nadhani hii line inaimbika hivi
" Enyi vijana silikilizeni, acheni mchezo wa mapenzi..."
 
Waacheni wapumzike kwa amani huko waliko, Kila mmoja alikuwa na utemi wake, Marijani alikuja wakati Mbaraka ni mtemi; yeye mwenyewe akaja kuwa mtemi wakati Mbaraka ana matatizo ya vyombo.
 
Hii ni sawa na kuwalinganisha wakali wa soka wa enzi hizo kina Eduardo Gonçalves de Andrade (Tostão), Edison Arantes do Nascimento (Pelé), George Best... na wengineo (wa Miaka ya 1900's) na wachezaji wa miaka ya hii ya 2000's.

Huwezi kuwalinganisha, maana kila kizazi kilikuwa na mastaa wake.

Kwa ufupi nyimbo zao zilikuwa na maudhui maridhawa na zikigusa jamii, tofauti na hizi nyimbo za sasa, (msanii mmoja aliwahi kuziita Big G, chew gum), maana hazikawii kupoteza radha.
 
kama ningekuwa nawapanga kimpangilio ningepanga hivi;
1-Mbaraka Mwishehe
2-Marijani Rajabu
3-Hemed Maneti
 
Konaball nawakubali hao wawili wa mwanzo ila Maneti mmh sijui, Marijani alikuwa ana powerful voice sikiliza ukewenza, DAH ZUWENA miaka hiyo ya 79-84 nilikuwa Sumbawanga kuna Mwanameka. ila wadau mimi hawa wana SIKINDE NGOMA YA UKAE ya wakati ule ilikuwa inatisha si mchezo, Kuna Huyu jamaa anaitwa Hassan Rehani Bitchuka(wakati ule) sauti yake kwa kweli haikuwa na mpinzani ilikuwa inapanda mpaka mwisho(Highet pitch) sasa hivi kwishnei, nna kanda yao yaani kila ikifika ijumaa naiweka kusikiliza ule wa wimbo wa wikiendi, tufurahi na wana sikinde tucheze leo ngoma ya ukae, ukitaka kufurahi, kila jumamosi njoo uburudike na wana sikinde oyee halafu wanataja majina ya kundi zima enzi hizo akina KING ENOCK, Mwanyiro, Gama, dah mpaka mwili unasisimka. Hapo msondo enzi hizo ilikuwa haioni ndani kwa sikinde, kuna vibao kama Duniani kuna mambo, Selina-WADAU kweli vipaji vilikwepo sasa hivi eti wanamziki wa Ubongo wa Fleva akauambia nilipata idea hiyo hapo hapo nikaanza kuandika verse nikaenda studio nikamkuta DUNGA tukapanga vyombo baada ya nusu saa track imekamilika kweli JAMANI? NDO MAANA INAITWA Bongo Flavour sababu ni ka fleva fulani hivi ka muda wa wiki kadhaa baada ya hapo kwishnei
 
Marijani Rajabu ni mkali ile mbaya. Hakuna wa kumkamata. Haijapata kutokea na sijui kama itakuja kutokea akapatikana mkali zaidi yake.

yani umenisoma % 100. Tatizo hata picha zao hatuzijui achilia mbali nyimbo zao. Niliwahi kuona picha ya marijani akiwa junk. Presley na marijani ni droo ila watz walishindwa kumtangaza
 
Marijani tungo kali na sauti nzuri vinamfanya awe na ladha ya kipekee. Mbaraka alikuwa ni muhuni, nyimbo zake za shemeji shemeji huku mwazima taa na mtaa wa saba zimedhihirisha
 
wote walikuwa wakali na walikuwa na vitu tofautitofauti
marijani alikuwa anatumia nahau, misemo na vijineno sana kwenye nyimbo zake,
Mbaraka alikuwa straight foward
 
Back
Top Bottom