Mbali ya kuwa ni jina la Chama Cha Kisiasa hapa nchini, neno "CHADEMA" pia ni surname (ubini) ya watanzania wa kabila (ukanda) lipi hapa kwetu???????

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,317
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums. Mimi mdogo wenu Infantry Soldier nipo mzima kabisa wa afya. Thanks to God the Almighty. Eti ndugu zangu watanzania;

Mbali ya kuwa ni jina la Chama Cha Kisiasa hapa nchini, neno "CHADEMA" ni surname (ubini) ya watanzania wa kabila (ukanda) lipi hapa kwetu?

Nimeamua kuuliza hivi kwa maana kwamba nilipokuwa ninaangalia matokeo ya wanafunzi katika website ya NECTA ndio nikakutana na baadhi ya watanzania wenye majina yanayoshabihiana na vyama vya kisiasa. Tazama screenshots chache hapo chini; Kuna majina yamefanyiwa highlighting kwa rangi ya orange.

(1) ZUBERI MHINA CHADEMA
(2) ASHURA CHADEMA MUSSA
(3) LAMECK CHADEMA KIMELA
(4) MROCKI CHADEMA MVUNGI
(5) JAMES CHARLES CHADEMA
(6) JUMA HAMISI CHADEMA

IMG_20200503_174330_588.jpg


IMG_20200503_174240_746.jpg


IMG_20200503_174203_203.jpg

Pia fungua link ya Google Search Engine hapo chini kwa ushahidi zaidi

https://www.google.com/search?ei=fdSuXoSyBYK7lwSww6i4CQ&q=chadema+site:necta.go.tz&oq=chadema+site:necta.go.tz&gs_lcp=ChNtb2JpbGUtZ3dzLXdpei1zZXJwEAxQAFgAYNfyM2gAcAB4AIABAIgBAJIBAJgBAA&sclient=mobile-gws-wiz-serp

ANGALIZO: Ninaomba uzi huu usigeuke ukawa ni uwanja wa mabishano ya kisiasa baina ya wafuasi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) pamoja na Chama Cha Mapinduzi (CCM) na vyama vingine vya kisiasa. Nisaidieni kujua hili ni jina la kabila gani.

OUR MOTTO: KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA MIMI PAMOJA NA WEWE. SOTE TUTIMIZE WAJIBU WETU IPASAVYO.
 
Back
Top Bottom