Nelson nely
JF-Expert Member
- Jan 25, 2014
- 4,256
- 2,862
Mbalamwezi ikiwa kwenye umbo lake kamili huwa kuna vivuli fulani vinaonekana pale,hivi vivuli vinazungumziwa kwa namna mbalimbali kulingana na mawazo na mazingira tofauti,mfano:
Dodoma
Nikiwa mdogo kijijini kwetu kongwa huko,niliambiwa vile vivuli ni mwanaume na mkewe wakikata kuni porini!
Kigoma
Wanadai yule ni mvuvi akihangaika kuvuta nyavu iliyosheheni samaki(migebuka)toka ziwani
Iringa
Wanadai ni baba akiwapa usia wanawe!
Wanasayansi
Wanadai mwezi umetawaliwa na maji kwa sehemu kubwa na vile vivuli ni eneo la nchi kavu...
Lakini....
Vile vivuli ni taswira ya Baba yetu Abraham akijiandaa kumchinja mwanae mpendwa Isaka.
Over.