Mbagala Rangi Tatu, Uchafu umezidi mno

manka1

Member
Nov 4, 2014
11
23
Wadau naleta kwenu changamoto ninayoiona Mbagala Rangitatu. Pale kuna biashara nyingi tena za vyakula lakini uchafu ni mwingi sana sijui hata kama tuna maafisa wa afya eneo hilo marundo ya taka, mitaro imejaa maji machafu. Ombi langu ni wahusika wafanyie kazi kero hii maisha ya watu yako hatarini.
 
Umetumwa na mabeberu wewe! Tutakufungulia kesi ya uhujumu uchumi..ohhh...
 
Dah afadhali umeleta uzi..nilikua naona uvivu kuleta ila ukweli tangu Mzalendo namba moja aseme wafanyie biashara barabarani uchafu umekua mara dufu yaani mbagala ni chafu kupitiliza sitashangaa kama kikilipuka kipindupindu.
 
nafikiri ungeambatanisha na picha thread yako ingekuwa na mashiko zaidi, lakini unastahili pongezi kwa kuibua changamoto hii ya uchafu kwenye majiji yetu hakika ni tatizo ambalo limekosa utatuzi.
 
Dah afadhali umeleta uzi..nilikua naona uvivu kuleta ila ukweli tangu Mzalendo namba moja aseme wafanyie biashara barabarani uchafu umekua mara dufu yaani mbagala ni chafu kupitiliza sitashangaa kama kikilipuka kipindupindu.
Huyu nani alitokea huko, huyu wa muziki asadie
 
Changamoto ya mbagala ni uchafu tuu, lakini ni moja ya sehemu ambayo maisha ni rahisi sana,
Vitu bei yake iko chini sana
 
Ni kweli kabisa, watu wanatafuna supu ya magozi ya ng'ombe hata habari hawana na ofisi ya kata ya charambe ipo karibu na wanapita hapo hapo wanaona.
 
Rais JPM, alipotamka wafanyabiashara ndogondogo waachwe wafanye biashara pale wanapoona panafaa kwa biashara zao!!!

Viongozi wa maeneo husika akili zikaganda hawajui kipi wawafanyie wafanyabiashara hawa!! Sasa wamebaki hovyo hovyo.

Hawana usimamizi wowote, kama wanawaogopa kwa sababu ya tamko la Rais ! Basi wawaombe wao wenyewe wachaguane na kupeana majukumu ya usafi na usajili wa mjasiriamali mpya anayejitokeza wampe masharti ikiwemo USAFI.
 
Upo sahihi mkuu, ukianzi roundabout ya Charambe kuja terminal mtaro umetapika kabisa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom