Mbagala ni sehemu ya hovyo, unajengaje nyumba ya kifahari Mbagala?

Ukitaka kununua kiwanja kwenye mji wowote ule, usinunue Kusini au Magharibi. Hayo ya Mbagala utayaepuka vizuri tu.
Sio kweli hata kidogo.. Tembea ujione miji ilivyotofauti. Ukute TZ nzima umefika mikoa miwili tu PWANI NA DSM
 
Kwa mfanyabiashara uswahilini ndo kwenye pesa Kama biashara zako zipo uswahilini na zinakuuingizia pesa ndefu kwann usijenge karibu na biashara zako.
Maliza chuo ajira hakuna utaelewa au jiajiri kuikosoa serikali then ufike bei kwa kuunga juhudi upate pesa ufanye shughuli zako
deep sana hii....wazazi wapo ubungi mi nilipanga mbagala kuu sasa nmejenga mwandege...changamoto kubwa madogo wengi wanaishi maisha ya kusadikika akishamponda Rais akawasha twitter na kulike stori za kigogo anaona kamaliza kabisa na maisha kayaotea....anashindwa sahau mbagala ilikua inaonekana hivyo kwa ajili ya barabara kuminywa so ila kwa sasa mwendokasi unakuja,barabara inapanuliwa na kama unataka wahi posta sidhani ka kuna njia rahisi zaid ya kilwa road...sema kwa umri huu hata mda wa kubishana na huyu lofa siuoni maana majukumu yananiangalia
 
Yeah ni kweli kabisa Mbagala ni pabovu mno,nadhani hakuna kiongozi wa serikali anaekaa kule ni kama mji uliotengwa...ila Kisemvule ndio kunachipuka kuzuri kiasi kuzidi Mbagala
 
deep sana hii....wazazi wapo ubungi mi nilipanga mbagala kuu sasa nmejenga mwandege...changamoto kubwa madogo wengi wanaishi maisha ya kusadikika akishamponda Rais akawasha twitter na kulike stori za kigogo anaona kamaliza kabisa na maisha kayaotea....anashindwa sahau mbagala ilikua inaonekana hivyo kwa ajili ya barabara kuminywa so ila kwa sasa mwendokasi unakuja,barabara inapanuliwa na kama unataka wahi posta sidhani ka kuna njia rahisi zaid ya kilwa road...sema kwa umri huu hata mda wa kubishana na huyu lofa siuoni maana majukumu yananiangalia
Ulipata MKE huko Mbagala?

sisi watoto wa uswazi mbagala ndio home...vigodolo minanda,,micbiriku ndio imetukuza mzeee..uko ushuwani hatukuwezi mzeee....
 
Sijui kwanini napachukulia Mbagala kama sehemu ya hovyo namna hii.

Kule ni pahovyo sana uswahili ni mwingi sana.

Nyumba zinajengwa jengwa hovyo tu bila mpangilio Mbagala ni Tandale ijayo maana nyumba zinajengwa kiajabu ajabu sana.

Mitaa yenye mambo ya ajabu ni mbagala yaani nikachezee pesa nikajenge mbagala nitakua mzima?

Mtu na peza zake anaacha kujenga mjengo mkali huko bunju mbezi kinyerezi au angalau basi Chanika eti anaenda kujenga Mbagala, Vikindu, Kisemvule sijui wapi huko tena.

Acheni kuchezea pesa sijui napachukuliaje Mbagala yaani ni sehemu ya ajabu mno.

Mfano mrahisi tu tuchukue eneo la Kimara tu jaribu kuiwaza Kimara huku ukiilinganisha na mbagala kisha kuna picha utaipata kichwani

Utagundua kabisa kwamba kimara ni mara 1000 ya mbagala huwezi kuta kimara watu wanacheza vigoma vya ajabu ajabu huwezi kuta Kimara watu wakila utumbo na miguu ya kuku huwezi kukuta Kimara watu wakigombea daladala na kupitia dirishani lakini Mbagala yapo hayo

Tahadhari: Nyumba za chini ya kiwango a.K.a lipua nihamie zinapatikana maeneo ya Mbagala, pakifuatiwa na Vikindu Temeke na kisha Gongo la Mboto Ulongoni haya maeneo nyumba zao nyingi ni za chini ya kiwango mfuko mmoja wa cement unafyatua matofali 100 ujenzi mbovu nyumba zinajengwajengwa tu hovyo vichochoro ndo vingi mwisho Nyumba zinasongamana tu hata gari haiwezi kupita
Kwa maelezo haya umewahi kuishi mbagala
Unganisha na vingunguti manina hakufaii mvua ikinyesha aibu
 
Tena mbagala nipazuli sana..kuna maeneo yana mazingira Safi na salama kuishi,pia maisha ya mbagala ni cheap sana kuliko hata huko kunduchi ,goba na huko sijui mbezi N.K
Huku sukari kwa ndawale au makonde shop, wanapima kwa vijiko 200..
Raha ya uswazi ni mzunguko wa pesa
 
Mbagala siyo kabisa, ila mi Naona kisemvule kuzuri Sana, hewa, ardhi,miti ya kutosha
 
Sijui kwanini napachukulia Mbagala kama sehemu ya hovyo namna hii.

Kule ni pahovyo sana uswahili ni mwingi sana.

Nyumba zinajengwa jengwa hovyo tu bila mpangilio Mbagala ni Tandale ijayo maana nyumba zinajengwa kiajabu ajabu sana.

Mitaa yenye mambo ya ajabu ni mbagala yaani nikachezee pesa nikajenge mbagala nitakua mzima?

Mtu na peza zake anaacha kujenga mjengo mkali huko bunju mbezi kinyerezi au angalau basi Chanika eti anaenda kujenga Mbagala, Vikindu, Kisemvule sijui wapi huko tena.

Acheni kuchezea pesa sijui napachukuliaje Mbagala yaani ni sehemu ya ajabu mno.

Mfano mrahisi tu tuchukue eneo la Kimara tu jaribu kuiwaza Kimara huku ukiilinganisha na mbagala kisha kuna picha utaipata kichwani

Utagundua kabisa kwamba kimara ni mara 1000 ya mbagala huwezi kuta kimara watu wanacheza vigoma vya ajabu ajabu huwezi kuta Kimara watu wakila utumbo na miguu ya kuku huwezi kukuta Kimara watu wakigombea daladala na kupitia dirishani lakini Mbagala yapo hayo

Tahadhari: Nyumba za chini ya kiwango a.K.a lipua nihamie zinapatikana maeneo ya Mbagala, pakifuatiwa na Vikindu Temeke na kisha Gongo la Mboto Ulongoni haya maeneo nyumba zao nyingi ni za chini ya kiwango mfuko mmoja wa cement unafyatua matofali 100 ujenzi mbovu nyumba zinajengwajengwa tu hovyo vichochoro ndo vingi mwisho Nyumba zinasongamana tu hata gari haiwezi kupita
Na shauri upande yake mabasi ya Mbagala utoe haya maneno halafu utulete mrejesho.
 
Hahaha! Sasa unalalamika nini wewe?
Hivi katika sehemu zote za Dar es Salaam kwanini umeichagua Mbagala na kuieleza hivyo utakavyo? Watu hawajengi Mbagala....labda kufanya ukarabati. Viwanja hakuna Mbagala. Shida yenu Chamazi, Mbande nyie kote mnakuita Mbagala. Anyway, Unazijua sehemu zifuatazo:-
1. Kawe
2. Mikocheni Kisiwani
3. Msasani maeneo ya Maandazi Road
4. Kinondoni Moscow
5. Mwananyamala A&B, kwa Kopa, Kisiwani, Kwa Manjunju, Ujiji na Mwinjuma
6. Tandale...kwa Tumbo, Sokoni, Kwa Mtogole
7. Manzese....tip top, kilimani, sweet corner, argentina
8. Mburahati
9. Mabibo
10. Kigogo
11. Buguruni
12. Vingunguti
13. Tabata...matumbi, kimanga, dampo, makuburi
14. Tandika
15. Mtoni kwa azizi ali, mtongani
16. Yombo... dovya, kwa limboa, kilakala, kwa chande, BAKWATA
17. Gongo la Mboto
18. Kiwalani
19. Aiport....maeneo yote mpaka kukaribia chuo cha VETA
20. Keko....toroli, magurumbasi, mwanga
21. Kurasini
22. Kigamboni....ferry, Tungi, Vijibweni
23. Tegeta kwa Ndevu
24. Temeke Mikoroshini na Sandali
25. Ununio sikumbuki jina la mtaa exactly lakini kuna sehemu fulani kuna wenyeji sana.
Hivi sehemu hizo zote hapo juu unazifahamu vizuri?

Zina tofauti gani na Mbagala kwa hali za maisha ya watu na makazi yao?
Kwanini umeichagua Mbagala? Kwanini usiseme Kinondoni Mkwajuni au sehemu nyingine?

Hayo meneo yote hapo juu niliyoyataja ni sehemu ambazo zina makazi ya miaka mingi. Ni sehemu kongwe zenye nyumba nyingi za urithi. Waliozijenga wameshatangulia mbele za haki. Ni sehemu walizokaa masikini wazawa hasa Wazaramo wa mkoa huu wa Dar.

Sehemu unazotaka kuzifananisha nazo kama Kimara ni sehemu za makazi mapya, miaka 20 iliyopita Kimara kulikua mashamba matupu yenye miembe tu. Huko Kinyerezi ndio hata dalili kama kuna watu watakwenda kuishi haikuwepo. Lazima maeneo hayo yawe na nyumba za Kisasa na zenye mpangilio. Mbagala kuna nyumba za miaka ya 80, something you can't find Bunju au Kinyerezi.

Hata Kijichi, Mgeninani, Toangoma ni makazi mapya, makazi yake ni tofauti sana na maeneo mengi ya jirani yake kama Mbagala Kuu na Kongowe.

Huko Kisemvule, Vikindu ni mkoa wa Pwani. Nako kuna nyumba nyingi mpya na kuko vizuri tu. Kinachokusumbua ni kwamba ili ufike huko ni lazima upite Mbagala. Shida ni nini? Hiyo si njia tu.

Tafuta sehemu nyingine ya kuilinganisha na Mbagala sio Kimara, Mbezi, Bunju, Kinyerezi sababu ziko katika era tofauti.

Waache watu na maisha yao.
Dah Jomba umenikumbusha maeneo mpaka mwili umesisimka...Now naishi Kimara..but those places ulizozitaja ndio zimelea au kukulia watoto wengi wa MJINI HAPA DAR..Achana na watu kutoka mkoa..namaanisha wapiganaji,makontawa,maninja wa JIJI LA DAR..

Kama umezaliwa DAR na hujawai kukaa hizo sehemu asee MAISHA YA DAR huyajui na hutopata raha zake..labda uwe umetoka mkoa kuja kutuuzia tangawizi,vitenge,maparachichi,asali n.k
 
Watoto maboya sana hawa. Hawa wamekuja juzi mjini, na kilichowaleta ni chuo kikuu cha Dar es Salaam. Baadae wakapata ajira hapa wamekopa benki wakajenga Kimara huko huko basi wanaidiss Dar na mitaa yetu iliyotukuza.

1998, ubalozi wa Marekani unalipuka mi niko Mwananyamala mitaa ya Kambangwa pale kile kishindo mpaka leo nakikumbuka. Mtu kama hujakaa mitaa hiyo, hujaishi huko, huijui Dar na hutaijua....

Peace.
 
Back
Top Bottom