mbagala, madiwani wanachekesha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

mbagala, madiwani wanachekesha

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Lukwangule, Feb 17, 2010.

 1. L

  Lukwangule Senior Member

  #1
  Feb 17, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 150
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi nadhani waheshimiwa Madiwani Temeke warekebishe mambo yao kwani ile barabara iliyojengwa sub standard ahh hapana ile barabara iliyojengwa kwa kodi za Wajep kuanzia Bendera Tatu hadi Rangi Tatu inaonekana haiwezi kukamilika mpaka mlungula uwe umeliwa kwelikweli.kama si kweli kumbe nini tatizo?:mad:
  Tunaambiwa ili imalizike lazima kuwapo na kituo, na kituo hicho kipo katika misele ya ajabu kabisa hali inayotafsiriwa na akina yahe kweli kuna shida ya mlungula na mtu kupata fedha za kuendea katika uchaguzi.
  kwa wale wakazi wa Mbagala hawatasita kabisa kuzungumzia ukubwa wa eneo hilo la Mbagala na haja ya kujengwa kwa terminal kubwa kuliko Terminal zote za dar es salaam.
  Hii inatokana na si tu uwingi wa watu bali Mbagala inakuwa kama sehemu ya kwanza ya kuingilia mjini kutoka maeneo kama ya Kongowe, Mkuranga, Chamazi, na kwingineko.
  sasa madiwani wanataka gari ziingie eneo hilo na kufikia katika soko ambapo kiusalama na kuingia katika barabara kuu kuna hitaji ubishi zaidi kuliko natural flow.
  kama unataka natural flow ni lazima kituo ukiweke mkabala na St Mary International school. lakini madiwani kwa kuelewa kuwa pale ndio hasa wanastahili kuweka kituo sasa wameshaanza kuuza eneo hili kwa wengine, kila mtu anashika kasi ya kujenga eneo hilo ambalo lingewezwa tu kugezwa eneo la kuegesha magari kirahisi.
  Unaingia kutoka barabara kuu,na unatokea barabara ya maji matitu unaingia barabara kuu pale Rangi tatu, lakini hili wazo la kuingia kiburugwa kuingia sokoni italeta shida kutoka kwani gari za barabara kuu zitaingia na zitalazimika kutoka pamoja na zile zinazotoka kama nimeeleweka.
  pamoja na kutengeneza kituo hicho muhimu pia ipo haja ya kuweka mzunguko katika eneo linalotoa bara kutoka Kiburugwa na Mbagala kuu na basi angalau wafukiwe mashimo pale ilipoishia barabara ya Wajep.
  Sasa unaweza kujiuliza nini hasa kinatokea katika Mbagala hii ambayo ukuaji wake si wa kawaida?hakuna nidhamu kabisa ya kugeuza magari pale na foleni inaanzia palepale.
  Kuna mtu kweli anaweza kusema? Nina mashaka mhandisi hajui na bwanausi (huyu meya)ambaye anaishi Kongowe wala hajali kinachotokea pale rangi tatu ndio maana wazee wa kazi mara nyingi wanachukua fedha pale kwani miondoko ya magari na usalama si sawasawa.
  Lukwangule
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...