Mbagala, Dar: Polisi yawanyakua watu 27 Walioiba Saruji kwenye ajali

KUKAMATWA WATU 27 KWA TUHUMA ZA KUIBA MIFUKO YA SARUJI BAADA YA AJALI YA MALORI MBAGALA

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam linawashikilia watu 27 kwa tuhuma za kuiba mifuko ya saruji baada ya ajali ya malori mawili eneo la Mbagala Mission.

Mnamo tarehe 04/10/2021 saa 04:30 asubuhi eneo la Mbagala Mission, Lori lenye namba za usajili T 164 DKC aina ya Horse na tela lake namba za usajili T 342 DJZ likiwa limebeba mifuko ya saruji lilipata ajali na kutumbukia kwenye mtaro kutokana na tairi kupasuka.
Baada ya ajali hiyo kutokea zaidi ya watu 50 walijitokeza na kuiba mifuko ya saruji.

Aidha, tarehe 05/10/2021 majira ya saa 06:40 usiku eneo la Mbagala Mission, Lori lingine lenye namba za usajili T 705 AUE lililokuwa na tela lenye namba za usajili T 911 ATR likiendeshwa na MUHIDINI HUSSEIN (39),mkazi wa Morogoro, likitokea Mbagala kuelekea mjini likiwa limebeba zaidi ya mifuko 700 ya saruji nalo lilipata ajali.

Polisi walifika mapema eneo la tukio na kuwakuta watu 27, wakiwa wanaiba saruji kwa kuipakia kwenye Pikipiki na Bajaji. wote walikamatwa na jumla ya mifuko 368 iliokolewa ikiwemo 10 iliyokutwa kwenye nyumba za watu.

Watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani haraka iwezekanavyo.

Onyo;-
Jeshi la Polisi halitasita kushughulika kikamilifu kwa mujibu wa sheria na watu wote wenye tabia ya kukimbilia kwenye matukio ya ajali badala ya kuokoa watu na mali, wao wanageuka kuwa wahalifu/wezi.

MULIRO J. MULIRO
KAMANDA WA POLISI
KANDA MAALUM DAR ES SALAAM

Pia soma;

Thread 'Mbagala: Lori lililobeba saruji laanguka, Wananchi wajibebea mifuko ya saruji' Mbagala: Lori lililobeba saruji laanguka, Wananchi wajibebea mifuko ya saruji
Job well done Police force
 
Hivyo vijiji vya watu wa magendo dili
Wazee wa kufaulisha,wewe huwesi kuvijua
Sukari huko kg1 inauzwa 1000 tu
Ukitaka taili za gari,betri godoro mpya etc unapata
Narudia wakazi wote huko ni wezi

Ova

Hajui kitu huyo mwache aendelee kulala

Hajui Kuna watu wanaserikali yao kwa km Kadhaa za barabara wengine ikiangukia kulia hyo yetu ikiangukia kushoto yenu.

Hajui kuna sehemu watu wanamwaga mafuta ya kula kwenye lami ili Lori likanyage huko mbele yasafari kwenye Kona au mteremko akiingia Kati anakuta hola?
 
Ndomana namuambia aumize kichwa
Wenzake ss tunapuyanga tunaona na kukutana
Na mengi,hatuhadisiwagi
Yah mafuta pale maseyu wajanja tukipitaga tunapitaga na speed 10 mdg mdg wezi wenyewe wanajua ma master wamepita hapa wanapajua,wale wazee wa speed wanaipataga

Ova
 
Hata hivyo polisi walizembea Sana tena Sana. Yaani watu mpaka wanaiba wao walikuepo wapi
Halafu ni asubuhi ndo utajua jinsi gani vyombo vyetu baadhi ya maeneo walivyowezembe ni hatari sana. No frequent road patrol
 
Ndomana namuambia aumize kichwa
Wenzake ss tunapuyanga tunaona na kukutana
Na mengi,hatuhadisiwagi
Yah mafuta pale maseyu wajanja tukipitaga tunapitaga na speed 10 mdg mdg wezi wenyewe wanajua ma master wamepita hapa wanapajua,wale wazee wa speed wanaipataga

Ova

Hao ndo wale akiingia kwenye Basi anataka akae na demu au wale wanaovaa earphone na kulala safari nzima haya Mambo hawawezi kuyajua.

Kuna muda unaamua kupanda Lori ili ujue maisha yakule yapoje na her kwa changamoto unazoziona wapi nawe unaeza pata fursa ya kupata chochote kupitia changamoto hzo.

Nawaoneaga huruma wale wanaochaguaga basi la kupanda eti nataka 2by2 nauli 57k wakati Kuna chuma za 15k kwanza njia zima unapata stori za kila Kijiji ukimaliza safari unakusanya na kuchambua muhimu kwako zen unaingia field kukomaa.
 
Kweli kabisa

Hii dunia ni uwanja vita

Mabarabarani kuna visa hatari

Ova
 
Back
Top Bottom