Mbagala, Dar es Salaam: Mahabusu wadaiwa kumpiga askari na kutokomea kusikojulikana

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,813
4,545
Mahabusu waliokuwa wanashikiliwa kwenye Kituo cha Polisi cha Maturubai, kilichopo Mbagala wilayani Temeke wametoroka baada ya kumpiga askari kisha kuvunja lango la chumba cha mahabusu na kutokomea kusikojulikana.

Tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa moja usiku, jijini Dar es Salaam limethibitishwa na Jeshi la Polisi huku likisema wanaendelea na msako wa kuwabaini walipo mahabusu hao.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Murilo alipotafutwa na Mwananchi azungumzie tukio hilo, alisema yuko msibani Kibondo, atafutwe kaimu wake, Daniel Shila ambaye ni Mkuu wa Upelelezi wa Polisi Kanda ya Maalum Dar es Salaam azungumzie hilo.

Kamanda Shila alipotafutwa na Mwananchi alikiri kuwapo kwa tukio hilo, lakini akasema “waliotoroka ni mahabusu wenye makosa madogo waliokamatwa kwenye doria iliyofanywa na jeshi hilo, si wale wenye kesi mbalimbali.”

MWANANCHI
 
Kimeunana
FB_IMG_1623256598340.jpg
 
Kituo cha polisi Maturubai ni miongoni mwa vituo vinavyosifika kwa kutesa watuhumiwa. Ukisikia mateso wanayopata watuhumiwa wakiwa kituoni hapo utajiuliza hivi inakuaje baadhi ya watu wakapewa kazi ya uaskari

Kuna askari anaitwa Trump( kama bado yupo hapo kituoni) ni mtesaji na katili sana hasa kwa vijana wadogo wanaokamatwa kwa tuhuma za makosa mbalimbali

Kupigwa mpaka kuvunjwa viungo vya mwili, kurundikwa watu wengi sana kwenye selo ndogo na kubambikiwa kesi ni miongoni mwa mateso wanayokutana nayo mahabusu wa kituo cha Maturubai

Vyombo vya sheria na usimamiaji haki vifanye uchunguzi kuhusu jambo hili ili vibaini uvunjwaji mkubwa wa haki za binadamu kwa watuhumiwa
 
Hao askari wa aina hiyo huwa wanajisikiaje ndani ya nafsi zao!
 
Back
Top Bottom