Lububi
JF-Expert Member
- May 3, 2013
- 2,123
- 3,736
binafsi huwa sipendi kusalimiwa au kusalimia SHIKAMOO. sababu kubwa ni historia ya neno lenyewe kuwa la enzi za utumwa "NIKO CHINI YA MIGUU YAKO" lakin ningependa kumsalimia kwa adabu anayestahili. sasa wataalam wa lugha na maadili mnisaidie mbadala wa matumizi ya neno hilo na maana na adabu ibaki palepale. nilipokuwa Pemba nilifurahia matumizi ya asalaam aleikhum kwa rika zote. lakin kwa huku mikoani ni salaam yenye tafsiri ya dini ya uislam. huwez kuitumia pote ukaeleweka.