Mbadala wa JK

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
22,603
29,744
mjadala umeshakuwa wa wazi sasa ambapo mwanzo tulikuwa tunanong'ona. Je unadhani kuna mwanaccm ambaye ni kuntu kupokea kijiti kutoka kwa muungwana???

lete jina na wasifu tuchambue hapa. (angalizo: hakuna aliye msafi kwa 100%)
 
achane ulongo, ukitaka kuandika hapa weka habari iliyotafitiwa - no research no right to speak
 
Kwa nini tusimpate Zuma wa bongo?? yaani ngangari wa misimamo asiyeogopa kichuguu wala mlima ambaye anaweza kupita milango hata yenye zengwe kali lakini nia iwe moja tu kurejesha heshima ya nchi.

kwa hapa nchini naona wassira anafaa sana, kama mkimkataa basi namleta kwenu mzee wetu mahita.
 
naona leo jua limechomozea magharibi.

unadhani wabongo watampigia kura mmasai huyu tena??? why not Samweli Sitta?? maana ameonesha mwelekeo wa msimamo thabiti dhidi ya tabia legevu ya serikali ktk maamuzi mazito.
 
ada ya mja hunena muungwana vitendo
semeni wazi kuwa hamumpendi jk
mbona wakati wa bm hamkuthubutu kusema????
Mzee rukhsa alilizika azimio la arusha mbona hamsemi
chakufahamu hapa ni hata kama sisi wana jf wote hatumtaki pamoja na wasomao magazeti lakini mjue kuna mamilioni ambao wako nyuma yao jee hao wote ni wajinga??????

Hivi ni raisi gani amewahi kuthubutu kuwapeleka mahakamani idadi kubwa ya viongozi tangu tupate uhuru???? Au mlitaka awahukumu kwa kuwaweka kizuizini kama zile enzi???????
 
si haba umetoa maoni yako mkuu.
ila kuwapeleka viongozi wengi mahakamani huku njia inayowatoa hatiani unaiona since day one ya kusikilizwa kesi huo si ufanisi. matumizi makubwa ya serikali yasiyo na udhibiti ni dalili ya kuelemewa. na kwa kuwa waliomzunguka wamemzidi ujanja na hataki kusikia sauti zetu (umma) basi huko ni kukwama. Unaposema mamilioni wapo nyuma yake sikatai hilo kwani heshima yetu ya uoga ya watanzania ndiyo iliyotufikisha hapa.

tunataka action zaidi na si kuwapeleka mahakamani pekee. kwani kuzuia akaunti zao wakisubiri hukumu kusomwa ni adili sana kwani hao walioko mahakamani wameshajiandaa na wameshatorosha wanachoweza kutorosha.
 
ada ya mja hunena muungwana vitendo
semeni wazi kuwa hamumpendi jk
mbona wakati wa bm hamkuthubutu kusema????
Mzee rukhsa alilizika azimio la arusha mbona hamsemi
chakufahamu hapa ni hata kama sisi wana jf wote hatumtaki pamoja na wasomao magazeti lakini mjue kuna mamilioni ambao wako nyuma yao jee hao wote ni wajinga??????

Hivi ni raisi gani amewahi kuthubutu kuwapeleka mahakamani idadi kubwa ya viongozi tangu tupate uhuru???? Au mlitaka awahukumu kwa kuwaweka kizuizini kama zile enzi???????

Kwanza kabisa, kwamba mwizi mmoja kaiba na hajakamatwa haihalalisha kwa mwizi wa pili kuiba, na akikamatwa hawezi kusema "mbona fulani hamjamkamata".Huu si utetezi, ingekuwa hivyo justice system isingeweza kufanya kazi maana ili kumkamata mwizi mmoja ingebidi kukamata wezi wote, kitu ambacho hakiwezekani. Two wrongs do not make a right.

Pili, wewe unaongelea Mkapa na Mwinyi gani? Mbona tumewasema sana sio hapa tu, kuanzia Nyenzi, Tanzanet BCS, YA mpaka Jamboforums na sasa Jamii Forums, wewe unaongelea hawasemwi wapi?

Of course kwa sasa Kikwete atasemwa zaidi kwa sababu yeye ndiye rais na mtu mwenye responsibility ya mwisho Tanzania.

Watu wanamsema huyo golden boy wa propriety bongo, Julius KAmbarage, itakuwa huyu muhuni asiyejua kujifuta kamasi za kisiasa Jakaya Kikwete?

Forget about marais, watu wanamsema huyo mungu mwenyewe, itakuwa hawa binadamu?

Kuhusu kupeleka watu mahakamani, tatizo si kuwapeleka mahakamani, tatizo ni nini kinafanyika baada ya hizi sarakasi za mahakamani? Na kama kweli anataka kupeleka watu mahakamani anasubiri nini kuwapeleka kina Chenge na Mkapa?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom