Mazyar Ebrahimi: Nililazimishwa na Iran kuwa Jasusi wa Israel

FRANC THE GREAT

JF-Expert Member
May 27, 2016
5,328
7,702
Mazyar Ebrahimi: Iran ilinitesa na kunilazimisha kukiri kuwa Jasusi wa Israel

1565723577824.png

Mazyar Ebrahimi anasema aliteswa kwa siku 40 mfululizo usiku na mchana.

Aliyekuwa mfanyabiashara mwenye mafanikio wa Iran wakati mmoja anasema ana bahati kuwa hai baada ya kuteswa na mamlaka za Iran baada ya kulazimishwa kukiri kuwa jasusi wa Israel na kuhusika na mauaji ya wanasayansi wa nyuklia, uhalifu unaoadhibiwa kwa kunyongwa.

Hadithi ya Mazyar Ebrahimi, ambaye kwa sasa anaishi ng'ambo, pia inatoa mwangaza zaidi juu ya uhasama mkubwa baina ya mashirika ya ujasusi ya Iran, kama anavyoelezea mwandishi wa BBC idhaa ya Persia Jiyar Gol.

Alikutana na Mazyar Ebrahimi mjini Frankfurt Julai, miezi kadhaa baada ya kumpigia simu bila kutarajia kutoka Ujerumani. Gol alishanga sana, kwani alifikiri kuwa alikuwa ameuawa muda mrefu.

Hii ni kwasababu mwaka 2012, yeye na watu wengine 12 walionekana kwenye televisheni ya taifa wakikiri kufanya makosa kadhaa ambayo adhabu yake ilikuwa ni kifo. Huku wakiangalia kwenye kamera ya televisheni, walisema kuwa walikuwa wakipokea mafunzo nchini Israel kabla ya kurejea nchini Iran na kuwauwa wanasayansi wa nyuklia.

Maandishi waliyokuwa wakiyasoma yalikuwa yameandikwa na Wizara ya Ujasusi - moja ya mashirika mawili ya ujasusi ya Iran ambalo lilidai kuwa lilivunja mtandao wa ujasusi wa Israel. Katika chumba chake cha hoteli, tulitazama video ambapo alidaiwa kukiri.

Akionekana mwenye kutetemeka bado hata baada ya miaka yote hii, Mazyar Ebrahimi anasema alikubali ''kukiri'' baada ya kufanyiwa msururu wa mateso kwa karibu siku 40 mchana na usiku.

"Walionihoji walikuwa wanapiga nyayo za miguu yangu na waya wa umeme,"

Alikumbuka Mazyar Ebrahimi mwenye umri wa miaka 46.

"Walivunja mguu wangu. Kipigo kiliendelea kwa miezi saba."

Kabla ya kukamatwa na wizara ya ujasusi, Bwana Ebrahimi alikuwa anaendesha kampuni ya kutengeneza studio za Televisheni. Alikuwa akisafiri mara kwa mara nje ya nchi kufanya kazi hiyo. Anaamini mmoja wa washindani wake alimshutumu kufanyia ujasusi mataifa ya nje kimakosa.

1565723757623.png

Kikosi cha Iran cha Revolutionary Guard Corps (IRGC) kilianzishwa mwaka 1979 I kulinda mfumo wa kiislam wa Iran.

Mwaka 2010 hadi 2012, wanasayansi wanne wa nyuklia wa Iran waliuawa, na huduma za ujasusi za Iran zilikuwa chini ya shinikizo kubwa kuwapata wahusika wa mauaji hayo. Bwana Ebrahimi walikuwa mmoja wa watu zaidi ya 100 walishutumiwa kuwa majasusi.

Anaseama alikuwa tayari kukubali lawama yoyote ile na alitaka kufa ili kuepukana na mateso makali na kudhalilishwa. Lakini licha ya "kukiri kwake", Bwana Ebrahimi anasema, waliomuhoji walitaka zaidi.

Mwaka 2011, milipuko mikubwa iliharibu kiwanda cha makombora kinachoendeshwa na kikosi cha Iran cha Revolutionary Guard Corps (IRGC). Wataalamu kadhaa wa makombora waliuawa. Bwana Ebrahimi anasema shirika la ujasusi lilimtaka akiri kuwa alihusika na milipuko hiyo.

"Aliyenihoji alisema: 'wenzetu kutoka kikosi cha IRGC watakuuliza maswali kadhaa. Uzungumzie tu kuhusu mlipuko, useme kile tu ulichoambiwa,'"

Anasema Bwana Ebrahimi.

Wakati huo kulikuwa na ushindani mkubwa baina ya IRGC na wizara ya ulinzi katika kukabilia na ugaidi. Na nilikuwa ninahojiwa na afisa wa ujasusi wa IRGC juu ya miezi saba baada ya kukamatwa kwa mara ya kwanza na hilo lilimnusuru, anasema Ebrahimi.

Afisa huyo alikasirika baada ya kugundua kuwa kulikuwa na utofauti wa wazi katika ushahidi alioutoa Bwana Ebrahimi uliobuniwa na wizara ya ujasusi. Ghafla, kipigo kikasitishwa , na wizara ya ujasusi hata ikaomba msamaha kwa Bwana Ebrahimi na watu wengine waliokuwa wanakabiliwa na mashtaka sawa na yake.

Lakini Bwana Ebrahimi na wafungwa wengine walisalila gerezani kwa siku nyingine 26, na wakaachiliwa huru 2015.

Mashirika ya huduma za ujasusi za Iran yamekuwa yakibuni kesi na kuwalazimisha watu wasio na hatia kukiri kutekeleza uhalifu, anasema mtaalamu wa masuala ya usalama Muiran Mehdi Mahdavi Azad anayeishi Bonn.

1565723863749.png

Kikosi cha Iran cha Revolutionary Guard Corps (IRGC).

Anasema miaka michache iliyopita huduma za ujasusi za kikosi cha IRGC ziliwashutumu wapatanishi wa masuala ya nyuklia na wanamazingira kufanya ujasusi, lakini wizara ya ujasusi baadae ikathibitisha kuwa kesi zao zilikuwa zimebuniwa.

Baada ya kuachiliwa huru, Bwana Ebrahimi aliwasilisha malalamiko yake dhidi ya wizara ya ujasusi, Televisheni ya taifa ya Iran na magazeti kadhaa yaliyomshutumu kimakosa kuwa yeye ni jasusi wa Israeli. Hata hivyo, aliacha malalamiko yake baada ya jaji aliyekuwa akichunguza malalamiko yake kummshauri akubali fidia. Alisema kuwa jaji alimwambia kuwa:

"Mtu fulani anaweza kukuchoma kisu mgongoni gizani usiku mtaani. Wewe ni kijana ,usijihatarishe."

Mbunge maarufu mwanamageuzi wa mjini Tehran, Mahmoud Sadeqi, alituma ujumbe wa twitter alitoa wito kwa wale waliohusika na kuwalazimisha watu kukiri kimakosa kutoa maelezo.

Bwana Ebrahimi alihamia Ujerumani miezi sita iliyopita, na kuomba uhamiaji huko. Lakini hata sasa, huwa anawasiwasi mkubwa, na uti wake wa mgongo umeharibiwa. Miongoni mwa wale "waliokiri" kufanyia ujasusi Israel, ni mmoja tu aliyehukumiwa kunyongwa, Anasema Ebrahimi.

1565723957847.png

Televisheni ya Iran ilionyesha paspoti ya Israeli yenye picha ya Bwana Fashi

Majid Jamali Fashi alinyongwa miezi miwili kabla ya kukamatwa kwa Bwana Ebrahimi. Televisheni ya taifa ya Iran ilionyesha kile ilichosema ni Paspoti ya Fashi ya Israeli . Ilionekana kama picha iliyotengenezwa ya paspoti ya Israeli iliyochukuliwa kutoka kwenye mtandao wa Wikipedia.

Inaaminiwa kuwa Bwana Fashi alikamatwa baada ya mtandao wa Wikileaks kuchapisha kuhusu mtandao wa kibalozi wa Marekani mwaka 2009. Mtandao ulionekana kuwa na mahusiano na mkutano katika ubalozi wa Marekani mjini Baku, Azerbaijan, ambako Bwana Fashi alizungumzia juu ya mateso nchini Iran. Wikileaks bado haijajibu ombi la mahojiano kuhusu suala hilo.

Video hapo chini wakati Mazyar Ebrahimi akikiri katika televisheni ya taifa mwaka 2012:






BBC Swahili | BBC World News
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom