Mazuri ya Edward Lowassa

quarz

Member
Sep 3, 2006
84
16
Mambo ya pm Lowassa hayo, anatukumbusha enzi zile za pm sokoine.

Lowassa aendelea kuumbua vigogo

Ingawa Wahenga wana msemo usemao mgeni njoo mwenyeji apone kwa mabosi wa mkoa wa Kigoma hali imekuwa tofauti baada ya mgeni wao, Waziri Mkuu Bwana Edward Lowassa kuwaonjesha joto ya jiwe hadharani.

Miongoni mwa walioonja shubiri ya Waziri Lowassa ni Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, Bw. John Mongella ambaye bila kutarajia alijikuta akikatizwa kusoma ripoti yake yenye kurasa zaidi ya 10 wakati ndiyo kwanza amefika ukurasa wa tatu.

Ripoti hiyo ilianza kumchafua Waziri Mkuu pale Mkuu huyo wa Wilaya aliposema kuwa chanzo cha kuzorota kwa kilimo cha kahawa ni ukosefu wa wataalam wa zao hilo.

Bw. Lowassa akasema hayo ni mambo ya zamani asiyotaka kuyasikia katika ziara yake na badala yake anahitaji kuona wakuu hao wa wilaya wakionyesha kwa vitendo uelewa wao baada ya kupigwa msasa wa nguvu na Rais Kikwete kwenye semina elekezi iliyomalizika hivi karibuni huko Arusha.

''John huna taarifa, afadhali twende kwenye ziara'', akasema Bw. Lowassa na kuinuka kuendelea na ziara.

Bosi mwingine aliyekumbwa na kasheshe hilo ni Mkuu wa wilaya ya Kibondo Luteni Kanari John Mzurikwao ambaye naye aliambiwa ripoti yake ni mbovu.

Waziri Mkuu akazidi kumuumbua mkuu huyo wa wilaya kwa kusema kuwa anashangazwa na utendaji wake wa kazi kwa vile ni tofauti kabisa na jinsi anavyomfahamu.

Akasema inaonekana wakuu hao wa wilaya hawakuambulia kitu katika semina elekezi iliyoendeshwa na Rais Kikwete hivi karibuni katika hoteli ya Ngurdoto iliyopo nje kidogo ya Jiji la Arusha.

''Inaonyesha kuwa semina ile haikueleweka wala hotuba ya Rais aliyoitoa mwishoni mwa mwezi uliopita haikusikilizwa, ndio maana mambo haya yanajitokeza'', akasema Bw. Lowassa.

Kana kwamba hiyo haitoshi, Lowassa pia akamuibukia Katibu Tawala wa wilaya ya Kigoma, Bw. Martin Mgongolwa na wakurugenzi wa wilaya hiyo kwa kushindwa kumsaidia mkuu wa wilaya na badala yake wakamuandalia hotuba iliyopitwa na wakati.

Akasema Mkuu wa wilaya hiyo bado ni mgeni na anahitaji msaada wa viongozi wengine wa wilaya ambao wana uzoefu na maeneo yao.

''Mnashindwa kuwasaidia vijana hawa na mnataka sisi tuwashambulie bure'', akacharuka Bw. Lowassa.

Waziri Mkuu yuko mkoani Kigoma kwa ziara ya siku tano akikagua miradi mbalimbali ya maendeleo.
 
kijana John Mongella pole sana, naona wazee/wakongwe/experienced wameshindwa kukupa ushirikiano, be careful next time wasikuingize mkengeni.
 
Lowasa tuta muumbua kama hataleta mvua kujaza maji Mtera na mengine tulimie mboga zetu zamu yake inakuja .
 
Pm anaonesha mfano kwa dagaa, wakati hata yeye ni fisadi tu, huko ni kujikosha eti anafanya kazi, mangapi wanafanya kuzidi hilo la mkuu wa wilaya kg, kama ye shujaa, aanzie juu kushuka chini. Mapapa ya uozo hayashughulikii, lakini dagaa ndo anaonea. Mungu atawahukum siku moja.
 
Vitendo vya kuumbuana mbele ya kadamnasi si busara na siku moja Lowassa atakutana na Mkuu wa Wilaya mbishi (kama wapo watu wa aina hiyo, naamini wanawachuja karibu wote) atakayejibishana naye itakuwa mambo ya aibu.

Mara nyingi sana Lowassa anafanya haya mambo ya kimangimeza inanifanya nijiulize hivi kweli kati ya Lowassa anayekaa Dar-es-salaam na Wakuu wa wilaya wanaokaa Wilayani nani anayajua zaidi matatizo ya wilayani?

Hivi Lowassa ana point kwamba wakuu wetu wa wilaya kila anapokwenda ni hopeless au ni yeye ndiye aliye na matatizo ya umangimeza?

Mbona hajajibu hoja ya ukosefu wa wataalamu?
 
Hivi ina maana Waziri Mkuu huwa hakutani na hao wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi, ama Wakuu wa Mikoa kwanza kwenye mikutano ya viongozi pekee kupata briefing na kuuliza maswali kabla ya kwenda mbele ya wananchi? Kama viongozi hawafanyi hivyo basi hilo ni kosa la kiutendaji.

Mwalimu mkuu hawezi kuja kugombana na mwalimu au hata Head Prefect mbele ya wanafunzi. Wakiwa Public wote wako kwenye upande mmoja...wakiwa kwenye closed doors huo ndio muda wa kuuliza maswali na kukataa risala, na hata kukunjana mashati wakipenda.

Halafu hii tabia ya PM kuwashukia "vidagaa" (wenyeviti wa vijiji, makatibu kata, makatibu tarafa, wakurugenzi, na wakuu wa wilaya) wakati kuna "ma-papa" yamejaa hapo Dar kwenye wizara na sehemu nyingine nyeti za Serikali kama vile BoT, TRA, TANESCO, Kwa bwana Hosea, n.k. its simply showing kwamba he doesn't know his borders.

Hivi PM unapowafuatilia ma-DC, ma-RC wao wanafanya nini?
 
hivi wakuu wa mikoa huwa hawapeleki ripoti zao za mwaka
kwa waziri mkuu na badala yake wanangoja waziri mkuu
awatembelee ndio watoe ripoti? kama huwa wanangoja waziri mkuu awatembelee ndio wampe ripoti na hali hiyo waziri mkuu anaikubali basi kuna tatizo la kiutendaji katika ofisi ya waziri mkuu.

je waziri mkuu anapotembelea mikoa na wilaya huwa hapati ripoti kabla ya kuanza ziara yake ili kama kuna suala la kiutekelezaji linalohitaji majibu/suluhisho awe amelifanyia kazi na kwenda kuwapa wananchi majibu ya uhakika?

binafsi naamini wakati mwingine majibu makali au mtu mkali huwa anajaribu kuficha udhaifu wake au mapungufu yake.

wakati mwingine kumdhalilisha mtendaji wako mbele ya wananchi kunaweza kukawa na athari zaidi kuliko manufaa.

hapo juu kuna mtu ameuliza kama kuna mkuu wa wilaya anayeweza kumbishia waziri mkuu hadharani. ndio mwaka jana mkuu wa wilaya ya nyamagana (kama sikosei) mwanza ambaje ni mjeshi alimwambia waziri mkuu hadharani kwamba anauzoefu wa uongozi wa miaka 24 kwa hiyo waziri mkuu hawazi mwambia eti hajui kazi.
 
Mimi namuunga mkono Lowassa maana report nyingine ni utumbo usio na kikomo. Kuna matatizo ambayo yapo ndani ya uwezo wa wilaya kuyatatua lakini hawafanyithen kiongozi wa juu akija ndio wanasema.

Nakumbuka 2006 nilikuwa nafanya kazi kwenye wilaya kama tisa hivi na kuna rasimu ilipitishwa kwamba kila wilaya na kila Idara lazima ipeleke report ya utendaji kila alhamis kwenye wizara husika na lazima ihidhinishwe na DED/RAS au DC.

So inawezekana Lowassa alishajua uozo hata kabla hajatoka Dar so alitaka kusikia tu ni sababu gani watakuja nayo. kumbuka kamwambia "Huna taarifa".

Lakini bado haisaidii kumwuumbua bali kuwaachisha wale wote walioshindwa kufanya kazi.

Inawezekana kuna mgawanyo wa kazi kati ya Pm na mkuu wa kaya. Mawaziri na wakuu wengine Wizarani ni kazi ya mkuu wa kaya. Tusbiri tuone na yeye atamuumbua nani.
 
HIVI MMESAHAU KAULI YA JK KUWA ATAWASEMA HADHARANI? baadhi yenu mkaona si adhabu kubwa? sasa PM kaanza kuifanyia kazi NYIE MNALALAMIKA...kuwamwaga hadharani nako kutafanya hawa viongozi wajiandae..wewe ukasome page 10 yanini? kwanini viongozi wasiwe wakweli? Pia kuwalaumu wakurugenzi pia si vyema. ina maana Mkuu wa WILAYA kum-by pass mtendajji ni sawa?

Au MKUU WA WILAYA ALITAKA MISIFA? aonekane kijana kaandaa ripoti safi...?KIONGOZI ANASHINDWA NINI KUWA MBUNIFU...au UBUNIFU HAUNAO KWANI USIWAULIZE SENIORS? au WATAALAMU UNAWAAMINI?

NAPENDA KUMUULIZA MZEE ES..ina maana huyu mkuu wa WILAYA NI MTOTO WA MONGELA?
 
Lowassa ni bogus sana.

Kama protokali ya kazi inasema kuwa waziri mkuu akija wilayani inabidi mkuu wa wilaya hiyo amsomee ripoti ya shughuli za maendeleo wilyani humo inakuwaje yeye anataka utaratibu huo ubadilishwe on the fly?

Anatafuta sifa zisizokuwa na kichwa wala miguu.
 
HIVI MMESAHAU KAULI YA JK KUWA ATAWASEMA HADHARANI? baadhi yenu mkaona si adhabu kubwa? sasa PM kaanza kuifanyia kazi NYIE MNALALAMIKA...kuwamwaga hadharani nako kutafanya hawa viongozi wajiandae..wewe ukasome page 10 yanini? kwanini viongozi wasiwe wakweli?.......................

Kwa nini "aweseme hadharani" wakati ni yeye aliyewateua. Anatakiwa kuwafukuza kazi mara moja, siyo kutafuyta visingizio.
 
Vitendo vya kuumbuana mbele ya kadamnasi si busara na siku moja Lowassa atakutana na Mkuu wa Wilaya mbishi (kama wapo watu wa aina hiyo, naamini wanawachuja karibu wote) atakayejibishana naye itakuwa mambo ya aibu.

Mara nyingi sana Lowassa anafanya haya mambo ya kimangimeza inanifanya nijiulize hivi kweli kati ya Lowassa anayekaa Dar-es-salaam na Wakuu wa wilaya wanaokaa Wilayani nani anayajua zaidi matatizo ya wilayani?

Hivi Lowassa ana point kwamba wakuu wetu wa wilaya kila anapokwenda ni hopeless au ni yeye ndiye aliye na matatizo ya umangimeza?

Mbona hajajibu hoja ya ukosefu wa wataalamu?

Mbona ashakumbana nae sana tu kule Mwanza?
Hii ilikuwa ni mwaka jana mwishoni mwishoni, kuna mkuu wa wilaya (simkumbuki jina) alimnanga EL mbele ya wananchi, kwamba yeye yuko madarakani kwa miaka 25, sasa iweje Lowassa amwambie hajui Kazi? Lowassa alikuwa kakataa ripoti ya jamaa huyu. Vichwa ngumu wapo wa mukwaga tu sasa, sio sawa na enzi za Mwalimu.
 
Nchi yetu inahitaji viongozi shupavu na si kidogo, mimi ninaunga mkono staili hii ya Mh Lowasa. iwapo kiongozi anashindwa kutimiza majukumu yake kwa uzembe huyo si wa kumuonea haya hata kidogo. haiwezekani mathalani Waziri mkuu apewe /asomewe ripoti kuhusu ubadhirifu wa pesa za wilaya halafu eti akae kimya asikemee waziwazi hali hiyo eti angoje vikao ndo akakemee.

besides Waziri mkuu ana majukumu mengi, kwa nini akae kupoteza muda kusikiliza hotuba karatasi kumi wakati ni dhahiri hotuba hizo hazina substance.si bora aendelee na shughuli nyingine muhimu za ziara?.

mfano wa mkuu wa shule na walimu mbele ya wanafunzi sidhani kama unaendana hapa,mwanafunzi ni kama askari utii mbele na wala si kuhoji hoji utendaji wa wakubwa, wakati wananchi ndo mabosi wa serikali, kwa hiyo Waziri Mkuu kuwasema wakuu wa wilaya wenye utendaji mbovu mbele ya wananchi ni sawa kabisa kwa sababu wananchi wana haki ya kuona Matatizo yao yanashughulikiwa na wale waliopewa dhamana ikiwa ni pamoja na kutowaonea haya watendaji wabovu.
 
Mkuu Gamba la Nyoka..

Kama kiongozi anashindwa kazi kwa nini asiwe let go? Na kwa nini hii tabia ni kwa watendaji wa ngazi za chini? Je imeonyesha wapi imefanya kazi?

Ni kweli viongozi wetu wengi ni wabovu na ndio maana majengo mengi ya Serikali hupigwa rangi na mawe kupakwa chokaa siku Rais, PM, wanapotembelea hilo eneo. Maana yangu ni kwamba...viongozi wengi hawafanyi kazi mpaka siku anakuja bosi kuwatembelea ndio na wao wanaanza matayarisho ya ghafla ya zima moto.

Mimi naona kosa ni la ofisi ya Waziri Mkuu kwa kutokuwa na standard perfomance measurements ambazo zinatakiwa ziwe reviewed kila baada ya miezi 6 au kila mwaka. Kama hawa wakuu hawakufikia goals zilizowekwa, they should be fired, lakini ni ukiritimba tu umetujaa.
 
Back
Top Bottom