Mazungumzo ya Biden na Macron na mgogoro wa Nyambizi

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,991
17,888
Ijumaa Rais Joe Biden wa Marekani alikutana na kuzungumza na mwenzake wa Ufaransa Rais Emmanuel Macron kuhusu mkataba wa mauzo ya nyambizi kati ya Washington na Canberra, ambao umeikasirisha sana Paris.

Rais Biden amesema katika mazungumzo hayo yaliyofanyika mjini Rome Italia kwamba Washington haikuzingatia busara na kuihusisha Paris kabla ya kutia saini mkataba huo. Mazungumzo hayo ni sehemu ya juhudi za karibuni kabisa za Marekani zinazolenga kupunguza mvutano kati yake na Ufaransa kuhusu mkataba huo. Hata kama Biden hakumuomba msamaha rasmi Mocron kuhusu mkataba huo lakini alisema Marekani haikupasa kumuweka gizani rafiki yake huyo mkongwe kuhusu jambo hilo.

Biden ameonana na kuzungumza na Macron katika safari yake ya pili barani Ulaya tangu achaguliwe kuwa rais wa Marekani Januarai mwaka huu. Viongozi hao wameonana na kuzungumza pembeni mwa kikao cha siku mbili cha viongozi wa kundi la G20 huko Rome Italia.

[https://media]Nyambizi zikiwa kwenye shughuli za kawaida majini

Uhusiano wa Marekani na Ufaransa umeingia doa tokea kutangazwa mwezi Septemba kubuniwa muungano mpya wa kiulinzi AUKUS, kati ya nchi tatu za Marekani Uingereza na Australia, na ambao umepelekea kufutiliwa mbali mkataba wa mauzo ya nyambizi kati ya Australia na Ufaransa kwa manufaa ya Marekani.

Kufuatia kufutilia mbali mkataba huo, Marekani imepanga kuiuzia Australia nyambizi nane za nyuklia ambapo Uingereza nayo itashirikishwa kwenye mkataba huo kwa kuijengea Australia taasisi nyeti za kiulinzi katika bandari ya Adelaide.

Kufutiliwa mbali mkataba huo bila shaka kumetoa pigo kubwa la kisiasa na kiitibari kwa Ufaransa. Marekani inadai kwamba nyambizi hizo zitaongeza pakubwa uwezo wa kijeshi wa Australia ambayo ni rafiki yake mkongwe katika eneo la Indo-Pacific, katika kukabilian na eti tishio la China.

Pamoja na hayo lakini radiamali ya viongozi wa Paris inathibitisha wazi uongo wa madai hayo ya viongozi wa Washington. Ufaransa ambayo ni rafiki mkongwe wa Marekani imekasirishwa sana na hatua hiyo ya Marekani na kusema ni usaliti wa wazi dhidi ya Paris, jambo lililoipelekea kumuita nyumbani kwa muda balozi wake huko Washington.

Serikali ya Biden ambayo haikutarajia radiamali hiyo kali ya Ufaransa ililazimika kulegeza msimamo na kuanza kutumia maneno matamu kwa ajili ya kuwatuliza Wafaransa. Licha ya Marekani kutuma Ufaransa viongozi wake wa ngazi za juu akiwemo Anthony Blinken, Waziri wa Mambo ya Nje kwa ajili ya kuwatuliza viongozi wa Paris lakini bado Ufaransa imeendelea kukashifu na kuikosoa Marekani kwa usaliti wake dhidi ya marafiki zake wakongwe.

Celia Belen, mchambuzi wa masuala ya Ulaya na Marekani anasema: Mgogoro wa sasa kati ya Paris na Washington, ni pigo kubwa kwa Wafaransa. Hii ni kwa sababu hakuna hatua yoyote ya msingi iliyochukuliwa kwa ajili ya kuifidia Ufaransa kutokana na hasara iliyopata baada ya kufutiliwa mbali mkataba wa mauzo ya nyambizi wala nchi hiyo kushirikishwa katika muungano wa kiulinzi katika eneo la Indo-Pacific.

[https://media]Mkataba wa AUKUS baina ya Marekani, Uingereza na Australia

Kwa hakika serikali ya Biden imekuwa ikitamka maneno matupu tu ya kidiplomasia na yasiyo na maana yoyote kwa ajili ya kuwafurahisha Wafaransa. Kwa ibara nyingine ni kuwa Marekani imekuwa ikikanyaga wazi maslahi ya Ufaransa kwa ajili ya kujidhaminia maslahi yake ya upande mmoja katika eneo muhimu la Indo-Pacific.

Hilo ndilo jambo ambalo limemkasirisha Macron na kumpelekea ZzitakE nchi za Ulaya zisihadaike na utapeli wa Marekani katika uhusiano wa pande mbili.

Katika safari yake barani Ulaya, Biden amedai kuwa amekutana na Rais Macron ili kuondoa hasira na dhana mbaya iliyopo kati ya pande mbili na kurejesha uhusiano wa Paris na Washington katika hali ya kawaida. Pamoja na hayo, ni wazi kuwa hatua kama hizo za kimaonyesho tu hazitaweza kupunguza hasira ya Wafaransa kuhusu usaliti wa karibuni waliofanyiwa na Wamarekani.

4by5e82280dd361y4d4_800C450.jpg
 
Back
Top Bottom