Mazungumzo na Maureen Minanago wa TBC Kitabu cha Judith Listowel ''The Making of Tanganyika'' (1965) tarehe 25 Januari, 2021

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,857
30,205
MAZUNGUMZO NA MAUREEN MINANAGO WA TBC KITABU CHA JUDITH LISTOWEL ''THE MAKING OF TANGANYIKA'' (1965)

Kesho Jumatatu Insha Allah saa tatu na nusu asubuhi Maureen Minanago katika kipindi, ''Kurasa Darasa,'' atanihoji kwa mara ya pili kuhusu kitabu alichoandika Lady Judith Listowel, ''The Making of Tanganyika.''

Judith Listowel ndiyo mtafiti na mwandishi wa kwanza kuandika historia ya uhuru wa Tanganyika, historia ambayo imejaa utata mkubwa hata pale yalipoandikwa Maisha ya Julius Nyerere (2020) maswali bado yamebakia kuwa mengi.

Kwa nini baadhi ya wazalendo waliopigania uhuru wa Tanganyika chini ya TANU na wengine kuasisi TANU yenyewe, imekuwaje historia zao zimekuwa kama vile zinawatisha watafiti hawawezi kuziandika sawasawa?

Kuna tofauti gani kati ya Judith Listowel na waandishi wengine waliokuja kuandika historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika baada yake?




 

Similar Discussions

Back
Top Bottom