Mazungumzo kati ya Tanzania na Malawi juu ya Ziwa Nyasa yavunjika tena!

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,985
20,263
Kwamjibu wa taarifa toka vyanzo vyetu muhimu ndani ya ardhi ya Malawi, ni kuwa majadiliano yaliyotakiwa yaendelee yamevunjia baada ya kutofautia misimamo ya wahusika!

Taarifa zaidi itawajia punde!
 
Hivi vinyasa dawa yao ni kuvitandika tuu, kwenye mazungumzo tunapoteza muda!
 
Meza ya majadiliano bado inahitajika kwa kila njia,

Dunia inaona, lazima tuungwe mkono na kila mmoja wetu
 
Hahahahaaaaa watasusaaaaaa lakini tusije ambiwa "tumeona kwa ajili ya amani basi ziwa loooote tuwaachie" haki ntapiga mtu!!!!
 
Ogopa vita kama ukoma.
Cha msingi ni suluhu,hakuna haja ya kupoteza maisha ya watu wetu. Tujiulize ni kwa nini miaka yooote hiyo Wamalawi walikuwa kimya?Jibu:ni kuwepo fununu za mafuta ndani ya ziwa Nyasa-bado haijadhibitika.

Tujiulize ni maisha ya watu wetu wangapi yamepotea ktk migodi yetu eg. North Mara,Buzwagi etc? Je,ikiwa kweli mafuta yatapatikana ni wavuvi wangapi watakaopoteza maisha huko? Tuwe serious jamani. Leo tuanze kupoteza askari na raia wetu,halafu tukishalichukua(kama tutaweza) wavuvi waanze kuuawa mara tu watakapoonekana wakipita eneo lenye mafuta. Huu si wendawazimu?! Halafu nani katudanganya kuwa tutawashinda malawi kirahisi hivyo,au hata tukiwashinda,tunadhani tutabaki salama?

Hebu tuache masikhara jamani.Wote tunafahamu uwezo wa Israel kijeshi na ule wa Palestine;je waisrael wanakaa kwa amani?
 
Hivi Maziwa yote tuliyonayo yanatunufaisha lipi! kwanza naomba nielimishwe hapo halafu mnipe na faida ya sisi kuwa na madini.
 
Kule Malawi wakaazi wana mchanganyiko mkubwa sana Mkuu. Kuna vikabila vingi sana kule, likiwapo kabila la Wanyakyusa, Wandali, Walambya na Wanyiha, makabila ambayo yapo pia Tanzania. Kuna wajomba za watu kule, mashemeji, kuna kina baba mkubwa, baba mdogo, mashemeji na kadhalika. Vita na malawi itakuwa sawa na mtu anajipiga nyundo vidole. Sema tu ikibidi mtu unafanyaje sasa....

Kweli tatizo ni mafuta. Inavyoonekana Mkondo wa mafuta umeingia ndani ya ziwa; lakini kuna viashiria mkondo huo umepita nchi kavu katika upande wa tanzania, ambapo upande wa Malawi mkondo huo haupo nchi kavu; kwa hiyo wanataka kufosi wapate mafuta hayo kwa kutumia Ziwa. Pana harufu ya vita hapa kwa hakika, kwa sababu stakes are very high! Mimi binafsi nipo tayari hata kujitoa mhanga kulinda kupisi chetu cha ziwa, na ninajua karibu watanzania wote tunawaza hivi.

Sema tu pana kijitatizo: kuwa hatutakuwa tunapigana na Malawi. Malawi ni rafiki mkubwa sana wa Israel na Uingereza. Na kila unapomkuta Israel na Uingereza, ujue na Marekani yupo. Hivyo vita hii itakuwa ni vita kati ya Tanzania na hasa hasa Uingereza na Marekani. Sina shaka kabisa na mtizamo huu. Tujipange tu vizuri. They are human and just as vulnerable, as long as they live here on planet earth.

Malawi anapata wapi kiburi?
 
Mimi nisichoelewa ni kwa nini mazungumzo yanang'ang'aniwa wakati kutoka enzi za nyuma yalishindikana. Waende mahakamani wakamaliza suala hili!
 
Kiburi cha wamalawi juu ya hilo ziwa ni kuwa UK na USA wana makampuni yao ya utafiti wa mafuta ndio maana wana kiburi wanajua Tanzania hata iweje hawataweza kuwachapa hizo nchi zitaikemea Tanzania na wataendelea kupiga kelele kupatanishwa!kelel zao si bure
 
Tutawavumilia mwisho tutachoka
 
natamani ziwa lote lichukuliwe na Malawi maana hatuna faida nalo kabisa!
 
Ogopa vita kama ukoma.
Cha msingi ni suluhu,hakuna haja ya kupoteza maisha ya watu wetu. Tujiulize ni kwa nini miaka yooote hiyo Wamalawi walikuwa kimya?Jibu:ni kuwepo fununu za mafuta ndani ya ziwa Nyasa-bado haijadhibitika.

Tujiulize ni maisha ya watu wetu wangapi yamepotea ktk migodi yetu eg. North Mara,Buzwagi etc? Je,ikiwa kweli mafuta yatapatikana ni wavuvi wangapi watakaopoteza maisha huko? Tuwe serious jamani. Leo tuanze kupoteza askari na raia wetu,halafu tukishalichukua(kama tutaweza) wavuvi waanze kuuawa mara tu watakapoonekana wakipita eneo lenye mafuta. Huu si wendawazimu?! Halafu nani katudanganya kuwa tutawashinda malawi kirahisi hivyo,au hata tukiwashinda,tunadhani tutabaki salama?

Hebu tuache masikhara jamani.Wote tunafahamu uwezo wa Israel kijeshi na ule wa Palestine;je waisrael wanakaa kwa amani?
Natamani ungekuwemo kwenye tume ya majadiliano.Ndo Busara sasa izo.Thumbs up mkuu
 
Mhe.Membe,unawajibika moja kwa moja.Busara zitawale ktk hili.Yamalizike bila Vita.Uchumi wenyewe ndo wa ku unga na Super glue,what do we expect kama tutaanza kudundana?
 
Back
Top Bottom