"Mazungumzo Baada ya Habari " TBC yamekufa?

Ibrah

JF-Expert Member
Mar 22, 2007
2,729
528
Kwa karibu wiki moja sasa nimekuwa nifuatilia kile kipindi maarufu cha enzi zile za ukiritimba wa Chama Kimoja na RTD. Katika muda huo sijasikia kile Kipindi cha enzi na enzi kilichotumiwa na Kina Kingunge Ngombale -Mwiru kuwazodoa na kuwalima Wapinzani wa CCM, Mabeberu, Mafisadi na kuwadanganganya Wa-Tz kwa propaganda za Uongo-na-kweli. Kwa hakika kipindi hicho mara nyingine kilitumika vibaya sana ingawa mara chache kilikuwa kinaburudisha na kuzungumzia mambo ya maana.

Wadau, naomba mwenye uhakika wa kipindi hiki atuahabarishe; kipindi kimekufa au hakuna Mazungumzo mapya baada ya habari?
 
MAZUNGUMZO BAADA YA HABARI OF 1980s to early 1990s yalikuwa very educative na babu yangu alituweka sote pamoja jioni kusikiliza kuanzia MICHEZO hadi MAZUNGUMZO BAADA YA HABARI then watoto tuliambiwa tukalale kama siku hiyo hakuna MCHEZO WA REDIO....!
JUST NIMEKUMBUKA.....!
TIDO DO SOMETHING....!
 
MAZUNGUMZO BAADA YA HABARI OF 1980s to early 1990s yalikuwa very educative na babu yangu alituweka sote pamoja jioni kusikiliza kuanzia MICHEZO hadi MAZUNGUMZO BAADA YA HABARI then watoto tuliambiwa tukalale kama siku hiyo hakuna MCHEZO WA REDIO....!
JUST NIMEKUMBUKA.....!
TIDO DO SOMETHING....!

Mkuu,

Umenikumbusha mbali sana!

Hasa michezo ya redio kama ule wa ukikataa pema.....!

Mimi nilikuwa na ratiba kwamba baada ya michezo then mazungumzo yaliyosomwa na S.S Mkamba na then mchezo wa redio (lakini Ijumaa tu).

Siku zingine ni mambo kama benki yako, CRDB, pamba yako, Posta na simu na ATC, du!

Anyway, ndio dunia.
 
TUKUBALI UKWELI.....!
VIPINDI VIMEKUWA VIKITOA ELIMU AMBAYO NI NADRA KUIPATA.....!
SHERIA, BENKI,SIASA, FUNDI UMEME, KODI, NK.
KILA UKIFUNGUA REDIO UNAKUTANA NA MADA AMBAYO KAMA HAITAKUSAIDIA LEO BASI KESHO.....! (tuache burudani 24/7 FM)
 
Who says so??
TBS inatakiwa ijiendeshe, inabidi ifuate mwelekeo wa soko
soko linataka ujinga wao watatoa ujinga.
hio ndio sera ya ubepari, ndio tumechagua
 
Mazungumzo ya habari namkumbuka sana Abdul Ngarawa huyu jamaa miaka ya 1990 alikuwa mwiba na adui mkubwa kwa wanafunzi wa chuo kikuu na madaktari wa Muhimbili haswa pale Mzee wa ruksa alipoamua kwenda kucheza kwasakwasa ya Kanda Bongoman badala ya kusikiliza matatizo yao ya msingi. Jamaa alikuwa hodari sana wa propaganda
 
Si ajabu TBC kusitisha kipindi hicho maana yanayozungumzwa humo yanasuta matendo ya viongozi wa chama tawala ccm. Jitihada zifanyike ili maandishi yake yakipatikana yaandikwe na kusambazwa (ikiwezekana bure) nchi nzima ili kuelimisha wananchi. Yakisikilizwa na kusomwa, uozo wa viongozi wa ccm utajitokeza kama jipu lililoiva!
 
Nakumbuka baadhi ya mazungumzo haya ni:

  • Nokora mpumbavu
  • Urembo wa ndonya
  • Mwizi mwenye suti
  • Unyonge wa Mtanzania
na mengine mengi...
 
Wanajamii msipate taabu. Mazungumzo Baada ya Habari yapo na yataanza kuletwa kwenu na Kiwi. Ni hazina kubwa sana tuliyopewa na Mungu ambayo kuna walioikalia, tunaifufua. Tumejaribu kuyarudisha TBC wamegoma, tunayamwaga jamvini. Kila mwenye macho na masikio asome na kusikia.
 
Back
Top Bottom