Mazuio ya Usafirishaji Mazao Kilimo KM na Waziri Mna Interest Gani

Babu Mdende

New Member
Jul 25, 2017
1
1
Sheria ya hifadhi ya Hifadhi ya Mimea ya Mwaka 1997 ni sheria mama inayoiiunganisha Tanzania na jumuiya za kimataifa katika kufanya Biashara za mazao ya kilimo. Moja ya vipengele vilivyomo katika sheria hii ni kutoa masharti ya kuzingatia ili mazao yao yanapoletwa nchini yawe yamekidhi viwango vya ubora hasa katika masuala ya usafi wa mimea (Phytosanitary). Utaratibu huu unafanywa kupitia kiballi kinachoitwa Plant Import Permit (PIP). PIP hutolewa tu pale ambapo uchambuzi wa kisayansi yaani Pest Risk Analysis (PRA) unapofanywa na mtaalamu na kubaini kuwa zao linaloingia nchini linashambuliwa na visumbufu kadhaa ambavyo haviko kwetu na vinaweza kuingia nchini kupitia njia ya mazao hayo.

Kibali hiki kimisingi ni masharti yanayotolewa na nchi inayopokea mzigo wa bidhaa za kilimo,ili kujilinda na visumbufu vipya ambavyo vinaweza kupitia mazao hayo na kuleta madhara makubwa katika uzalishaji nchini. Baadhi ya visumbufu vigeni ambavyo vimewahi kuingia nchini na kusababisha madhara makubwa katika sekta ya kilimo ni pamoja na dumuzi, inzi wa Matunda, Mnyauko wa ndizi na MLND. Magonjwa haya yametupotezea masoko ya Matunda kwenda nchi za , yanatishia kuondoa zao la Migomba Mikoa ya Kagera, dumuzi serikali imetoa mabilioni ya sh kutokomeza dumuzi katika hifadhi za mahindi.

Huduma za ukaguzi mazao ya kilimo ni nusu kaputi, baadhi ya mipaka haina hata ofisi za ukaguzi tumekuwa jalala la kila ugonjwa unaotokea duniani kwa sababu tu wizara haitilii mkazo kitengo muhimu hiki.

Wameingia hawa wajenga barabara Tizeba na Mtigumwe sijui kwanza wanafanya nini Wizara ya Kilimo (They are most bogus top Ministry in the history of the Ministry of Agriculture) wanataka kufuta vibali, hawaoni umuhimu wake, kimsingi kufuta Import Permit ni kufuta PHS, wakaguzi walioko mipakani zikiwemo bandari na Viwanja vya ndege wanafanya kazi usiku na mchana kuzuia magonjwa na visumbufu vigeni ambavyo vinaweza kuleta majanga makubwa katika kilimo na misitu yetu.

Wameingia madarakani wame freeze export za mazao yote zikiwemo nyanya, Vitunguu, mashudu, Ufuta kwa kisingizio cha usalama wa chakula. Uwekezaji katika kilimo unakufa kibudu na tutarajie a huge decline ya pato la taifa litokanalo na sekta ya kilimo kwa sababu hakuna export za mazao ya kilimo kabisa ambayo ndio chanzo kikubwa cha fedha za kigeni.

Tanzania ni nchi mwanachama wa shirika la Biashara duniani, moja ya makubaliano yaliyomo kwenye itifaki ya hiyo (WTO SPS Protocol) ni nchi wanachama kufanya Biashara huria bila kuingiliwa. Leo hii Tanzania hairuhusiwi kuingiza mazao wala kusafirisha mazao nje ya nchi. Waziri na Katibu Mkuu wake wanataka ku sign vibali wao kazi ambayo kisheria hawana mamlaka hayo. Kuna interest gani na biashara za mazao sasa, mazuio haya ya mpaka nyaya na Vitunguu na mashudu hayakuwepo miaka ya nyuma na watanzania walifurahia soko huria la kuuza mazao yao.

Mkulima wa Tanzania amekuwa mtu wa kuonewa tu na kukandamizwa kila kukicha. Wakati analima mazao yake serikali haimpi hata senti tano lakini punde anapovuna serikali inakuwa kiranja mkuu wa kuzuia kuuza mazao yao kwenye masoko yanayolipa, Hii ni aibu kubwa. Mfanyakazi hapangiwi matumizi ya mshahara wake, wala mfugaji hapangiwi idadi ya kuuza Mifugo yake wala maziwa anayokamua kwa ng’ombe. Mnyonge wa serikali yetu ni mkulima tu ambaye serikali inadhani yeye ni punguani asiyeweza kupanga ni kiasi gani ahifadhi na kiasi gani auze. Leo hii debe la mahindi na mpunga linauzwa kwa sh elf 6 tu. Mipaka yote imefungwa , kenya wanatafuta unga kwenye ma supermarket kwa tochi. Kama tunampenda mtanzania masikini kama tunavyo imba kwenye majukwaa tungemruhusu akauze mahindi yake kenya apate maradufu. Punde mahindi yataa adimika mkulima ataanza kununua mahindi hayo hayo kwa debe elf 20. YEYE ALIYE JUU ANAWAONA.

Marufuku za kuuza mazao nje ya nchi au kuingiza mazao nchini zina tija gani kwa taifa letu?? WHY now?? Tangu lini serikali ikajiingiza kwenye Biashara za watu binafsi?? Serikali si mdhibiti tu ???

Sasa Mmwage Mboga sisi Tunamwaga Ugali ....................................
 
Nilikua naongea na Boss Mmoja wa Mazao dar, Anadai hadi Sasa serikali haitaki kutoa vibali na pia haitaki mbaazii isafirishwe Nje ya nchi,, hadi Muda huu ninavyoandika zao La mbaazii linanunuliwa Kwa wakulima Kwa shs 300 Kwa kilo 1, hii ni Hatar Sana, Mwaka Jana bei ilikua 1200,, ilishuka hadi 1050...

Huku Kusini zao Hili linawasaidia wakulima kupata pesa Kwa ajili Ya kuhudumia mikorosho, sasa gunia moja ni 30,000 kwakwel serikali inabid iliangalie Hili Kwa Umakini Mkubwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom