Crocodiletooth
JF-Expert Member
- Oct 28, 2012
- 20,056
- 23,506
Zanzibar Post
POLISI ZANZIBAR WAFUMBUIA
MACHO UWEPO NA HUJUMA ZA
MAZOMBI SASA KUTUNGULIWA
KWA MISHALE YA KIMASAI ILI
UTAMBULISHO WAO UPATIKANE.
Watu wasiojulikana wanaoingia
mitaani na kupiga wananchi katika
maeneo mbalimbali ya Unguja,
Zanzibar maarufu kama ‘mazombi’,
wameendelea kuvitesa Visiwa vya
Unguja, huku Jeshi la Polisi
likisema halina taarifa zao.
Watu hao wanaojifunika soksi
usoni, wanadaiwa kutumia silaha
za moto na jadi kujeruhi, kupiga
watu mbalimbali hasa katika
maeneo ya Mkoa wa Mjini
Magharibi, Unguja.
Mitaa inayotajwa kuathiriwa na
mazombi hao ni Tomondo,
Sarayevo, Darajabovu, Msumbiji,
Magogoni, Amani Kwa -Mabata,
Mtoni, Bububu, Sharifu Msa,
Kihinani, Kinuni na Welezo.
Hata hivyo, Kamishna wa Polisi
Zanzibar, Hamdan Omari alisema
suala hilo pia linawapa tabu kwa
sababu wanasikia tu kupitia watu
na vyombo vya habari lakini
hawajawahi kupata taarifa rasmi.
Kuhusu watu kuumizwa na
kupigwa na mazombi hao, alisema
wanasikia na wanatamani mmoja
wao aende kutoa taarifa ili iwe
rahisi kwao kulifanyia kazi kuliko
kusikia juujuu bila kuwa na cha
kushika.
“Kama kuna suala linatusumbua ni
hili la mazombi. Mwananchi
mtusaidie kufikisha ujumbe huu,
yeyote atakayedhuriwa na hao
watu aje kutoa taarifa polisi au
apige simu namba za usalama
akiwa eneo la tukio ili iwe rahisi
kuanza kazi ya kuwasaka wahalifu
hao, hatuwezi kushughulikia kesi
bila kuwa na ushahidi,” alisema
Kamishna Omari.
Wakati kamishna huyo wa polisi
akisema hayo, mkazi wa Bububu,
Maalimu Rashid Abdalla alisema
mwanzoni waliwachukulia
mazombi kama mamluki hasa
katika chaguzi tofauti na sehemu
zao wanakoishi, kumbe hali ni
tofauti.
“Mimi nilishuhudia mamluki hao
katika uchaguzi mdogo wa
Mwakilishi wa Jimbo la Bububu
Agosti 16, 2012 walipokuja na gari
aina ya pick-up na kupiga risasi
ovyo hewani kuwatawanya watu
waliokuwa wakipiga kura wakiwa
wamefunika nyuso kwa vitambaa
ili wasionekane,” alisema.
Mkazi wa Sharifu Msa, Bakari
Juma alisema amewahi kuwaona
mazombi akisema ni makundi ya
vijana wapatao 80 ambao hufunika
nyuso kwa soksi, wanatumia
magari yanayobandikwa namba
baadhi ya vikosi vya SMZ ‘pick-
up’, wana bunduki, mapanga,
mikuki, mashoka na kila aina ya
silaha.
“Mnaona kazi hii, mimi nimeponea
chupuchupu siku ile ya uchaguzi,
mazombi walipoingia mitaani pale
Mtoni tukiwa tumekaa ofisini
wakatuvamia,” alisema kijana
huyo, huku akionyesha gamba la
risasi alilodai ni miongoni mwa
yaliyotawanywa na mazombi
mtaani kwao Oktoba 25, mwaka
jana.
Mapema mwaka huu, Kaimu
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa
CUF, Ismail Jussa Ladhu alilaani
vitendo vinavyodaiwa kufanywa na
mazombi hao ikiwamo kuvunja
maskani ya ‘Commonwealth’
iliyopo Michenzani na kung’oa
bendera ya chama chake iliyokuwa
eneo hilo.
‘Mazombi’ wanadaiwa pia kuvamia
Kituo cha Redio cha Hits FM cha
Migombani, Unguja mwishoni mwa
mwaka jana na kusababisha
uharibifu mkubwa wa mali na
kutishia maisha ya watu
waliokuwa studio.
Akisimulia madhara aliyoyapata
kutoka kwa watu hao, Juma
Yassin anayekaanga chipsi katika
eneo la Kibweni, Unguja, alisema
alipigwa na kuporwa fedha zaidi
ya Sh100,000.
“Walipomaliza kufanya
waliyodhamiria walinichukua na
kunitupa vichakani kule karibu na
kiwanja cha mpira cha Meli Nane
(Kihinani, Wilaya ya Magharibi)
mpaka nikapoteza fahamu,
nilipojitambua nikajiburuza,
nikaomba msaada usiku wa
manane nikarudishwa,” alisema
Yassin.
Watu wengine walioripotiwa
kukabiliwa na mazombi usiku wa
kuamkia Jumatano ya wiki hii ni
waziri mstaafu ambaye pia alikuwa
Kamishna wa Mapato Zanzibar,
Mohamed Hashim Ismail ambaye
katika uchaguzi uliopita,
aligombea uwakilishi katika Jimbo
la Dimani kupitia CUF.
“Hawa ni maharamia na walaaniwe
kwa nguvu zote kwani
wanatumiwa kuleta vurugu na
hawaitakii mema nchi hii,” alisema
Mkurugenzi wa Habari na
Uhusiano wa Umma wa CUF,
Salim Bimani.
Suala la mazombi lilitinga pia
bungeni na Naibu Waziri wa
Mambo ya Ndani, Hamad Masauni
alisema Serikali haiyaelewi
makundi hayo lakini itafuatilia kwa
kina taarifa zao.
Aliyekuwa mgombea mwenza wa
urais kwa tiketi ya Chadema na
Ukawa, Juma Duni Haji alisema
kila siku mazombi hao wanapiga
watu, wanatumia magari ya
Serikali na hawachukuliwi hatua.
“Waziri wa Mambo ya Ndani
anajibu bungeni kwamba hakuna
kitu kama hicho, wakati kimekuwa
kikiendelea Visiwani, ” alisema
Duni.
POLISI ZANZIBAR WAFUMBUIA
MACHO UWEPO NA HUJUMA ZA
MAZOMBI SASA KUTUNGULIWA
KWA MISHALE YA KIMASAI ILI
UTAMBULISHO WAO UPATIKANE.
Watu wasiojulikana wanaoingia
mitaani na kupiga wananchi katika
maeneo mbalimbali ya Unguja,
Zanzibar maarufu kama ‘mazombi’,
wameendelea kuvitesa Visiwa vya
Unguja, huku Jeshi la Polisi
likisema halina taarifa zao.
Watu hao wanaojifunika soksi
usoni, wanadaiwa kutumia silaha
za moto na jadi kujeruhi, kupiga
watu mbalimbali hasa katika
maeneo ya Mkoa wa Mjini
Magharibi, Unguja.
Mitaa inayotajwa kuathiriwa na
mazombi hao ni Tomondo,
Sarayevo, Darajabovu, Msumbiji,
Magogoni, Amani Kwa -Mabata,
Mtoni, Bububu, Sharifu Msa,
Kihinani, Kinuni na Welezo.
Hata hivyo, Kamishna wa Polisi
Zanzibar, Hamdan Omari alisema
suala hilo pia linawapa tabu kwa
sababu wanasikia tu kupitia watu
na vyombo vya habari lakini
hawajawahi kupata taarifa rasmi.
Kuhusu watu kuumizwa na
kupigwa na mazombi hao, alisema
wanasikia na wanatamani mmoja
wao aende kutoa taarifa ili iwe
rahisi kwao kulifanyia kazi kuliko
kusikia juujuu bila kuwa na cha
kushika.
“Kama kuna suala linatusumbua ni
hili la mazombi. Mwananchi
mtusaidie kufikisha ujumbe huu,
yeyote atakayedhuriwa na hao
watu aje kutoa taarifa polisi au
apige simu namba za usalama
akiwa eneo la tukio ili iwe rahisi
kuanza kazi ya kuwasaka wahalifu
hao, hatuwezi kushughulikia kesi
bila kuwa na ushahidi,” alisema
Kamishna Omari.
Wakati kamishna huyo wa polisi
akisema hayo, mkazi wa Bububu,
Maalimu Rashid Abdalla alisema
mwanzoni waliwachukulia
mazombi kama mamluki hasa
katika chaguzi tofauti na sehemu
zao wanakoishi, kumbe hali ni
tofauti.
“Mimi nilishuhudia mamluki hao
katika uchaguzi mdogo wa
Mwakilishi wa Jimbo la Bububu
Agosti 16, 2012 walipokuja na gari
aina ya pick-up na kupiga risasi
ovyo hewani kuwatawanya watu
waliokuwa wakipiga kura wakiwa
wamefunika nyuso kwa vitambaa
ili wasionekane,” alisema.
Mkazi wa Sharifu Msa, Bakari
Juma alisema amewahi kuwaona
mazombi akisema ni makundi ya
vijana wapatao 80 ambao hufunika
nyuso kwa soksi, wanatumia
magari yanayobandikwa namba
baadhi ya vikosi vya SMZ ‘pick-
up’, wana bunduki, mapanga,
mikuki, mashoka na kila aina ya
silaha.
“Mnaona kazi hii, mimi nimeponea
chupuchupu siku ile ya uchaguzi,
mazombi walipoingia mitaani pale
Mtoni tukiwa tumekaa ofisini
wakatuvamia,” alisema kijana
huyo, huku akionyesha gamba la
risasi alilodai ni miongoni mwa
yaliyotawanywa na mazombi
mtaani kwao Oktoba 25, mwaka
jana.
Mapema mwaka huu, Kaimu
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa
CUF, Ismail Jussa Ladhu alilaani
vitendo vinavyodaiwa kufanywa na
mazombi hao ikiwamo kuvunja
maskani ya ‘Commonwealth’
iliyopo Michenzani na kung’oa
bendera ya chama chake iliyokuwa
eneo hilo.
‘Mazombi’ wanadaiwa pia kuvamia
Kituo cha Redio cha Hits FM cha
Migombani, Unguja mwishoni mwa
mwaka jana na kusababisha
uharibifu mkubwa wa mali na
kutishia maisha ya watu
waliokuwa studio.
Akisimulia madhara aliyoyapata
kutoka kwa watu hao, Juma
Yassin anayekaanga chipsi katika
eneo la Kibweni, Unguja, alisema
alipigwa na kuporwa fedha zaidi
ya Sh100,000.
“Walipomaliza kufanya
waliyodhamiria walinichukua na
kunitupa vichakani kule karibu na
kiwanja cha mpira cha Meli Nane
(Kihinani, Wilaya ya Magharibi)
mpaka nikapoteza fahamu,
nilipojitambua nikajiburuza,
nikaomba msaada usiku wa
manane nikarudishwa,” alisema
Yassin.
Watu wengine walioripotiwa
kukabiliwa na mazombi usiku wa
kuamkia Jumatano ya wiki hii ni
waziri mstaafu ambaye pia alikuwa
Kamishna wa Mapato Zanzibar,
Mohamed Hashim Ismail ambaye
katika uchaguzi uliopita,
aligombea uwakilishi katika Jimbo
la Dimani kupitia CUF.
“Hawa ni maharamia na walaaniwe
kwa nguvu zote kwani
wanatumiwa kuleta vurugu na
hawaitakii mema nchi hii,” alisema
Mkurugenzi wa Habari na
Uhusiano wa Umma wa CUF,
Salim Bimani.
Suala la mazombi lilitinga pia
bungeni na Naibu Waziri wa
Mambo ya Ndani, Hamad Masauni
alisema Serikali haiyaelewi
makundi hayo lakini itafuatilia kwa
kina taarifa zao.
Aliyekuwa mgombea mwenza wa
urais kwa tiketi ya Chadema na
Ukawa, Juma Duni Haji alisema
kila siku mazombi hao wanapiga
watu, wanatumia magari ya
Serikali na hawachukuliwi hatua.
“Waziri wa Mambo ya Ndani
anajibu bungeni kwamba hakuna
kitu kama hicho, wakati kimekuwa
kikiendelea Visiwani, ” alisema
Duni.