Mazoezi ya kijeshi ya pamoja ya Syria na Russia

STRUGGLE MAN

JF-Expert Member
May 31, 2018
8,638
16,566
Majeshi ya Russia na Syria yamefanya mazoezi ya pamoja ya kijeshi katika Bandari ya Tartus ya Syria katika pwani ya Bahari ya Mediterranea.

Alexander Yuldashev, Kamanda wa mazoezi hayo ya pamoja ametangaza kuwa: "Wanajeshi wa Russia na Syria wamefanya mazeozi ya pamoja katika Bandari ya Tartus kwa lengo la kuimarisha uwezo wa kulinda harakati za kimataifa za kiuchumi baharini.

Yuldashev ameongeza kuwa, zaidi ya askari 2000 na meli saba za kivita zilishiriki katika mazoezi hayo ya kijeshi yaliyofanyika kuanzia Januari 18-20.

Wanajeshi wa majini wa Russia na Syria mwezi uliopita wa Disemba pia walifanya mazoezi ya pamoja katika kituo cha kijeshi cha Bandari ya Tartus.

Mji wa Tartus una bandari ya pili kwa ukubwa Syria baada ya mji wa Latakia katika pwani ya Bahari ya Medietrennea ya nchi hiyo ya Kiarabu.

Russia ina kituo cha jeshi lake la majini katika Bandari ya Tartus. Mkataba wa kituo hicho ulitiwa saini baina ya Russia na Syria mwaka 2017 na kwa mujibu wa mkataba huo, Russia itatumia kituo hicho kwa muda wa miaka 49.

4bv523c59f651f1kyw0_800C450.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kheri kuwa mjinga kuliko kuwa mpumbavu, unakimbia mto wenye mamba unakimbilia bwawa lenye viboko 😝😝
 
Tatizo Putin naye mnafiki. Wakimaliza mazoezi anamwita Netanyahu Moscow na kumpa michongo yote including weaknesses za hao jamaa.
 
Back
Top Bottom