Mazoezi magumu zaidi ya majeshi ya nchi tofauti duniani

Mazoezi ya kijeshi yote hufanana takribani yote, ila inategemea na nchi. Mfano, kuna nchi zenye barafu na zisizo na barafu, nchi za joto kali na baridi kali, zajangwa na zisizo na jangwa.

Ndiyo maana huwa wanashirikiana majeshi ya nchi tofauti kupeana uzoefu.

Hata kama wanalipwa kiasi kidogo, ukishajitoa kuitumikia nchi yako na watu wake, siku zote suala la malipo haliangaliwi sana, yaani UZALENDO kwanza.

Majeshi yetu Afrika, yapo vizuri pia, sema tu vifaa bado siyo vya kisasa kama mnavyowaona wa mbele huko. Mf, tazama wanajeshi wa jirani zetu Sudan Kusini, na Congo, huwa nawaona wakiwa na zana hafifu sana, mfano mdogo tu Buti zao, yaani wanavaa zile za mvua, ambazo ww na mimi tunazivaa (baadhi, na tunawaona Osteri Malivika, wa ITV, anayeripoti tokea huko).

Sasa viatu kama vile, hata kukimbia umbali mrefu ni shida. Kama unaye ndugu yako aliyeenda kulinda amani huko, muulize akuchambulie ya huko.

Ahsante!
Wanajeshi wa Kibongo wapo vizuri sana ndio maana unaambiwa kama uliwahi kufanyiwa Operation yoyote kwenye mwili usijaribu kuingia jeshini maana itafumuka,hapo ndipo utajua wabongo noma kwenye Jeshi,ukitaka kujua jeshi letu lipo au laah kamuulize Iddi Amin anaijua shughuli yetu.
 
Mazoezii mengi..
Suicide boomer mmoja tuu..mwenyekujua wapi ajilipue anatosha
 
ISS ndio kiboko cha wote. pass out lazima uchinje mtu live !! ukishindwa hapo wanakuchinja na mchezo umeisha
 
Yaani yote hii ni kutaka kuwa mahiri kwenye kuua watu. Yaani ili nchi ijione iko salama basi inapasa kuwa na uwezo mkubwa wa kuua watu! Ama kwa wanajeshi wako au mabomu, vifaru, ndege n.k..... Bwana utuhurumie
Ndo maana ake....au ufe wewe...je wewe unakubali kuuliwa??..
 
Back
Top Bottom