Mazoezi magumu zaidi ya majeshi ya nchi tofauti duniani

  • Thread starter kisu cha ngariba
  • Start date

kisu cha ngariba

kisu cha ngariba

JF-Expert Member
Joined
Jun 21, 2016
Messages
22,201
Likes
47,981
Points
280
kisu cha ngariba

kisu cha ngariba

JF-Expert Member
Joined Jun 21, 2016
22,201 47,981 280
Mazoezi kwa wanajeshi ni kitu cha muhimu sana. Majeshi duniani huhakikisha kuwa wanawafunza wanajeshi wao mafunzo ya kuikakamavu kuweza kuwajenga kimwili na kiakili ili kuweza kupambana na hali tofauti tofauti wanazokumbana nazo wakiwa vitani au katika mazingira mengine.

Hizi hapa ni picha za majeshi tofauti tofauti duniani zikionyesha mazoezi magumu ambayo huwa wanfanya.
d26a71a3ed8fe921056bed64d43b600d.jpg

Wanajeshi wa China wakifanya mazoezi kwenye matope.
a4dd2e343e51e867805e2a00c732b3ce.jpg

Mwanajeshi wa China akitambaa chini ya nyaya zinazowa waka moto wakati wa mazoezi.
4ac4eb541f2908207779c044500c7d65.jpg

Baada ya kutambaa na kufanya mazoezi kwenye moto, sasa wanafanya mazoezi ya viungo.
3b6e6267459487121dd507eb725683db.jpg

Mazoezi wakati mwingine huwa ni adhabu kwa wanajeshi. Hapa wanajeshi wa China wakitakiwa kubana pumzi na kuweka uso ndani ya maji.
eefaf722359032997aaf6f0d46ad8d04.jpg

Wanajeshi wa China wakifanya mazoezi yao kwenye barafu. Maeneo haya yana baridi ya hali ya juu.
fb2deb9525e6a13852c933d9646e7ca6.jpg

Wanajeshi wa kitengo maalum cha kivita nchini Korea ya Kusini wakifanya mazoezi yao kwenye barafu.
fc68de10b88d764bb6b2ae85ba08209f.jpg

Mwanajeshi wa nchini Canada akifanya mazoezi katika maji yenye barafu ikiwa ni mazoezi ya NATO.
7b0172a37593b886eea1a9c58ede34c5.jpg

Wanajeshi wa majini wa Marekani pamoja na Korea Kusini wakifanya mazoezi pamoja katika milima nchini Korea Kusini.
05a6cee0a5b9c424104fcc3041ee2ee5.jpg

Wanajeshi wa Marekani wakiwa mazoezi Thailand. Katika kujifunza namna ya kushi katika hali ngumu, wanajeshi hao hulazimika kunywa damu ya Chatu.
b92385f48332f42f98dad8f2dbf0140a.jpg

Mwanajeshi wa Marekani wakiwa mazoezini ambapo anaruka kutoka kwenye helikopta akiwa na mbwa anayemfanyia mazoezi.
ad7dd9732348ff6248b2026bd764ece4.jpg

Wanajeshi nchini Japan wakifanya mazoezi ya kuning’ia kwenye helikopta kwa kutumia kamba.
c4c18bc56f8040ddeb8bd931fda02f0a.jpg

Ili mwanajeshi ahitimishe mafunzo ya wiki tisa nchini Taiwan, unatakiwa kutembea umbali wa futi 150 juu ya mawe na miamba.
39621f4ad36d5c68e78f001dc559525b.jpg

Belarus, ili uweze kuwa mmoja wa kundi la Red Berets, unatakiwa kupita kwenye vikwazo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupita juu ya bomba kwa kutembea.
614ac43836f5e804fa009610da0c9388.jpg

Mmoja wa wanakundi wa Red Berets akiwa amefukiza kichwa chake ndani ya matofali yenye moto ikiwa ni sehemu ya maonyesho ya kundi hilo kila mwaka.
c467e15c310037eab4975134f5bb8289.jpg

Mazoezi ya uvumilivu ni muhimu sana, wanajeshi wa Israel kila mmoja analazimika kutembea umbali wa maili 43 (69 km) ikiwa ni sehemu ya mazoezi.
e1f81b457891004968399176a2876430.jpg

Wanajeshi wa Palestina wakifanya mazoezi ya kuruka angani.
7ae2f3d2e46e1b7bf3e36ef7628685e5.jpg

Kundi la Kurdish YPG nchini Syria likifanya mazoezi katika viunzi vyenye moto
e3cea767ebcbb22374c74bc0d3ef9205.jpg

Wanajeshi wa Kishia nchini Iraq wakifanya maonyesho ya mazoezi yao wakati wa mahafali yao.
b50853fe79b36caa76df5960794c8cdb.jpg

Wanajeshi wengine wa Kishia nchini Iraq ili kuweza kuhitimu mafunzo yao wanalazimika kutambaa kwenye mchanga/udongo jangwani.

Asante.
 
Ochumeraa

Ochumeraa

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2015
Messages
1,622
Likes
1,299
Points
280
Ochumeraa

Ochumeraa

JF-Expert Member
Joined May 18, 2015
1,622 1,299 280
Mbona hujaweka ya tanzania
 
Jane Lowassa

Jane Lowassa

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2016
Messages
1,449
Likes
1,647
Points
280
Jane Lowassa

Jane Lowassa

JF-Expert Member
Joined May 10, 2016
1,449 1,647 280
Mhhhh
 
Fekifeki

Fekifeki

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2011
Messages
1,207
Likes
191
Points
160
Fekifeki

Fekifeki

JF-Expert Member
Joined Nov 18, 2011
1,207 191 160
Tuwekee na ya Kibongo mkuu
 
bakari bakari 1

bakari bakari 1

Senior Member
Joined
Jul 7, 2015
Messages
172
Likes
30
Points
45
bakari bakari 1

bakari bakari 1

Senior Member
Joined Jul 7, 2015
172 30 45
Hayo mbona kawaida sana bongo noma bana
 
Kitang'wa1

Kitang'wa1

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2014
Messages
460
Likes
202
Points
60
Kitang'wa1

Kitang'wa1

JF-Expert Member
Joined Dec 4, 2014
460 202 60
Mazoezi ya kijeshi yote hufanana takribani yote, ila inategemea na nchi. Mfano, kuna nchi zenye barafu na zisizo na barafu, nchi za joto kali na baridi kali, zajangwa na zisizo na jangwa.

Ndiyo maana huwa wanashirikiana majeshi ya nchi tofauti kupeana uzoefu.

Hata kama wanalipwa kiasi kidogo, ukishajitoa kuitumikia nchi yako na watu wake, siku zote suala la malipo haliangaliwi sana, yaani UZALENDO kwanza.

Majeshi yetu Afrika, yapo vizuri pia, sema tu vifaa bado siyo vya kisasa kama mnavyowaona wa mbele huko. Mf, tazama wanajeshi wa jirani zetu Sudan Kusini, na Congo, huwa nawaona wakiwa na zana hafifu sana, mfano mdogo tu Buti zao, yaani wanavaa zile za mvua, ambazo ww na mimi tunazivaa (baadhi, na tunawaona Osteri Malivika, wa ITV, anayeripoti tokea huko).

Sasa viatu kama vile, hata kukimbia umbali mrefu ni shida. Kama unaye ndugu yako aliyeenda kulinda amani huko, muulize akuchambulie ya huko.

Ahsante!
 
Kitang'wa1

Kitang'wa1

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2014
Messages
460
Likes
202
Points
60
Kitang'wa1

Kitang'wa1

JF-Expert Member
Joined Dec 4, 2014
460 202 60
Na ndiyo maana nchi zote kubwa kubwa, unazozijua wewe, wanawekeza zaidi kwenye majeshi, yaani bajeti ya majeshi huwa inakuwa kubwa kidogo - hapa nazungumzia lile jeshi la vita, na siyo majeshi mengine.

Vifaa na zana za kivita ni gharama mno, na hata mafunzo hayo ni gharama mno.

Afrika, pia tunaweza kuyafanya makubwa tu kwenye majeshi yetu, sema wanasiasa wanatuangusha.

Ahsante!
 
Shida na raha

Shida na raha

JF-Expert Member
Joined
Aug 8, 2014
Messages
3,783
Likes
3,288
Points
280
Shida na raha

Shida na raha

JF-Expert Member
Joined Aug 8, 2014
3,783 3,288 280
Hatuchambui kitu hapa.
 
GRAPHIX MASTER

GRAPHIX MASTER

Senior Member
Joined
May 22, 2015
Messages
166
Likes
54
Points
45
GRAPHIX MASTER

GRAPHIX MASTER

Senior Member
Joined May 22, 2015
166 54 45
Katika mazoezi yote zoezi lililonitisha ni hilo la kuburuzika kwenye mawe ukiwa kifua wazi
 

Forum statistics

Threads 1,236,848
Members 475,301
Posts 29,269,667