Maziwa ya S-26 yapigwa Marufuku Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maziwa ya S-26 yapigwa Marufuku Tanzania

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Invisible, Aug 26, 2009.

 1. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #1
  Aug 26, 2009
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 235
  Trophy Points: 160
  Fake S-26 Breast Milk Substitute invades East Africa

  [​IMG]

  Fake S-26 Breast Milk Substitute has been spotted being sold in East African supermarkets and shops. S-26 which is the most popular BMS among other brands has been faked.

  According to a nearly two-month survey, the fake powdered milk is sold in containers of different quantities and buyers hardly recognize that the product in question is counterfeit. Interviewed parents, both males and females were extremely shocked when asked whether they were aware of the existence of fake S-26. Without responding to the question they hurried home to check whether they are victims of the illegal business.

  Those who turned back said it was true that some of the containers they had bought were real fake. Speechless as they were angered and full of frustrations they blamed the government, authorities concerned, manufacturers, importers, wholesalers, and retailers for that anomaly.

  " I wonder what the authorities concerned are doing. I have been feeding my three month old toddler this good for nothing milk without knowing that it's fake. I now know the reason he is not gaining weight," lamented one parent who asked for anonymity.

  A score of parents who have fallen in that trap have exclusively said that their babies were not only underweight but do not also grow as they should.

  Paediatricians say there are serious effects when a baby and especially an infant takes inappropriate foods.

  They do not grow properly and they risk vomiting, diarrhoea, being under weight, among other complications.

  BTW: Nasikia serikali ya Tanzania imeyapiga marufuku maziwa haya Tanzania!
   
 2. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #2
  Aug 26, 2009
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 235
  Trophy Points: 160
  Well, nimeipata habari yenyewe:

  Maziwa haya ni hatari...!


  Na Sharon Sauwa

  [​IMG]

  Maziwa maarufu ya watoto Jijini na ambayo hutengenezwa nchini Afrika Kusini aina ya S-26.

  Maziwa maarufu ya watoto Jijini na ambayo hutengenezwa nchini Afrika Kusini aina ya S-26, yamebainika kuwa na madini hatari na hivyo kuanzia sasa yamepigwa marufuku nchini.

  Taarifa rasmi iliyotolewa leo na Serikali kupitia Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA), imetangaza hatua ya kupiga marufuku uagizaji, usambazaji na uuzaji wa maziwa hayo aina ya S-26, ambayo hutengezwa na kusambazwa na Kampuni ya Pharmacare Limited ya nchini Afrika Kusini.

  Taarifa hiyo inayoonesha kutolewa na Mkurugenzi wa TFDA, Bi. Magreth Ndomondo, imeeleza kuwa hatua ya kuyapiga marufuku maziwa hayo (ambayo ni maarufu Jijini) imechukuliwa baada ya kuthibitika kuwa yana madhara kwa binadamu.

  Aidha, wafanyabiashara wote wa maziwa hayo wameagizwa kutoa taarifa za kiasi cha maziwa hayo walichonacho katika ofizi za mamlaka hiyo na halmashauri ili yaweze kuondolewa sokoni.

  Aidha, taarifa hiyo imetoa onyo kuwa mfanyabiashara yeyote atakayeshindwa kutekeleza maagizo hayo atachukuliwa hatua kali za kisheria.

  “Kwa taarifa hii, TFDA inapiga marufuku uagizaji, usambazaji na uuzaji wa maziwa ya watoto wachanga aina ya S-26 yanayotengenezwa na kusambazwa na Kampuni ya Pharmacare Ltd ya Afrika Kusini hadi mtengenezaji atapokidhi matakwa ya sheria,”akasema.

  Aidha, katika taarifa hiyo, Mkurugenzi wa TFDA, amesema mamlaka yake iliamua kuyafanyia uchunguzi maziwa hayo baada ya kupata taarifa ya kuwepo kwa maziwa ya watoto ya S-26 katika soko la nchini yanayotiliwa shaka.

  Akasema taarifa hizo zilieleza kuwa watoto waliotumia maziwa hayo walipiga chafya, kupata maumivu ya tumbo na kutapika.

  Pia ilielezwa hapo kabla kuwa maziwa hayo hayayeyuki vizuri katika maji na yana harufu mbaya kama mafuta ya kula yaliyoharibika.

  Akasema kuwa baada ya kupokea taarifa hiyo, walifanya ukaguzi katika maduka na maghala ya vyakula ikiwa ni pamoja na yale yanayotuhumiwa kuwa na maziwa hayo.

  Akasema katika ukaguzi huo, jumla ya makopo 38,560 ya S-26 yenye madini ya chuma ya ujazo wa gramu 400 kwa kila kopo, ambayo yametengenezwa na kampuni ya Pharmacare Ltd, Woodmead-Sandton yalikutwa sokoni na sampuli zake kuchukuliwa kwa uchunguzi zaidi.

  Mkurugenzi huyo akasema uchunguzi wao huo ulibaini kuwepo kwa kiwango kikubwa cha tindikali huru za mafuta (free fatty acids) na kemikali aina ya peroxide, hali ambayo inaashiria kuharibika kwa mafuta yaliyomo katika maziwa hayo na hivyo kutofaa kwa matumizi ya binadamu.

  “Wananchi wanatahadharishwa kutotumia maziwa hayo na kutoa taarifa watakapobaini kuwepo kwa maziwa hayo sokoni," ikasema sehemu ya taarifa hiyo ya Mkurugenzi wa TFDA.

  Aidha, ikasisitiza kuwa taarifa za kuendelea kuuzwa kwa maziwa hayo ambayo yamejaa tele Dar es Salaam, zitolewe katika ofisi za TFDA Makao Makuu au kanda na ofisi za afya za Mikoa na halmashauri ili hatua zaidi za kisheria ziweze kuchukuliwa.


  Chanzo: ALASIRI
   
 3. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #3
  Aug 27, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Je wanaishia kupiga marufuku au hata kuhakikisha yanaondolewa kabisa katika soko kwani sio wote wanaosoma magazeti au kuangalia TV.

  Suali ni vp yaliingia tanzania na kupenya mpaka sokoni,? vp madhara watakayoyapata wale waliokwisha tumia? Je kuna utaratibu gani huko tanzania mara mizigo kama hii inapoingia?

  Nina masuala mengi sana.
   
 4. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #4
  Aug 27, 2009
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Ingekuwa bora wangetoa pia maelekezo kwa wauzaji na wasambazaji. Issue ya kuteketeza stock iliyopo n.k. Halafu hawa wauzaji ni wadau muhimu sana na wanawajibika kuweka input yao kuwahabarisha wateja ili afya ya mlaji isidhurike.

  Napendekeza katika hali kama hii, iwe ni sheria kwa wauzaji kuweka tangazo mlangoni kuhusu tahadhari hii. Iwe rahisi pia kwa wateja kuwatambua wauzaji wasio na taarifa hizi. Hapa itatoa fursa kwa mteja kumhabarisha muuzaji asiye na taarifa.

  Hii habari ya "taarifa zitolewe kwa atakayeendelea kuuza" is not very effective in my opinion.
   
 5. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #5
  Aug 27, 2009
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  ....atakayekaidi kuweka bandiko kwenye mlango/ukuta wa dula lake, huyo ni dhahiri atakuwa ni kati ya watu wachache ambao wako tayari kudhuru afya ya mlaji.
  Hapa ndipo kipande cha "taarifa zitolewe" kinapoweza kuwa effective.
   
 6. N

  Ndele Member

  #6
  Aug 28, 2009
  Joined: Dec 27, 2008
  Messages: 82
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Nimempatia mtoto wangu zaidi ya miezi minne sasa! na kila siku analia kama vile tumbo linauma na kupiga chafya! sasa sijui mnanishauri nitumie maziwa gani badala ya haya kwani mtoto kwa kipindi cha mchana anatumia maziwa hayo mpaka mama yake arudi toka kazini ndo ananyonya kwa mama yake! lakini ukipiga mahesabu ni karibia asilia 60 anatumia maziwa hayo na asilimia inayobaki ni kutoka kwa mama je nitumie maziwa gani badala yake?
   
 7. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #7
  Aug 29, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA), imepiga marufuku matumizi ya maziwa ya watoto wachanga yajulikanayo kama S26 yanayotengenezwa Afrika Kusini baada ya kubainika yana madhara kwa watoto.

  Kwa mujibu wa taarifa ya Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Margareth Ndomondo, walipokea taarifa kwa nyakati tofauti ya kuwepo katika soko maziwa hayo ambayo yamesababisha madhara kwa watoto wachanga na kuamua kufanya ukaguzi katika maduka na maghala ya vyakula ili kubaini ukweli wake.

  Alisema taarifa hizo zilieleza kuwa watoto waliotumia maziwa hayo yanayotengenezwa Afrika Kusini, walipiga chafya, kupata maumivu ya tumbo, kutapika na wengine kuharisha.

  Pia alisema taarifa nyingine zilidai kuwa maziwa hayo hayayeyuki vizuri katika maji na yana harufu mbaya kama mafuta ya kula yaliyoharibika ambapo kutokana na ukaguzi, taarifa hizo zilikuwa za kweli.

  “Katika ukaguzi huo, jumla ya makopo 38,560 ya S26 yenye madini ya chuma ya ujazo wa gramu 400 kwa kila kopo yaliyotengenezwa na kampuni ya Pharmacare Ltd, Woodmead-Sandton yalikutwa sokoni na sampuli zake kuchukuliwa kwa uchunguzi zaidi,” alisema Ndomondo.

  Alisema uchunguzi wa kimaabara ulibaini kuwepo kwa kiwango kikubwa cha tindikali huru za mafuta (free fatty acids) na kemikali aina ya peroxide, hali ambayo inaashiria kuharibika kwa mafuta yaliyomo katika maziwa hayo na hivyo kutofaa kwa matumizi ya binadamu.

  Taarifa hiyo ilisema kutokana na matokeo ya uchunguzi huo, mamlaka hiyo imezuia matumizi ya maziwa hayo ya S26 kutoka Afrika Kusini na inawataka wananchi kutoyatumia na endapo watabaini kuwepo kwa maziwa hayo madukani, watoe taarifa kwa mamlaka makao makuu au katika ofisi za kanda na ofisi za afya za mikoa na halmashauri ili hatua zichukuliwe.
  http://www.darhotwire.com/home/news/2009/08/27/maziwa_ya_s26_marufukuuu.html
   
 8. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #8
  Aug 29, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  nchi imeoza hiiiii,,,,,,,,,,,,,mpaka watu wadhurike ndo hatua zichukuliwe,,,,
   
 9. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #9
  Aug 29, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Leo nilikuta muuza duka mmoja anafoka sana baada ya mteja mmoja kumstua mwingine aliyetaka kununua S26 No.2. Hii ni hatari kwani hawa jamaa wa TFDA walitakuwa kutoa amri maziwa yote yaliyoko madukani yeteketezwe!
   
Loading...