Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,495
- 9,275
Maziwa ya ng’ombe ni mojawapo ya chakula kilicho na virutubisho vingi vinavyofaa kwa afya ya binadamu. Pamoja na ubora wake huu, aina hii ya maziwa haifai kwa mtoto mwenye umri chini ya mwaka mmoja kutokana na sababu kuu tatu.
Moja, huwa na kiasi kidogo sana cha madini ya chuma ambayo hayawezi kukidhi mahitaji ya mtoto ambaye hukua kwa kasi wakati huo, hivyo kuyategemea sana kunaweza kusababisha mtoto apatwe na changamoto ya upungufu mara kwa mara wa damu.
Pili, miongozo mbalimbali ya WHO , CDC pamoja na utafiti maarufu sana wa Ekhard E Ziegler et al (2007) vinaelezea kuwa wastani wa asilimia 40 ya watoto chini ya mwaka mmoja wanaopatiwa maziwa ya ng’ombe hupatwa na tatizo la kuvujia kwa damu kwenye utumbo hivyo kuwafanya wapoteze damu nyingi kupitia choo.
Tatu, huwa na kiasi kikubwa sana cha protini pamoja na madini ambavyo kwa umri wake huwa ni ngumu sana kuvitunza mwilini. Kiasi cha ziada hupaswa kutolewa kupitia mkojo, hivyo ni lazima mwili wa mtoto upoteze pia maji mengi katika kutoa nje uchafu huu. Kuna taarifa za uhakika kuwa watoto wanaopatiwa maziwa ya ng’ombe kwenye umri huu hukabiliwa mara kwa mara na tatizo la upungufu mkubwa wa maji mwilini.
Maziwa haya ni mazuri kwa afya. Yanapaswa kutolewa kwa mtoto baada ya kufikia mwaka mmoja na siyo chini ya hapo.
Chanzo: AfyaInfo