Maziwa/uji kwa mtoto | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maziwa/uji kwa mtoto

Discussion in 'JF Doctor' started by Bizzly, Aug 9, 2010.

 1. B

  Bizzly Member

  #1
  Aug 9, 2010
  Joined: May 3, 2010
  Messages: 70
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  Wana JF ni umri gani hasa unafaa kumwanzishia mtoto mdogo uji au maziwa? na kipi kinashauriwa kuanza kati ya uji au maziwa. wa kwangu ana miezi 2. naomba ushauri wenu wa kitaalam.
   
 2. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #2
  Aug 9, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Uji subiri mpaka afikishe atleast miezi 6......Maziwa ya ng'ombe usimpe chini ya mwaka mmoja!Protein..potassium na sodium inayopatikana kwenye maziwa ya ng'ombe ni nyingi sana kwa miili yao!!!
   
 3. kisasangwe

  kisasangwe JF-Expert Member

  #3
  Aug 10, 2010
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 294
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  kama mama anamnyonyesha wakati wote( mchana pia kama haendi popote) basi hadi miezi sita uji, maziwa awezapewa kama ya mama hayamtoshi.ya n'omb einabid yawe yameondolewa kwa kiasi yale mafuta, (yachemshwe yaachwe yapoe kisha ondoa ile cream inayokua juu) then apewe kidogokidogo.

  kama mama ni wa kutoka kwenda job. akifika miezi 3 waeza mpa uji kijiko kimoja cha chakula kila siku ili azoee taratibu. plus maziwa. then miezi minne unampa ndizi.(ni vema ikachemshwa bila kumenywa hadi iive then unaimenya na kumpondea mtoto kiasi kidogo kwa kutumia supu ya samaki au nyama au pia maji ya moto.)
   
 4. P

  Paul S.S Verified User

  #4
  Aug 10, 2010
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  wangu anamiezi 7 nimemuanzishia maziwa ya ngombe wiki sasa inakaribia. tatizo anapata choo kigumu na kwa tabu sana, nimeambiwa nichanganye na maji maziwa.
  kuna mwenye ufahamu tafadhali
   
 5. B

  Bizzly Member

  #5
  Aug 10, 2010
  Joined: May 3, 2010
  Messages: 70
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  asante mdau, je huo uji ni unga wa mahindi, ulezi au kuna unga special kwa jili ya watoto wachanga?
   
 6. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #6
  Aug 10, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Wa mahindi tu (hasa yale yaliyokobolewa) hauna virutubisho kwahiyo haumfai mtoto mchanga:
   
 7. Mom

  Mom JF-Expert Member

  #7
  Aug 10, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 708
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  ni vizuri usimpe mtoto chochote katika umri wa miezi6 ya mwanzo.
  lakini kama mama ni mtu wa kazi, unaweza kuanza maziwa akiwa na umri wa miezi 3 kuna special formulars za watoto lakini siziamini sana. wa kuanzia unashauriwa kuchanganya maziwa na maji lets say 2/3 maziwa na 1/3 maji yachemshwe vya kutosha. uji aanze akiwa na umri wa miezi6 na mwanzoni unachuja ili kupata uji laini kabisa na unampa mara1 kwa siku na kuangalia tumbo litareact vipi. Then akishazoea lets say mwezi1 unaanza kumpa uji wa lishe kwa kuchanganya vitu vichache mpaka azoee
   
 8. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #8
  Aug 10, 2010
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,342
  Trophy Points: 280
  FYI, maziwa ya mama na ya ng'ombe yanatofautiana kwa quality na some ingredients. Maziwa ya n'gombe yawe diluted kama alivyoshauri mmoja hapo juu. usimpe ya n'gombe peke yake bila dilution. Katika miezi 7 mwanzishie vyakula laini kama viazi mviringo vilivyochanganywa na mchuzi wa samaki au nyama. Pia mpe papai litalainisha choo. Maji safi ya kunywa mara kwa mara hasa wakati wa joto ni muhimu, wengi tunadhani watoto hawasikii kiu! si kweli
   
 9. MNDEE

  MNDEE JF-Expert Member

  #9
  Aug 11, 2010
  Joined: Jul 10, 2009
  Messages: 494
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  Naungana na waliotangulia, ushauri wa madaktari mtoto apewe maziwa ya mama au yale special kwa watoto (kopo) hadi atimize miezi sita. Utakapomwanzishia vyakula uende taratibu, anza mara moja kwa siku kiduchu na nyakati nyingine maziwa. Epuka chumvi, sukari, mafuta, maji/juicy zisizo salama.

  The longer you wait to introduce people's food the better, vile vile chagua vyakula ambavyo vitajenga mwili, mfano badala ya uji wa ugali au ulezi, why not njegele kidogo, karoti, na kiazi mviringo robo chemsha ponda/blend changanya na maziwa uwe laini mjaribishe mtoto.
   
Loading...