Maziwa kulala na kuwa makubwa kwa wamama waliozaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maziwa kulala na kuwa makubwa kwa wamama waliozaa

Discussion in 'JF Doctor' started by Billie, Oct 11, 2011.

 1. Billie

  Billie JF-Expert Member

  #1
  Oct 11, 2011
  Joined: Aug 13, 2011
  Messages: 5,326
  Likes Received: 2,322
  Trophy Points: 280
  Ngoja nianze na swali."Kwa nini wasichana wengi wa nchi zinazoendelea wanapoteza 'shape' zao na hata zile za maziwa(breasts) kulala au kuwa makubwa na hata kushindwa kurudia shape yake ya awali kama ilivyo kwa wamama wa nchi endelevu'?
  Naomba nisaidiwe nini kinachosababisha ili nimuambie mke wng tuiepuke coz anakachanga changu na kama kuna namna au dawa au chochote kitachorudisha shape nzuri ya maziwa yake ya awali.NITAFURAHI SANA KUPOKEA USHAURI KUTOKA KWA WATAALAM KUTOKA HUMU sio ushauri wa kizushi.
   
 2. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #2
  Oct 11, 2011
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Kukua kwa matiti kunachangiwa sana na hormones za mwanamke, ambapo level ya hormones hizo inatofautiana kati ya mwanamke na mwanamke, au wanawake wa eneo fulani na eneo jingine, au wanawake wa race moja na nyingine. Matiti hufikia kilele (peak ) chake cha kukua pale mwanamke anapojifungua na kunyonyehsa. Breast tissue huwa inaongezekwa kiasi kikubwa ili kuweza kuzalisha maziwa ya kutosha kwa mtoto, pia kunakuwa na mwongezeka wa damu kwenye titi ili kupeleka virutubisho vya kutengeneza hayo maziwa, kwa hiyo titi linajaa. Lakini anapoacha kunyonyesha (maziwa yanapoisha) breast tissue inasinyaa na msukumo wa damu unapungua hivyo yanalala mpaka uzao mwingine.

  Lakini kama nilivyosema awali, wingi na effect za hormones hizi kwa matiti unatofautiana kati ya mwanamke na mwanamke, kwa hiyo wengine matiti yao yanaathirika sana, na wengine kidogo na wengine hayaathiriki kabisa.
   
 3. Billie

  Billie JF-Expert Member

  #3
  Oct 11, 2011
  Joined: Aug 13, 2011
  Messages: 5,326
  Likes Received: 2,322
  Trophy Points: 280
  Asante sana doctor ila naomba uniraidie ni namna gani naweza tukayarudisha katika hali ya awali na je kuna dawa au jinsi yeyote inayoweza kutumika ku recover matiti mazuri aliyokuwa nayo.
  Kingine ni kuwa kwa nini hili tatizo halionekani nchi zilizoendelea kama U.S.A na kwingineko.JE WANATUMIA NINI?
   
 4. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #4
  Oct 11, 2011
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135

  .......Kama una pesa mfanyie mkeo breast implants baada ya kunyonyesha, Ulaya/USA wanawake walio wengi kwanza hawanyonyeshi watoto.
  Na hao wachache wanaonyonyesha wanazaa idadi ya watoto wanaotaka baada ya kumaliza uzazi wanafanya breast implants. Upo hapoooooo!!!!
   
 5. Billie

  Billie JF-Expert Member

  #5
  Oct 11, 2011
  Joined: Aug 13, 2011
  Messages: 5,326
  Likes Received: 2,322
  Trophy Points: 280
  asante kwa ushauri ila inafanywa namna gani na je haiatarishi afya ya mama?
   
 6. v

  valid statement JF-Expert Member

  #6
  Oct 12, 2011
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 2,737
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  Lakini kuna wanawake wamebarikiwaaa!
  Kazaa watoto wanne, lakini ukicheki TWIN TOWERS, zimesimama kuliko za BOT, Ukirudi shepu ndo kwaaaanza utadhani hajawahi hata beba mimba.
   
 7. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #7
  Oct 12, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  tHANKS

  Pia tukumbike kuna maumbile (could be hormones) where wengine wana nyama laini kiasi kwamba hata small breasts bado zinaweza kuanguka, na pia kuna firm tissues (nyama) ambapo wengine wanakua firmer
   
 8. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #8
  Oct 12, 2011
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Mfumo wa hormone wa mwanamke (na hata wanaume) na pia maumbile huwa yanakuwa tofauti genetically, hivyo ukaona wengine matiti yao yako vile vile, na wengine wakrespond kwa matiti yao kuharibika....Manshivo, I am afraid hakuna dawa ambayo unaweza kumeza ili kurudisha matiti kama yalivyokuwa kabla ya mimba na kunyonyesha.

  Unaweza kufanya upasuaji (cosmetic surgery) kuweka implants kama alivyoshauri Pretty...lakini hii procedure inavyofanywa ni kuwa breast tissue yote inatolewa kisha wanaireplace na silicon implants na unachagua mwenyewe how big you want the boobs to be and what shape you like. Kwa kuwa breast tissue yote inakuwa removed, huyo dada hataweza tena kunyonyesha katika maisha yake yote...so kama mnaplan kuzaa tena atleast hold it mpkaka mtakapoamua sasa watoto wanatosha ndio mfanye!
   
 9. Billie

  Billie JF-Expert Member

  #9
  Oct 12, 2011
  Joined: Aug 13, 2011
  Messages: 5,326
  Likes Received: 2,322
  Trophy Points: 280
  Naipenda jf kwa sababu ya majibu matamu kama haya.ASANTE KWA MARA YA PILI Dr.riwa
   
 10. fxb

  fxb Senior Member

  #10
  Oct 12, 2011
  Joined: Jun 22, 2011
  Messages: 124
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Pamoja na majibu mazuri naomba nishauri kuwa kumyonyesha mtoto kwa mfululizo siyo tu ni neema kwa mtoto bali hufanya maumbile ya mama yasibadilike kiivyo (Mama hakikisha mtoto ananyonya maziwa ya mama acha maji akiwa na kwikwi sijui nini nyonyesha tu). kwa kuwa Riwa amehasema vizuri chakula kilivyotengenezwa kikitumika chote hakifanyi tissues kukuwa zaidi ya matumizi.
   
 11. N

  Nsagali Member

  #11
  Oct 12, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 90
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  asante doctor
   
 12. Leonard Robert

  Leonard Robert JF-Expert Member

  #12
  Oct 12, 2011
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 9,143
  Likes Received: 2,465
  Trophy Points: 280
  dr.maelezo yako huwa ninayaelewa haraka.asanteh.
   
 13. Billie

  Billie JF-Expert Member

  #13
  Oct 12, 2011
  Joined: Aug 13, 2011
  Messages: 5,326
  Likes Received: 2,322
  Trophy Points: 280
  Thanx wote
   
Loading...