Maziwa Fresh yasiyochemshwa yana madhara?

Royal Son

JF-Expert Member
Dec 22, 2016
587
973
Habari wakubwa,

Naomba kuuliza hivi ukinywa maziwa fresh yasiyochemshwa kuna faida au madhara yoyote wakuu sababu nayapenda sana maziwa mabichi.
 
Habari wakubwa naomba kuuliza hivi ukinywa maziwa fresh yasiochemshwa kuna faida au madhara yoyote wakuu sababu nayapenda sana maziwa mabichi
Yeah, madhara yapo. Weupe wa maziwa usikufanye ukahisi yap salama hivyo. Yanaweza yawe safi lakini si salama, hapa nazungumzia huwepo wa vimelea vya magonjwa, kama bacteria, virus kwa jamii yake.

Kuanzia uvunaji wa maziwa, uhifadhi na hata wavunaji wenyewe huweza kuleta vimelea humo.
Hapa sija zungumzia magonjw na vimelea vinavya bebwa na ngombe mwenyewe kutoka katika chakula, maladhi, magonjwa n. K

Kuna mengi kidgo, humu. Lakini ukiya chemsha hakuna mengi ya kupoteza
 
Kwa mujibu wa huyu dogo hakuna tatizo.
 
madhara yapo mkuu ikama kupata kifua kikuu maana vimelea vya tb vinaweza patikana ata katik maziwa kama ngombe anaumwa tb,pia kuhara kwa sababu maziwa huvutia bacteria wengi kuish ndani yake..xo sio poa kunywa bila kuchemxha ata kiasi maana bacteria wengi hufa kwa joto la kawaida
 
Mh! Wengine kumbe tumekua kwa neema tu.
Maziwa yanakamuliwa kwenye kipeyu bado yanatoatoa moshi unakandamiza huku upo kifua wazi.
 
Dunia sasa imekumbwa na madaliko ya hali ya hewa.Nakumbuka zamani sisi wa vijijini tulikuwa tunakunywa tuu mda mwengine yakichemshwa sa yasipo chemshwa heri zaidi..
Mleta mada usipo chemsha maziwa kuna uwezekano mkubwa yakawa na madhara...Chemsha maziwa kwa afya yako.
 
pale kigoma kwa bela sheli kuna madogo wanauza yaliyoshachemshwa ni mwendo wa kugigida tu.
 
Upo uwezekano wa kupata magonjwa hatari, kuna TB ya ng'ombe inaweza kumpata Mtu akitumia maziwa yasiyochemshwa.

Huku Kaskazini maziwa yanayogandishwa kienyeji hawachemshi, ila kutahadharishwa ni jambo moja na kuchukua tahadhari ni jambo lingine.

Aliyekaa maabara na kuja huo utafiti ni Mzungu, kwa sisi Wamatumbi Bibi atakwambia tunakunywa tangu utotoni na tunaishi...kazi inabaki kwako kuwasikiliza 'Wazungu' uogope kunywa maziwa mabichi au umsikilize Bibi upige maziwa.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom