Mazito yaibuka kesi ya Lissu, walalamikaji waadhibiwa mahakamani, Chiligati na Mrema watajwa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mazito yaibuka kesi ya Lissu, walalamikaji waadhibiwa mahakamani, Chiligati na Mrema watajwa!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Isango, Apr 3, 2012.

 1. I

  Isango R I P

  #1
  Apr 3, 2012
  Joined: Jul 23, 2008
  Messages: 295
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  [h=2] [/h][h=2]Na,Jumbe Ismailly,Singida Apr,03,2012 Mahakama kuu[/h][h=2]Kesi ya kupinga matokeo ya Lissu yaibukika mambo mazito.[/h][h=2]Chiligati atajwa kuhusika kuandaa ushahidi,[/h][h=2]Mrema na mwanae watumika kusaidia CCM kumpinga Lissu,[/h][h=2]Mashahidi waingia tena mitini, jaji aamuru walalamikaji walipe gharama kwa uzembe[/h][h=2] [/h][h=2]KESI ya kupinga matokeo ya uchaguzi yaliyompa ushindi wa ubunge wa jimbo la Singda mashariki (CHADEMA),Bwana Tundu Lissu jana na iliibua mambo mapya baada ya mshitakiwa wa kwanza katika kesi hiyo kutoa waraka Mahakamani ulioandikwa na aliyekuwa Katibu wa Halmashauri kuu ya Taifa,Itikadi na Uenezi,Kapteni Mstaafu John Chiligati[/h][h=2]Kwa mujibu wa barua hiyo yenye kumbukumbu namba CCM/OND/559 VOL.II/10 ya machi,23,2011 iliyoandikwa na kusainiwa na John Chiligati iliomba kufahamu kama ni kweli TLP iliweka mawakala katika jimbo la uchaguzi la Singida mashariki,au kama mihuri iliyotumika ya TLP ilikuwa ni sahihi au ni ya kughushi[/h][h=2]Pamoja na barua hiyo kuna barua nyingine pia iliyotoa majibu kwa Chiligari ambayo iliwasilishwa Mahakamani hapo na Bwana Tundu Lissu iliyotoka kwa Hamadi R.Tao aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa TLP,yenye namba TLP/HQ/VOL.V/165 iliyokiri kuwa mawakala wa TLP hawakuteuliwa au kama waliteuliwa utaratibu haukufuta taratibu za chama.[/h][h=2]Hata hivyo barua ya TLP ilipingana vikali sana na barua ya Mwenyekiti wa TLP wilaya ya Singida iliyoindikwa kumjibu katibu wa TLP Taifa ya apr,12,2011juu ya mawakala hao kusimamaia katika uchaguzi mkuu bila malipo[/h][h=2]Hata hivyo mjadala wa mahakamani ulikuwa Mkubwa, baada ya Shahidi wa 19, Bw. John Madindilo, ambaye ni Mwenyekiti wa TLP Mkoa wa singida kukubaliana na hoja zote za Lissu, na kumtaja Mtoto wa mwenyekiti wa TLP Taifa,Bwana Augustino Mrema, Bwana Michael Mrema kuwa alitumwa singida kama afisa wa Chama kwenda kufuatilia suala hilo,hata hivyo alipopewa taarifa hiyo, hakuridhika nayo badala yake aliwaelekeza wale viongozi wa Singida, kuandika barua kwa Katibu Mkuu kadiri itakavyompendeza Mwenyekiti wa TLP, Augustino Mrema.[/h][h=2]Baadhi ya mahojiano yalikuwa kama ifuatavyo: Baina ya Tundu Lissu na SHAHIDI, JOHN MADINDILO[/h][h=2]T/L Ni kweli au si kweli kuwa ulikasimu madaraka kwa Mwenyekiti wa TLP wa wilaya ya Singida, kwa kuwa wewe ulikuwa Mgombea, na Mwenyekitji wa Wilaya ya singida, ulimwamini, kwa uwezo wake na uadilifu , na uzoefu wake?[/h][h=2]P/W:NDIYO NILIFANYA HIVYO LAKINI YEYE PIA YUPO MAKAO MAKUU YA MKOA HAPA MJINI.[/h][h=2]T/L Ni kweli au si kweli kuwa mliweka mawakala kulinda maslahi ya Chama,[/h][h=2]P/W NI kweli,[/h][h=2]T/L Ni sahihi au siyo sahihi, mnapokuwa na Mgombea urais, huwa mnaweka mawakala?[/h][h=2]P/W NI KWELI, pale ambapo mawakala wanakuwa tayari kujitolea.[/h][h=2]T/L Ni kweli au si kweli kuwa kwa mujibu wa barua ulizo nazo, kesi hii ipo kwa maslahi ya Chiligati na Mrema?[/h][h=2]P/W Ni kweli kwa mahusiano ya barua hizi walizoandikiana.[/h][h=2]T/L Kama nimekusikia vizuri uliiambia mahakama hii kuwa kuna Afisa wa Chama anakuja toka Mkao makuu, umpokee na umpe ushirikiano?[/h][h=2]P/W NI kweli.[/h][h=2]T/L Je huyo afisa wa chama alikuwa anaitwa nani?[/h][h=2]P/W: Siruhusiwi kumtaja[/h][h=2]JAJI: Kama umemtaja Augustino Mrema, Mwenyekiti wa TLP Taifa ni Afisa gani unashindwa kumtaja[/h][h=2]P/W: ni Mikaeli Mrema.[/h][h=2]T/L. Mikaeli Mrema ambaye ni mtoto wa Augustino Mrema?[/h][h=2]W/P.NDIYO[/h][h=2]T/L. Mikaeli Mrema alisema nini?[/h][h=2]P/w; alisema kuwa kulikuwa na mawakala hewa wa TLP waliwekwa Singida mashariki?[/h][h=2]T/L. Hukushangaa kupokea taarifa ya Malalamiko toka makao makuu wakati wewe Mwenyekiti wa Mkoa huna taarifa yeyote?[/h][h=2]P/W: NILISHANGAA SANA lakini nilipokea kwa kuwa inatoka kwa Mkubwa wangu wa Kazi.[/h][h=2]T/L: Nimeshtakiwa hapa, kwa mujibu wa barua mbalimbali ulizosoma, wanaitaka Mahakam itengue matokeo ya uchaguzi, kwa mujibu wa ufahamu wako, unasemahe juu ya hili?[/h][h=2]P/W: watakuwa wanakuonea.[/h][h=2]Kesi hiyo haikuendelea mchana, baada ya upande wa walalamikaji kushindwa kuleta Mashahidi mahakamani, kitendo kilichopelekea jaji kuwapiga faini ya kulipa nusu gharama ya siku katika kesi hiyo:[/h][h=2]Na mahojiano yalikuwa hivi:[/h][h=2]Wakili wa walalamikaji; Mheshimiwa jaji, naiomba Mahakama iahirishe kesi hii hadi kesho kwa kuwa shahidi wetu hajaja, na amefunga simu,[/h][h=2]JAJI: Ulichukua hatua kuleta shahidi mmoja tu?[/h][h=2]Wakili: huwa tunachelewa kutoka mahakamani, hivyo inakuwa vigumu kuwatafuta kwa siku inayofuata. Hata hivyo kazi ya kutafuta mashahidi sio yangu ni ya wateja wangu.[/h][h=2]TUNDU LISSU: Mheshimiwa jaji, uchelewashaji unaofanywa kwa makusudi unaniathiri mimi, kwanza kiuchumi kwa kuwa nakaa hotelini, pili ninashindwa kushiriki kazi za kibunge, na ninashindwa kuwatumikia wanachi wangu walionichagua. Siku nyingine ulinionya nisidai gharama, leo mheshimiwa jaji, naomba upande wa walalamikaji walipe gharama,[/h][h=2]Jaji: Mlalamikaji naomba usimame, unajua kuwa katika kesi hii mimi nalipwa na serikali, na hawa wanasheria watatu wa serikali, na katibu wangu?[/h][h=2]MLALAMIKAJI: NDIO,[/h][h=2]JAJI: mbona hampo ‘serious’ . Kuna uzembe mkubwa unatokea na leo hii sitaki kukubali kirahisi uzembe huu. Kuna uzembe unafanywa na walalamikaji, na tayari nilionya hili tangu mwanzo. Mtumzembe hukumbushwa na leo naamuru mtalipa nusu gharama ya ahirisho la kesi leo kwa uzembe wenu ili mjitume na mjue wajibu wenu sio kutupotezea muda hapa.[/h][h=2] [/h][h=2]Kesi hiyo iliahirishwa mpaka kesho (LEO) saa 3 asubuhi[/h]
   
 2. Limbani

  Limbani JF-Expert Member

  #2
  Apr 3, 2012
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 1,438
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Wanapoteza muda wa mahakama tu, hakuna kesi hapo!!
   
 3. M

  MpendaTz JF-Expert Member

  #3
  Apr 3, 2012
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 1,579
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Tuletee yaliyojiri leo tafadhali.
  Natanguliza shukrani zangu
   
 4. Pelekaroho

  Pelekaroho JF-Expert Member

  #4
  Apr 3, 2012
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 1,502
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 160
  Kesi ya Lisu leo imeendaje?
   
 5. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #5
  Apr 3, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Hapo kwenye red. Mi nataka kujua hizo gharama ni Shilingi ngapi?
   
 6. 1800

  1800 JF-Expert Member

  #6
  Apr 3, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 2,217
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Kama mpaka jaji katamka walalamikaji ni wazembe,basi wajue hakuna cha msingi hapo,!hv huyu mp***i A. Mrema nae kumbe ni kweli anafanya kazi za c.c.m?kweli kilaza mwenye njaa ni kilaza tu,na 2015 asahau kabisa ilo jimbo,maana yeye na Lusinde wamewa angusha sana wapiga kura wao!leo nilikua nasikiliza radio station fulani,kweli iliniacha nacheka tu kwa jinsi huyo kilaza Lusinde ambavyo amekua kichekesho midomoni mwa Watanzania,amewafanya walimchagua kua mbunge wao na waliomteua kwenda Arumeru,waonekane nao ni vilaza tupu kama yeye!
   
 7. c

  ckcacana Member

  #7
  Apr 3, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ni haki yao walalamikaji kulipa fidia.
   
 8. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #8
  Apr 3, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,816
  Likes Received: 330
  Trophy Points: 180
  Kesi ndio inaishia hivyo,mshnd amejulikana tayari!
   
 9. BASHADA

  BASHADA JF-Expert Member

  #9
  Apr 3, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 487
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Namwonea huruma tundu lissu, wanampotezea muda wake bureeee ili 2015 waseme hajawatekelezea wananchi ahadi alizotoa, hapo hakuna kesi
   
 10. J

  JuliusPm Member

  #10
  Apr 3, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Duh kweli apo hakuna kesi,wanapoteza muda kwa. Mbunge wetu.
   
 11. T

  Twins New Member

  #11
  Apr 3, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kesi imeendeleaje leo? please we need results.
   
 12. MANYORI Jr

  MANYORI Jr Member

  #12
  Apr 3, 2012
  Joined: Mar 25, 2012
  Messages: 63
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Hao waganganjaa,wajambia limao na vilaza watajuta kumfaham lisu.TLP,CCM kwisha kaaaazi...
   
 13. t

  tiamo New Member

  #13
  Apr 3, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  lisu wasikupotezee muda wako next time wadai fidia
   
 14. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #14
  Apr 3, 2012
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Mkuu Isango,
  Tunaomba updates kuhusu mambo yalivyoenda leo, ie kama gharama imelipwa na ni TSh ngapi, na mambo yote yaliyojiri!
   
 15. S

  SILVANUS NJENGA Senior Member

  #15
  Apr 3, 2012
  Joined: Feb 8, 2012
  Messages: 174
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kumbe KIBONGO-BONGO kuna watu wanaweza kuchezea-zea Mahakama kihurahisi hivi!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 16. S

  Shiefl Senior Member

  #16
  Apr 3, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 145
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wenda wazimu hawa. Na tukimaliza kesi watalipa gharama zote ndio wajue kuwa kesi siyo za kufungua tu
   
 17. Ork

  Ork Member

  #17
  Apr 3, 2012
  Joined: Mar 23, 2012
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Jamani leteni updates za Kesi ya Tundu Lissu. Naona wanacheza tu na mahakama na kumpotezea muda Lissu.......
   
 18. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #18
  Apr 3, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  soma vizuri ulichoandika. Nadhani hukutumia akili yako!
   
Loading...