Mazito ya Maige, Mwangunga yaibuka - sasa watuhumiwa kupoteza bil. 300/- | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mazito ya Maige, Mwangunga yaibuka - sasa watuhumiwa kupoteza bil. 300/-

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by palalisote, Jun 1, 2012.

 1. palalisote

  palalisote JF-Expert Member

  #1
  Jun 1, 2012
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 8,352
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  MAWAZIRI wawili wa zamani katika Wizara ya Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige na Shamsha Mwangunga, wanatuhumiwa kuliingizia taifa hasara ya sh bilioni 300, kwa kutumia madaraka yao vibaya.Tuhuma hizo nzito zimetolewa jana na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), Deo Filikunjombe, ambaye alidai hasara hiyo kubwa imetokana na uzembe uliofanywa na mawaziri hao wa zamani wakati wakiiongoza wizara hiyo.

  Akizungumza jana na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mara baada ya kumalizika kwa kikao cha kamati hiyo na watendaji wakuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya Taifa (Tanapa) Filikunjombe ambaye ni mbunge wa Ludewa (CCM) alisema kuwa Mwangunga ambaye alikuwa waziri, huku Naibu wake akiwa ni Maige, waliizuia mamlaka hiyo kutoza tozo zinazotolewa katika hoteli za kitalii kwa muda wote waliokuwa madarakani.Alisema uzembe huo umeathiri kwa kiasi kikubwa utendaji wa serikali na iwapo shughuli hiyo ingeachiwa hifadhi hiyo ya taifa kwa mwaka wangeweza kukusanya kiasi cha sh bilioni 21.

  “Pamoja na kuwa taarifa yao ni nzuri lakini sisi kama kamati tumegundua uzembe uliofanywa na Mwangunga pamoja na Maige juu ya jambo hilo maana fedha hizo zingeweza kujenga barabara na shule kila maeneo,” alifafanua.Alisema matatizo mbalimbali yanayolikabili taifa hili yanachangiwa kwa kiasi kikubwa na wanasiasa hivyo aliwataka kuacha shughuli za mashirika kufanywa na bodi walizonazo.“Matatizo mengi yanayojitokeza ni kutokana na wanasiasa kuingilia moja kwa moja shughuli zinazofanywa na mashirika kama ambavyo tumeliona hili lililowapata TANAPA ambapo kuna maamuzi ya kisiasa yaliyofanywa na Mwangunga pamoja na Maige,” alisema.Alisema kipindi cha uwaziri wa Maige alishindwa kulipatia ufumbuzi suala hilo kwani alilichochea hatua iliyohamasisha waliokuwa wakipinga uamuzi huo kukimbilia mahakamani.


  Alisema hadi sasa TANAPA imepata kiasi cha sh bilioni 4 pekee katika tozo za hotel hizo zilizo katika hifadhi mbalimbali nchini, hivyo kamati imeazimia kukutana na wizara hiyo ili kuangalia namna ya kulishughulikia tatizo hilo.Machi 21, 2011 wizara hiyo ilitetea sakata hilo la tozo huku ikimkingia kifua aliyekuwa Waziri Ezekil Maige kuwa hausiki na jambo hilo.Katika taarifa hiyo ambayo ilitolewa na msemaji wa Wizara hiyo George Matiko, ilieleza kuwa mtangulizi wa Maige katika wizara hiyo Shamsa Mwangunga, ndiye aliyekubaliana na pingamizi la wadau ambao hawakukubaliana na ongezeko hilo na kuliagiza shirika la hifadhi za taifa (Tanapa) kusitisha utekelezaji wa tozo mpya.

  Alisema Tanapa katika mwaka wa fedha 2008/09 lilipendekeza kuongezwa kwa tozo za watalii wanaolala katika hoteli na kambi za wageni ndani ya hifadhi za taifa na kwamba ongezeko hilo lilifuatia vikao vya pamoja kati ya shirika hilo na wadau mbalimbali katika sekta husika na wengi wao walikubaliana na ongezeko hilo.Kwa mujibu wa Matiko, wadau wachache katika sekta hiyo ya hoteli hawakuridhika na uamuzi huo wa kuongeza tozo hilo na waliamua kupeleka suala hilo wizarani wakitaka kusitishwa kwa uamuzi huo wakidai kuwa utaathiri biashara zao.Kuibuka kwa tuhuma hizo kumezidi kuwaweka waliokuwa mawaziri wa wizara hiyo katika wakati mgumu wa kujinasua na sakata nzito zinazojitokeza kila siku.

  Habari kwa hisani ya tanzania daima
   
 2. f

  falesy Senior Member

  #2
  Jun 1, 2012
  Joined: Mar 15, 2006
  Messages: 105
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwa nchi yetu kila kitu kinawezekana na kila mtu anaweza kushika nafasi yoyote. Tatizo nililo nalo ni weledi wa kila anayepewa nafasi ya juu serikalini maana mtu anaaminiwa, anapewa kila kitu na kulipiwa hadi ada za shemeji zake yet anahujumu taifa! Mifumo yetu ya kupata viongozi ina mushkeli na hili litaendelea kutughalim kama watu wenye nia safi wataendelea kuwa watazamaji na majizi yakaendelea kugombea nafasi mbalimbali!!

  Naipenda TANGANYIKA
   
 3. Puppy

  Puppy JF-Expert Member

  #3
  Jun 1, 2012
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 2,276
  Likes Received: 664
  Trophy Points: 280
  Shamba la Bibi.
   
 4. F

  FJM JF-Expert Member

  #4
  Jun 1, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Tuna tatizo kubwa sana tena sana la mfumo wa uendeshaji na usimamizi wa mashirika ya umma. Hizi board zinazoundwa ndizo zinaleta matatizo makubwa kwenye haya mashirika. Zina nguvu mno na mara nyingi wataalam wanakosa la kusema. Tulisoma saga ya Msekwa na Ngorongoro, ni mkurugenzi gani atakamtalia jambo Msekwa?

  Lakini pia, wabunge wanatakiwa watoke kabisa kwenye hizi boards. Hii ni conflict of interest.
   
 5. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #5
  Jun 1, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Du maige mwaka wake huu!!
   
 6. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #6
  Jun 1, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  zitto akisema haeleweki!

   
 7. B

  Bob G JF Bronze Member

  #7
  Jun 2, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 2,354
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Kamata Maige Na Mwangunga peleka kotini ili akome kumpakazia Nape, Hivi TAKOKURU mpo! au ndo mwendesha mashitaka kakalia file? Tanzania kila mtu ni rais kwenye ka taasisi kake USIMGUSE
   
 8. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #8
  Jun 2, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,326
  Likes Received: 1,792
  Trophy Points: 280
  Maige aangalie, hili kuti kavu linaweza kumtulia kichwani
   
 9. L

  Ludewa JF-Expert Member

  #9
  Jun 2, 2012
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 215
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  huyu filikunjombe ni mbunge wa CCM kweli?
   
 10. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #10
  Jun 2, 2012
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Halafu ndiyo huyo anapita kulalamika kila mahali kwamba ameondolewa uwaziri kutokana na wivu? Kwanini asinyamaze kama mwenzake Ngeleja?
   
 11. N

  Ndjabu Da Dude JF-Expert Member

  #11
  Jun 2, 2012
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 3,652
  Likes Received: 409
  Trophy Points: 180
  Mwandishi au huyo Filikunjombe wameshindwa kuonyesha ushahidi wa jinsi hasara ya hiyo Bilioni 300 ilivyopatikana. Maneno makubwa meengi lakini hakuna substance yoyote kwenye habari hii zaidi ya hiyo figure ya kutisha ya hasara ya "bilioni 300".
   
 12. i

  iMind JF-Expert Member

  #12
  Jun 2, 2012
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 1,907
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  Umeona enhee. Filikunjombe ni mropokaji. Hili sakata ni la muda mrefu. TANAPA siyo kwamba walikuwa wanataka kuongeza viwango vya tozo bali walitaka kubadilisha mfumo mzima wa kutoza tozo ya watalii wanaolala kwenye hotel za hifadhi. Kwa kawaida tozo ya kitanda huwa asilimia fulani ya bei ya kulala, wao walitaka wafanye fixed rate eti hotel ziwe zinalipa kiwango fulani kwa mwezi bila kujali idadi ya wageni waliolala. Hili ndo lilikataliwa na Mwangunga alisitisha, Maige alipoingia akaruhusu, wafanyabiashara wenye hotel wakaenda mahakamani. Mahakama ikazuia hadi sasa kesi inaendelea.
  Mtazamo wangu ni kwamba TANAPA walichemka. Wanata kuongeza mapato kwa nguvu. Haingii akikini ukatoza tozo ya mtalii kulala at a fixed rate bila kujali idadi ya watalii walio lala naa kiasi walicholipia. Haitakua tena bed night levy but something else.
   
 13. i

  iMind JF-Expert Member

  #13
  Jun 2, 2012
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 1,907
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  Hii haina mshiko. kesi iko mahakamani.
   
 14. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #14
  Jun 2, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Walikuwa wapi kuyaona na kuchukua hatua?we are tide na hizi bla bla! ule msemo wa hujafa hujaumbika upo very live katika siasa za bongo
   
 15. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #15
  Jun 2, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Wanataka kumziba mdomo kwa vile anawasumbua kichwa kwa kuwa walikuwa wanakula wote halafu yeye katolewa kafara.
   
 16. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #16
  Jun 2, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Alafu kuna watu wanadiliki kusema Filikunjombe ni mropokaji!
  Sisi tulio jikoni tunasema watz itachukua mda sana kuamka na umaskini utaongezeka!
   
 17. S

  Sometimes JF-Expert Member

  #17
  Jun 2, 2012
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 4,567
  Likes Received: 360
  Trophy Points: 180
  Akili ya kuambiwa changanya na ya kwako! Kama ungekuwa mfuatiliaji mzuri kwenye vyombo vya habari, taarifa hii ilitangazwa jana usiku na TV flani ya hapa nchini!
   
 18. Mpui Lyazumbi

  Mpui Lyazumbi JF-Expert Member

  #18
  Jun 2, 2012
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 1,853
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Watakuwa wameisikia hii, ngoja tusubiri majibu. Kaaazi kwelikweli.
   
 19. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #19
  Jun 2, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  wanasiasa wanatuvuruga sana, katiba mpya itabidi ijikite kwenye kuupa nguvu utaalamu na hawa wanasiasa wabaki kuwa observers.. penye siasa daima hakuna maendeleo
   
Loading...